Nikijibiwa tu haya Maswali yangu mawili ambayo huwa ‘ yananichanganya ‘ mno nitakuwa na Siku njema sana

DuppyConqueror

JF-Expert Member
Mar 30, 2014
9,442
2,000
Swali Namba Moja.

Hivi ni lazima kila ‘Spymaster ‘ akistaafu au akitumbuliwa Kazini ateuliwe kuwa Balozi?

Swali Namba Mbili

Kama bado huwa hatujui Vituo vya Kazi vya Mabalozi Wateuliwa kwanini huwa tunaanza Kuwatangaza?

Nayasubiri majibu yenu kwa hamu zote Wana Ndugu wa JamiiForums.
Fanya tafiti kwanza.
Col Dr. Hassy Kitine, Apson Mwang'onda au Rashid Othman walipelekwa ubalozi upi?
 
GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
36,842
2,000
Balozi kupangiwa kituo ni mpaka jina lake lipelekwe huko anakotakiwa kwenda na wakilikubali kituo kinatangazwa. Wao wanafanya pia vetting. Mfano hapa kwetu awamu ya nne kuna balozi alikataliwa kwa vile ni shoga.
Ni yule aliyetakiwa kwenda Taifa lenye Watu wenye Akili nyingi kuliko wengine ( hasa Barani Afrika ) la Rwanda au?
 
kookolikoo

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
2,607
1,500
Uteuzi wao uko palepale. Nchi X ikimkataa balozi A atapangiwa nchi Y na balozi B atabadilishwa na kupelekwa huko. Reshuffle itaendelea hadi wateule wote wapate vituo. Ni lazima uteuzi wako utangazwe ndiyo jina lipelekwe na sio vinginevyo.
Kwa nini wasiwatangaze baada ya kukubaliwa na hizo Nchi?
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
35,813
2,000
1. Sio kila spymaster hupelekwa ubalozini, kwa Tanzania, tangu tumepata uhuru tumekuwa na ma Spymasters 7, kati ya hao, ni mmoja tuu aliyepelekwa ubalozini ni Hassy Kitine, Kipilimba ni wa pili. Ila pia kuna ma Master Spy waliopelekwa ubalozini akiwemo Dr. Mahiga na Jack Zoka, pia kuna uwezekano pia kuna wengine, ukiwa sii mmoja wao, huwezi kuwajua ila balozi zote huwajaza watu hao.
2. Mtu kuteuliwa Balozi ni jambo moja, na kupangiwa kituo ni jambo jingine. Ubalozi ni cheo, mtu anaweza kuteuliwa balozi na asipangiwe kituo.

Jambo kama hili hufanyika hata polisi hata jeshini, askari wanapandishwa kwanza vyeo, kisha ndio wanapangiwa vituo.

Hata wewe ulipoingia sekondari, kwanza matokeo yanatoka, umefaulu, kisha selection inatoka umepangiwa shule fulani, na ukiisharipoti shuleni ndipo unapangiwa darasa.
P
 
GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
36,842
2,000
nani ajibu maswali ya kitaahira, tafuta kazi acha upuuzi
Na bahati nzuri hasa Wewe ndiyo ukiwa Rais wa Matahaira wote duniani. Kazi ninayoitaka ni ya Kukufundisha Wewe kuwa na Akili na kuacha ' Upumbavu ' unaokusumbua 24/7. Je unaweza ukaniajiri ili Kipato utakachonipa Kiweze Kunisadia Kimaisha hasa nikiwa kama Fukara na ambaye nataabika na Maisha?
 
GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
36,842
2,000
1. Sio kila spymaster hupelekwa ubalozini, kwa Tanzania, tangu tumepata uhuru tumekuwa na ma Spymasters 7, kati ya hao, ni mmoka tuu aliyepelekwa ubalozini niHassy Kitine, Kipilimba ni wa pili. Ila pia kuna ma Master Spy waliopelekwa ubalozini akiwemo Dr. Mahiga na Jack Zoka, pia kuna uwezekano pia kuna wengine, ukiwa sii mmoja wao, huwezi kuwajua ila balozi zote huwajaza watu hao.
P
Mbona kuna ' Spy Masters ' wengine lakini walipewa tu Vyeo vya Ubalozi huko nyuma hasa Awamu ya Rais Mstaafu Mwinyi hadi ile ya Rais Mstaafu Mkapa lakini hawakuwahi Kupangiwa Vituo vya Kazi? Kama Wewe ni ' Mfukunyuku ' na Mwandishi wa Habari wa Ukweli utakuwa unawajua na kama hadi leo huwajui basi nitatilia mno shaka uwezo wako Kitasnia japo Kitaaluma unaweza uko vyema ukizingatia ninakujua ' Kindakindaki ' Ndugu.
 
technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
9,416
2,000
90% Ya Mabalozi Sio Tu Kwa Tanzania Bali Nchi Nyingi Duniani Uwa Wanakuwa Watu Wa Idara Za Usalama Za Nchi Zao.

Sema Kosa Tunalofanya Ni Kupeleka Maafisa Abao Tayari Nchi Izo Zinawatambua Kwa Tittle Ya Kazi Zao Uko Nyumbani. Watawapa Ushirikiano Lakin Vile Vile Watakuwa Kweny Rada Ya Kuchunguzwa Kutokana Na Nchi Usika Afsa Aliyoko.

Ila Kupelekwa Kwa Kapilimba Nje Ya Nchi Ni Kuthibiti Nguvu Ya Membe Kuelekea Uchaguzi 2020 Wala Sio Kwa Maslai Ya Taifa.

Na Magufuli Apa Ndio Nimeona Kwamba Jamaa Ana Intelijensia Ambayo Sio Mchezo

Ningekuwa Karibu Na Membe Ningemshauri Aachane Na Mawazo Aliyonayo Awaache Vijana Wasio Na Makandokando Kama Lissu Na Zitto Wapambane Na Magufuli 2020.
 
GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
36,842
2,000
Ila Kupelekwa Kwa Kapilimba Nje Ya Nchi Ni Kuthibiti Nguvu Ya Membe Kuelekea Uchaguzi 2020 Wala Sio Kwa Maslai Ya Taifa.

Na Magufuli Apa Ndio Nimeona Kwamba Jamaa Ana Intelijensia Ambayo Sio Mchezo

Ningekuwa Karibu Na Membe Ningemshauri Aachane Na Mawazo Aliyonayo Awaache Vijana Wasio Na Makandokando Kama Lissu Na Zitto Wapambane Na Magufuli 2020.
Kudos Ndugu.
 
Mtumishi Wetu

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
5,530
2,000
Bwn BKMembe ni mwana CCM Bwn T Lisu na Zito Kabwe ni vyama tofauti hivyo hana sababu ya kutogombea huko CCM.
Hawa wengine wakagombea kupitia kwenye vyama vyao!!
 
naumbu

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
4,662
2,000
Uteuzi wao uko palepale. Nchi X ikimkataa balozi A atapangiwa nchi Y na balozi B atabadilishwa na kupelekwa huko. Reshuffle itaendelea hadi wateule wote wapate vituo. Ni lazima uteuzi wako utangazwe ndiyo jina lipelekwe na sio vinginevyo.
Unaweza kuwa Balozi na usiwe na kituo pia hata teuzi za leo kuna watu wamepewa Ubalozi ila wanaendelea na majukumu yao ya Ikulu
 
Songambele

JF-Expert Member
Nov 20, 2007
4,455
2,000
Ukimaliza ktk wateuliwa awamu hii yupi sio spy????
Swali Namba Moja.

Hivi ni lazima kila ‘Spymaster ‘ akistaafu au akitumbuliwa Kazini ateuliwe kuwa Balozi?

Swali Namba Mbili

Kama bado huwa hatujui Vituo vya Kazi vya Mabalozi Wateuliwa kwanini huwa tunaanza Kuwatangaza?

Nayasubiri majibu yenu kwa hamu zote Wana Ndugu wa JamiiForums.
 
mtu chake

JF-Expert Member
Aug 20, 2010
18,440
2,000
Ni yule aliyetakiwa kwenda Taifa lenye Watu wenye Akili nyingi kuliko wengine ( hasa Barani Afrika ) la Rwanda au?
Kumbukuku zangu zinaonesha aliyekataliwa na Tanzania kwa tuhuma hz alikua nadhani ni balozi wa ujerumani

Na balozi wa Tanzania aliyekataliwa Rwanda alikua balozi Siwa
 
Top Bottom