Nikichaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nikichaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ngida1, Oct 2, 2009.

 1. Ngida1

  Ngida1 JF-Expert Member

  #1
  Oct 2, 2009
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 554
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Ndugu wana-forum,

  Kama nikichaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, nitawatangazia Watanzania wote kuwa kila mtu anaweza kuomba uwaziri mkuu pamoja na uwaziri wa wizara yoyote anayoitaka, lakini anieleze tu kwanini anataka wadhifa huo. Hii inamaana nitataka nielezwe kwenye application kama nikimchagua kuwa Waziri Mkuu au Waziri wa hio wizara anayoitaka atafanya nini - yaani anayo malengo gani (visions) kwa wizara yake. Of course hayo malengo yake hayatokuwa the only criteria nitakayoitumia kumchagua. Pia nitataka kujua elimu yake na uzowefu wake wa kazi, lakini zaidi nikutaka kujua atafanya nini au ni mwenye mikakati gani kwa hio wizara ili Taifa lisonge mbele kwa haraka.
  Kabla Nd. Lampart hujanirukia, please, fahamu pia kwamba ninafahamu vizuri sana kuwa waziri ni mtekelezaji tu na kuwa nini wizara ifanye ni kutokana na mipango, malengo na sera ya Taifa na Chama kinachotawala na sio waziri.
  Naomba kutoa hoja.
   
 2. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #2
  Oct 2, 2009
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Nitamtafuta Ngida1 na kumuweka ndani mara moja ili kufuta ndoto yake ya kukalia kiti changu siku moja
   
 3. Ngida1

  Ngida1 JF-Expert Member

  #3
  Oct 2, 2009
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 554
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Ndugu Rais Ngida1,
  Huu ni mwaka 2020 na wewe jana umetangaziwa kuwa umechaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa wingi wa heshima na unyenyekevu ninaleta kwako application yangu ili unichague kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano kama sera zako za uchaguzi zilivyoeleza.
  Sifa zangu ni pamoja na kuwa shushushu wa serikali kwa miaka 20 chini ya wizara ya ndani.
  Ni mwenye shahada ya sheria na huko nyuma niliwahi kuwa mwalimu wa kujitolea kule kwetu(?).
  Nia yangu ya kutaka kuwa Waziri Mkuu ni kuiokoa nchi yetu kutokana na majanga mengi inayoipata. Ukinirihusu, hapa chini nitataja mambo ambayo nitayashughulikia nikiwa Waziri Mkuu pamoja na kuiendeleza CCM ikawa juyu, juyu, juyu zaidi.
  [1] Kwanza, nitahakikisha kuwa Zanzibar inakufa kama ilivyokufa Tanganyika na itakuwa Mkoa. Waznz wakileta ukorofi basi tutakipeperusha kisiwa mbali sana na pwani yetu kama alivyotaka Baba wetu wa Taifa.
  [2] Nitahakikisha kuwa wizara zote haziagizii tena mashangingi. Mawaziri wote watapanda gari za punda au ng'ombe - gari ambazo zitatoka kule kwenye kisiwa chetu maarafu cha Pemba. Kule kuna mafundi wazuri sana ambao siku hizi wamehamia Ilala kwa muda.
  [3] Nitahakikisha kuwa hakuna Waziri atakaevaa suti au nguo za kutizamika zaidi ya zako. Wote watavaa lubega isipokuwa wewe Mheshimiwa. Waznz watavaa kanzu na shuka tu kama huko nyuma.
  [4} Watanzania wote hawatoruhusiwa kula nyama ya ng'ombe. Nyama ya ng'ombe itakuwa inapelekwa nje kwaajili ya kupata pesa za kigeni.
  [5] Wanafunzi mashuleni hawatopewa madaftari ya kuandikia. Watapewa majani ya mgomba kuandikia. Karatasi mzee zinamaliza miti yetu na ni ghali sana.
  [6] Umeme wa kidato hautopelekwa tena Zanzibar, kwasababu hawalipi madeni yao. In fact, mzee, tokea hapo zamani walikuwa hawana umeme na wakitumia vibatari tu. Wakileta matatizo juu ya umeme tutawatajia jina la Seif Sharrif Hamad na hapo hapo watanyamaza.
  [7] Tutajenga viwanda vya kutengeneza vibatari kwaajili ya Pemba na Unguja na kwa njia hii tutaweza kujitosheleza kwa umeme wetu kwa viwanda vyetu hapa Bara.
  [8] Nitahakikisha kuwa kama Rais wa ZNZ doesn't attend mikutano ya Bara itakuwa keshajivukuza kazi. Kutokhudhuria kwake mikutano yetu inawapa maadui wetu akina Warioba kusema kuwa kuna ufa mkubwa sana kwenye Muungano wetu.
  [9] Wakongwe wote wa CCM tutawapeleka CUF kabla hatujawapeleka kaburini. At least this way tutajua wapo wapi wakihitajika - yaani either wapo CUF au kaburini.
  [10] Mawaziri hawatoruhusiwa kunywa bia au pombe yoyote. Watakunywa togwa kama wanavyokunywa Waznz wote. Hatuweza kuwa kwenye nchi moja upande mmoja wanakunywa togwa na wapili wanakunywa bia. This is not egalitate at all!
  Kutokana na mikakati yangu ya hapo juu, tutaweza ku-save billions of shillings kwa mwaka ambazo tutazitia kwenye miradi ya maendeleo ya wananchi na kwa muda wa miaka miwli tu nchi yetu itatajika kama nchi iliyoendelea.
  Lastly, Mr President, I hope you will give my application a very kind consideration ili nami niwe kama wenzangu katika kuifisidi nchi!
  Wako katika kazi za kujenga Taifa letu / Lampart.
   
 4. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #4
  Oct 2, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,598
  Likes Received: 3,890
  Trophy Points: 280
  Utakuwa rais wa Kwanza kufanya hivyo! pata kwanza urais utapata viongozi wengi tu wenye sifa.

  Ila wengi hupenda kuchagua watu watakaoweweseka na hicho cheo mpaka kaburini!

  See what JK did, amempiga chini kiaina Lowassa, akamchagua Pinda, Pinda hakuwa kuota hicho cheo, mpaka leo kila anachofikiri na kuota ni kuweweseka weweseka tu,

  Lengo PM asivume zaidi ya rais!

  Kamuulize Sokoine!
   
 5. Ngida1

  Ngida1 JF-Expert Member

  #5
  Oct 2, 2009
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 554
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Dear Nd. Lampart,
  Nimefurahi kuwa umekuwa wa mwanzo ku-apply kuwa waziri katika serikali yangu iliyochaguliwa jana na wananchi wetu. Kutokana na sifa zako za kuitumikia nchi hii na kutokana na mikakati yako ambayo utaitekeleza ukiwa Waziri Mkuu, ninafuraha kuwatangazia wananchi wa Jamhuri kuwa nimekuchaguwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano kuanzia leo October Mosi, 2020. Tafadhali, fahamu kwamba pamoja na mikakati yako, please, make sure that you consider the party's priorities as your main priorities too. Juu zaidi ni kuhakikisha kuwa tunalindana tukiwa kwenye wadhifa na pia tukiwa tupo nje ya wadhifa. Pia hakikisha kuwa CUF hawashindi kule ZNZ. In fact, Waznz wameingia kwenye huu Muunagno ili tuwalinde na kwahivyo hakikisha kuwa tunawalinda maisha, else watatoka.
  CCM juyu, juyu, juyu zaidi.
  IDUMU CCM.
  Nakutakia kila la kheri katika kazi zako mpya.
  Ndugu yako, Rais wa Jamhuri Ngida Al Nambar One.
   
 6. L

  Lampart Senior Member

  #6
  Oct 2, 2009
  Joined: Sep 18, 2009
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nd. Rais Kichuguu,
  Naomba mzee umsamehe huyu kijana aitwae Ngida1. Naona toka Pinda alivyoamua kutaka kumnyang'aya babu yake (Babu Ataka Kusema) ile suti yake na tai basi rafiki yangu Ngida1 kaharibikiwa akili kidogo.
  Kwa pamoja tumuombeeni dua ndugu yetu na rafiki yetu Ngida1 apone haraka na kwa pamoja pia tumlaani Pinda ili Babu Ataka Kusema asinyang'anywe suti yake.
   
 7. M

  Mayolela JF-Expert Member

  #7
  Oct 2, 2009
  Joined: Sep 21, 2009
  Messages: 383
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Rais Ngida 1,
  Hizo ni ndoto za kufikirika tena mchana wala sio usiku.
   
 8. l

  lukule2009 Senior Member

  #8
  Oct 3, 2009
  Joined: Sep 23, 2009
  Messages: 132
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivi jamani seriously naomba kuuliza: kuvaa ama kutokuvaa suti , it it a serious matter to deserve the attention of Honourable PM? or to deserve the discussion we currently see in the country or here in the JF? Kuvaa ama kutokuvaa suti , isi it urgent issue?Does it concern majority of Tanzanians to deserve the attention we are giving the issue?Seriously guys does it really matter? Pumba zingine tuwe tunaziacha zipite na upepo.. please magazeti iacheni hiyo issue ni aibu kwa taifa. Yani tunajadili kamam watu wavae au wasivae suti,kweli? Hivi suala la nguo gani mtu anavaa ni jukumu la Waziri Mkuu? Ni national issue? Let us go back to basi issues. Please guys ..
   
 9. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #9
  Oct 3, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  humu ndani watu sio serious.............
   
 10. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #10
  Oct 3, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  kwahiyo rais atakuwa anatekeleza vision ya PM, maana Rais mwenyewe hajasema anata kuifanyia nini Tanzania zaidi kutaka waziri apply kazi na ajieleze? hebu jieleze kama rais mtarajiwa.
   
Loading...