Mwana wa Nuru
JF-Expert Member
- Dec 3, 2012
- 588
- 410
Mimi ni baba wa watoto wengi na mume wa Mke mmoja. nimefanikiwa kuwa na vitu vichache kama mende wasiozidi hamsini, mahindi nusu debe na kibanda cha kupumzikia jua likichwa. hofu yangu ni Je, niliondoka nani atawaangalia mende ambao nimejitahidi kuwatunza kwa takataka kadhaa?
Mke wangu nani atamhudumia kama mimi? Nalazimika kwenda hospitali na kucheki afya yangu na kukuta vipimo vinaonesha mimi ni mwathirika anayetembea kwa kudra za walinzi wangu tu.
Najitahidi kumeza dawa nyingi ili niendelee kuishi milele nikiangalia mende wangu ambao hata babu yetu hakuweza kuwa nao wakati akiwa hai. wakati najilazimisha hivyo kutoondoka mapema ndipo swali likanijia, hivi na kifo kikija nitakigomea ili nisiache mende wangu na mke wangu akawa wa mwingine (kama mke wa Samora alivyochukuli na swahiba wake Madiba.
Tuache kujidanganya, sote tu sawa, pua zetu zinatazama (bila macho) chini, hivyo lazima siku moja tuwaachie wengine, kwa hiari au kwa lazima.