Nikikaa kwenye biashara ya mtu, siku hiyo lazima wateja wawe wengi. Nini siri ya hii hali?

Watu wa hivyo wapo sana wala sishangai.

kuna dogo mmoja tulimtoa bush huko akaletwa Dar kuuza Duka!

Kabla ya Dogo kuja mauzo yalikua laki 2 max.

Baada ya Dogo kuja biashara ikaanza kupaa mdogo mdogo, anauza peke yake mpaka laki 9 wakati mwingine anagonga hadi milioni.

Ule mtaa ulikuwa na maduka kama 10 hivi lakini cha ajabu wengine wakawa wanauza kidogo sana kulinganisha na duka alilokuwa dogo.

ikafikia hatua akaitwa msukule.

basi Bwana walimwengu hawana wema kabisa, Dogo kafanya kazi kwa Moyo, kuamka saa kumi alfajiri, kulala saa sita usiku lakini cha ajabu boss akamzulumu mshahara wa miezi mitatu

Dogo kaona isiwe shida, katoroka dukani na kama laki 1 hivi, elfu 60 ya tiketi mpaka kwao, 40 ikawa ya emergence..

Dogo kaamsha mpaka kwao kijijini huko kaacha Duka.

Wiki nyingi aisee wateja wakaanza kupungua, mmoja baada ya mwingine, duka likaporomoka kwa speed ya airforce

Boss kaamua kubembeleza tena ili Dogo arudi...

Dah ntarejea..
 
Kuna mwanamama mmoja ni mchepuko wangu wa kitambo sana,mara nyingi yeye ndo anayenitafuta mm kwa ajili ya shughuli na anagharamia kila kitu,kuna siku alinikera nikavunja mahusiano nae,alihangaika sana yule mama hadi kwa ndg zangu alifika kutaka aombewe msamaha,mwisho wa siku akaniambia nilivyokuwa na ww biashara yangu ilishamiri sana ila toka uniache sina ninachofanya,nilivyorudisha mahusiano biashara iko juu,tena anapenda ile asubuhi na mapema tunapita sehemu anapata cha asbh ndo anaenda kwny mishe zake hapo anakwambia siku nzima ni kuvuna pesa tu.
 
Kwa bahati hiyo uliyonayo mimi hata tuwe mia aisee... ;)
Tatizo natajirisha wenzangu mimi nabaki kuwa tajiri wa roho... Yaani hata bajaji nikiingia akikomaa kusubiri abiria wengine namwambia twende wasipopatikana nitalipa hiyo buku jero yao. Mita 20 tu anaanza kuwaokata hadi anajaza. This is weird!
 
Tatizo natajirisha wenzangu mimi nabaki kuwa tajiri wa roho... Yaani hata bajaji nikiingia akikomaa kusubiri abiria wengine namwambia twende wasipopatikana nitalipa hiyo buku jero yao. Mita 20 tu anaanza kuwaokata hadi anajaza. This is weird!
Hivi hii ni kweli CREOLE maana sasa naanza kuwa serious, wewe ni kiumbe adimu... :)
 
Habari wana great thinker

Nina hii hali, nikikaa kwenye biashara ya mtu mfano duka siku hiyo lazima wateja wawe wengi.

Hi hali huwa ina nitokea hata nikiwa bar. Hata kama bar hiyo haina wateja lakini siku nikichukua muda na kukaa sehemu hiyo hata kama sinunulii mtu kinywaji lazima wateja wajae.

Hii hali imekua ikinitokea mara nyingi ndugu zangu wana great thinker naomba kujua nini chanzo cha hii hali
Karibu kwenye biashara yangu.
 
Back
Top Bottom