Nikikumbuka ile siku tulimdanganya mwenzetu akakanyagwa kichwa na gari bado naumiaga sana

wa stendi

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
17,484
2,000
Sitokaa nisahau siku hiyo ilikuwa tarehe 24 mwezi 12 kulikuepo na kipaimara kijijini kwetu basi siku hiyo nyumba ya jirani kulikuwa na sherehe kuubwa hivyo magari mengi mengi yalikuja siku hiyo.

Basi kwa kuwa sisi bado wadogo wadogo ndio mara ya kwanza kuona au kushangaa gari likirudi nyuma (rivers)linapiga alam fulani hivi,siku hiyo katika kushangaa magari si (si mnajua tena kijijini?)basi kulikuwa na gari likirudi nyuma kuna mlio wa mtoto analia(ile alam likirudi rivasi)basi sisi tukisikia hivyo tunafurahi tunachekaaa basi katika lile kundi letu mtoto mmoja akasema nikichungulia nitamwona?mi nikamwambia huwezi kumwona hadi uingie huku chini mvunguni kabisa ndio kafichwa huko.

Basi lile gari likaondoka ile baadae likarudi tena kumbe lilikuwa linaenda kuchukua wageni stendi na kurudi (si mnajua tena kijijini stendi inakuwa mbali kidogo?)basi lile gari pale lilipopaki tukawa hatuchezi mbali ili likirudi rivasi tusikie mtoto anavyolia,basi pale nilimdanganya yule mwezangu ingia huko mvunguni jifiche huko mpaka dereva aje akivasha tuu gari utamwona mtoto .basi na sekunde chache tuu dereva akaja akaingia ile kuwasha yule dogo katika ule woga wa mtikisiko wa gari lilovuowaka si akajiachia?basi nilichoona lile gari lilivyorudi nyuma ni ile tyre ya mbele kama ilipanda jiwe fulani au tuta huku gari likirudi nyuma daaaa....

Ngoja nilie kwanza lile tukio kama nimeliona tena
Narudi baadae naingia lunch kwanza karibuni ...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom