Nikiingia ofisini nasikia usingizi, nifanyeje nisisikie usingizi?

Nov 20, 2016
70
35
Ndugu zangu wa JF,

Naombeni namna ya kufanya nikiingia ofisini asubuhi saa 2 nikikaa kwenye kiti tu nasikia usingizi wa ajabu mpaka najiuliza ni kwanini.

Sijui nifanyeje?
 
Ndugu zangu wa JF,

Naombeni namna ya kufanya nikiingia ofisini asubuhi saa 2 nikikaa kwenye kiti tu nasikia usingizi wa ajabu mpaka najiuliza ni kwanini.

Sijui nifanyeje?

hapo ofisini kwenu kuna mtu anakuonea kijicho anataka ushindwe kazi.....
cha kufanya.......ukiingia asubuhi....chukua chumvi changanya na maji......panda juu ya meza nyunyuza hayo maji kwa chini......kisha fagia kuingia ndani na si kutoka nje........m'baya wako utamjua siku si nyingi......
utanishukuru badae........
 
Hata mimi naamka asubuhi sana kuwai foleni, pia narudi home mida ya saa 3 hadi 4 usiku, hivyo nakuwa na tatizo la kulala. ninacho fanya uwa nafungulia AC kali sana, pia nakunywa kahawa, pia najitahidi niwe busy.
 
mzee karibu kunywa ENERGY DRINKS,
ila usijizoeshe saana.
kikubwa lala masaa yasiyopungua 8 na uwe unaoga kabla ya kwenda kazini,
Cuz kwakawaida maji yanauchangamsha mwili, pia jitahidi uwe unakunywa maji mengi
 
Kila ukianza kusinzia fikiria jinsi gani utaweza kumudu kodi ya pango,ada za watoto,chakula na heshima kwenye jamii bila hyo kazi,pia fikiria juu ya vijana kama million na ushee walioko mtaani wanawania hyo Chance yako,utagundua ni pepo jipu litaka utumbuliwe hutasinzia tena
 
Punguza mawazo,lala usingizi wa kutosha,kwa siku kunywa maji hata glass mbili(bora mbili kuliko kuacha kabisa) inasaidia na kuongeza hamu ya kula na kupunguza usingiz muda wote.
 
jibu tested huyo jamaa anajiita hacker mean mtu wa IT hawa watu kazi zao nyingi huzifanya usiku muda mwing wanacheza na code wanasahau mpaka kulala
utakuwa unaamka mapema sana,au unawahi foleni?lol,dawa ni kuongeza masaa unayolala,lol kama unalalaga saa nne,lala saa mbili,angalia kama situation yako baada ya kuongeza hayo masaa mawili ya kulala kama itasaidia,kama haisaidii muone doctor.
 
Sawa rebeca
 
Back
Top Bottom