Nikijiuzulu jimbo langu (Moshi rural) litakwenda chadema -Dr. Chami

Nipo hapa kata ya Ukaoni, tarafa ya Kibosho, jimbo la Moshi (V). Nimewasomea vijana hii thread pakaharibika. Wamenigeukia utadhan ni maneno yangu. Wanalalamika jamaa alichakachua kwenye kura za maoni wakaamua kumtosa kwenye uchaguzi nako akachakachua. Ila wanasema kwamba safari hii watapiga kura na kuzilinda. Natamani mngekijua kikibosho ndio mngeelewa hasira zao! Chaaa!?

Ni kweli hata mie wakati wa uchaguzi nilikuwa huko jamaa hasa vijana wengi hawampendi na nilishangaa alivyokwepa viunzi vyao,
 
Tujuavyo JK ndiye anawang'ang'ania hawa vilaza,sasa sijui kama na yeye ni mkibosho!!?

nakwambia nipo kibosho na jamaa hawamtaki kabisa! Hawakumchagua japo ni Mnama ,na wanashangaa ameshindaje?
 
Chagueni watu kama akina ndesa pesa mnababaika na cv haya oneni matokeo yake.
 
kwa mtu yoyote anayetaka kugombea ubunge kupitia ccm asikanyage kanda ya kaskazini....moshi arusha mwanza... labda wakimbilie kanda ya kusini ndio angalau ccm bado ina nguvu
 
Ni kweli hata mie wakati wa uchaguzi nilikuwa huko jamaa hasa vijana wengi hawampendi na nilishangaa alivyokwepa viunzi vyao,

WanaJF naomba mnijuze suala hili, kwamba ni vipi waziri anapovuliwa uwaziri wake kwa vitendo vya ubadhirifu na ufisadi anaendelea kuwa mbunge wakati hivyo ni vitendo vya jinai? Kwa wadhifa wa mbunge naye ni mjumbe wa baraza la madiwani ktk halmashauri yake ambalo hupitisha maamuzi mbalimbali, je huko hawezi ku-influence vitendo vyake vya ufisadi kwa wengine? cha kushangaza ni kwamba mbunge anapovuliwa uanachama kwa sababu zozote zile au anapoamua kwa hiari yake kujivua uanachama katika chama chake moja kwa moja hupoteza ubunge wake. Hii wanaJF imekaaje!!!aliyekuwa waziri fisadi anaendelea kuwa mbunge, anayepoteza uanachama wa chama chake hata kama ni muadilifu anapoteza ubunge. Hii ina-contradict.
 
Nani kamwambia kwamba CHADEMA ni maadui! kwanza watu wa Moshi hawajapata faida kwa yeye kuwa waziri! sasa anataka hati miliki ya kuwa mbunge?
 
alikuwa anasema ukweli kuwa akiondolewa kwenye chama kwa sasa na kuingia kwenye uchaguzi mwingine ni lazima jimbo lile lihamie chadema huu ni ukweli hivyo anaomba hifadhi ya jimbo walau mpaka 2015 ndo chadema walichukue.
 
alikuwa anasema ukweli kuwa akiondolewa kwenye chama kwa sasa na kuingia kwenye uchaguzi mwingine ni lazima jimbo lile lihamie chadema huu ni ukweli hivyo anaomba hifadhi ya jimbo walau mpaka 2015 ndo chadema walichukue.

hakuwa anaongopa hata kidogo!! Niliwahi kuzungumza na rafiki yangu mmoja wa old moshi alinihakikishia kwamba ....ikiwa uchaguzi utaitishwa leo jimbo la moshi vijijini litakwenda chadema. Alizidi kidadavulia kuwa jimbo ambalo sisiem ina uhakika nalo kutoka na mbunge wake kukubalika ni jimbo la siha peke yake.....katika majimbo yaliyo uchagani!!!!
 
Anajitetetea badala ya kuwajibika kwa manufaa ya wapiga kura wake na wananchi wa Tanzania.

Namshangaa sana Kikwete kwanini anawaomba wajiuzulu badala ya kuwafukuza kazi.
Ningelikuwa Jk, I should have get rid of them, sina mkataba na panya mimi!

Kwako ni panya, kwa Kikwete ni tools. The difference can't be much obvious!
 
Anajitetetea badala ya kuwajibika kwa manufaa ya wapiga kura wake na wananchi wa Tanzania.

Namshangaa sana Kikwete kwanini anawaomba wajiuzulu badala ya kuwafukuza kazi.
Ningelikuwa Jk, I should have get rid of them, sina mkataba na panya mimi!
Like!!!
 
Watu bwana kwani amefanya nini cha maaana mpaka aogope jimbo kuchukuliwa na cdm .aende zake mwizi mkubwa huyo
 
Watu wengine utadhani wanazungumza kama hawana kichwa vile,hakuna mwenye hati miliki ya jimbo,kama ameshindwa kutumia fursa aliyokuwa nayo akiwa waziri kwa kushawishi wawekezaji kujenga viwanda Moshi ndo basi tena.Wakiboshowengi asili yao ni mabucha ndo kazi wanayoiweza
 
Huyu nae ni kundi lile lile la mwaka 47 wanaofikiri ccm bado itaendelea 2015 . Wakati paa lake linavvuja kwa kazi ya mapipa kimbunga kimeikumba ccm watu hawaelewani
 
Hili jamaa zembe hili ni mbunge wangu wa kulazimishwa! yan ni zembe kupindukia, mi siishi moshi ila nimejiandikiha moshi na huwa naenda kupiga kura moshi, yan cjui kwa nini wakibosho wanamng'ang'ania huyu jamaa zembe kiasi hichi. Hakuna cha maana alichokifanya na uwaziri wake. Angalau angemleta mwekezaji mmoja ajenge kiwanda kule Moshi (V), yan limebweteka tu na uwaziri. Yan kwa kweli safari hii lazima tumle kichwa. Hana msaada kwa wananchi wa Moshi V, Mbona Ndesamburo Moshi (M), amefanya mambo yanayooneka mf, ameshinikiza lami kutoka YCMA hadi RAU, ameomba jengo lililokua kiwanda cha pamba zamani ajenge kiwanda kanyimwa, amechimba visima vya maji n.k, yeye huyu waziri anashindwa nini kufanya mambo ili nasi tujivunie uwaziri wake? Bora hata mramba alijenga barabara kule Rombo, japokua ni fisadi

i concur with you!
 
Back
Top Bottom