Nikasingiziwa kutembea na kabinti ka shule, kikanuka ukweni….! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nikasingiziwa kutembea na kabinti ka shule, kikanuka ukweni….!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Oct 30, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Kalikuwa ni kabinti kadogo kazuri.....!

  Ilikuwa ni Jumamosi mwaka 1999, Januari. Nilikuwa natoka nyumbani Mwananyamala kwenda kibaha Picha ya Ndege mkoa wa Pwani. Hapo Picha ya Ndege ndiko kulikuwa na wakwe zangu watarajiwa. Kwa kuwa ilishapelekwa posa na mimi kutambulishwa, nilikuwa na tabia ya kwenda kusalimia na kuonana na mke wangu mtarajiwa.

  Nilipofika hapo Picha ya Ndege nilielekea moja kwa moja kwa wakwe zangu ambao walikuwa hawakai mbali sana na barabarani. Nilipokaribia kufika hapo kwa wakwe zangu nilikutana na kasichana ambako umri wake ni kama miaka 12 hivi. Kalikuwa kanatafuta kitu kando ya barabara. Mimi napenda sana watoto, hasa kuwasaidia kutokana na malezi yangu ya utotoni ambapo sikubahatika kupata malezi ya mama kutokana na mama yangu kufariki na kuniacha nikiwa na umri mdogo sana.

  Nilipokaona kanatafuta kitu halafu kanajifuta machozi, nikaamua kukauliza kanatafuta nini, na kwa nini kanalia. Kalisema kwa kifupi kwamba kamepoteza hereni yake moja. Nilikakatuliza kwa kukaambia kasilie kisha nikaanza kukasaidia kutafuta hiyo Hereni yake.

  Wakati nikiendelea kukasaidia kutafuta hiyo hereni yake, haukupita muda, wakafika vijana wanne pale tulipokuwa. Walinivamia na kunishika kama vile nilikuwa kibaka. "Mshenzi wee, unaharibu watoto wa watu, leo utaona. Jitu zima kutembea na watoto tu." Mmoja kati yao alisema. Wale wenzie watatu walinikunja na mmoja akamshika yule binti mkono. "Twende serikali za mitaa, halafu Polisi. Lazima mtu apigwe mvua thelathini." alizidi kusema wakati wananikokota.

  Kwa sababu ya mshangao sikuweza kusema chochote. Yule binti alikuwa akijitetea kwa kusema. "Dada mwongo wala hakunikuta naye, mwongo tu…" Sikujua ni kitu gani. Akili ilinijia tulipofikishwa kwenye ofisi za serekali ya mtaa. Niliwauliza. "Nimekosa kitu gani kustahili adha kama hii….?" Mmoja kati ya wale vijana walionibeba msobe msobe alisema. "Hujui eh, utajua ukifika mahakamani, Malaya wee….."

  Sikuelewa kitu. Wakati nashangaa, nilimwona mama mkwe wangu mtaraji na shemeji zangu watarajiwa wawili na mchumbangu nao wakiwa wamefika pale. Mama mkwe mtarajiwa aliniuliza kulikoni. Nikamjibu. "Najua basi, naona jamaa wamekuja na kunishika tu na kunileta hapa…"

  Mmoja kati ya wale jamaa alisema, "Mwongo sana huyu jamaa. Huyu anatembea na haka kadogo ketu, ameshakaharibu. Bahati dada yetu leo amemshika wako pamoja njiani muda wa masomo. Dada alipomuuliza, akamshambulia dada yetu akisaidiwa na huyu mdogo wetu mapepe. Dada ameenda kuwaita wazazi waje hapa tuamue."

  Niliposikia hivyo niliogopa na kuona aibu kiasi kwamba, sikuweza hata kusema. Hasira, woga na aibu vikanifanya bubu kabisa. Hadi leo najiuliza namna akili na miili yetu inavyofanya kazi. Wale shemeji zangu watarajiwa, mama mkwe mtarajiwa na mchumbangu walikaa kando kujadili. Niliona kabisa nyuso zao zilivyo na hasira.

  Wakati wakinijadili na kunitizama kwa hasira, niliomba ardhi ipasuke niingie chini. Lakini huyo dada anayedaiwa kwamba nilimshambulia alifika akiwa na mwanamke na mwanaume, ambao niliamini ni wazazi wake. Walipofika pale, yule dada aliwauliza wale vijana wababe walionibeba juu juu, "yuko wapi huyo mshenzi?" Mmoja kati ya wale vijana alisema, "si huyu hapa umeshamsahau!" Alisema akinionyesha kidole. Yule dada alisema, "siyo huyu bwana . kwani huyu mmemtoa wapi?"wale jamaa walionekana kushangaa….. "Tulimkuta akiwa pamoja na Furaha, tukajua ndiye yeye."

  Yule dada alishangaa na kusema, "Jamani siyo huyo, mmemwaibisha kaka wa watu bure. Huyu kaka wala simjui. Kaka samahani sana, naomba uwasamehe hawa kaka zangu.." Alisema yule dada. Mimi sikujibu. Nilisimama na kuanza kuondoka. Umati wa watu waliojazana pale kufuatilia sakata langu ulikuwa kimya.

  Mchumbangu aliniita… "Rudi, hakuna kuwasamehe hawa, hadi mahakamani wakulipe fidia. Hawawezi kuvunjia watu heshima kwa sababu ya ubabe wao." Mimi sikugeuka wala kurudi. Nilirudi zangu Mwananyamala.

  Nasikitika kwamba huo ndio ulikuwa ni mwanzo wa mikosi kuniandama hadi uchumba wangu na Binti Picha ya Ndege ukavunjika…………..
   
 2. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #2
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Kuna watu hapa najua watasema maneno mbofu mbofu kuhusu uzi huu...
  Hii maneno si yangu wala hainihusu kabisaaa, inamuhusu jirani yangu....!
   
 3. M

  MAFUNZO Member

  #3
  Oct 30, 2012
  Joined: Sep 4, 2012
  Messages: 45
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 13
  So Sorry !
   
 4. Z

  Zero One Two JF-Expert Member

  #4
  Oct 30, 2012
  Joined: Sep 16, 2007
  Messages: 9,390
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  Unajitoa? subili upate unachostahili, maana mzee Mtambuzi. Inaonekana ni tabia yako ya kuzaliwa nayo
   
 5. Mgibeon

  Mgibeon JF-Expert Member

  #5
  Oct 30, 2012
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 7,441
  Likes Received: 9,090
  Trophy Points: 280
  Dah, inaumiza sana! Wakati flani tunahitaji kua makini tunapotoa Msaada! Mia
   
 6. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #6
  Oct 30, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Mmmmmhhhhh! Nimekwenda juani na mwezini ghafla! Narudi, the world is not fair!
   
 7. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #7
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Mia........? Umenikumbusha @figanigga
   
 8. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #8
  Oct 30, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,175
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  ni kama nataka nikutetee hasa nikizingatia historia yako lakini mh hili ni funzo i see!na hii michezo ya watu kukubambikia kesi ilivo mingi siku hizi ?tena bora hao kweli walikuwa hawajui walichukua tu haraka haraka kun amijitu unaisaidia siku hizi kumbe linakuja kukugeuka baada ya muda fulani!
  si unakumbuka ile ishu ya mdada pale muhimbili alikuwa anajifanya anaomba watu simu zao aweke line ili ampgie mume wake kuwa mtoto anatakiwa kulaza hapo ana mtoto mgongoni kisha anajifanya kusahau line yake kwako na kuhakikisha anapanda basi moja na huyo aliyemuazimisha simu(tena anakuwa na wenzie kama wawili hivi ambao hatawanotice ) akifika mbele kidogo anapiga kelele ''SIMU YANGU IMEIBIWA JAMANI'' watu haraka haraka hebu teja namba yako akitaja simu inaita kwa jamaa aliyemuazima handset!anapokeaje kichapo mpaka uje ujulikane simu ni yake na wameshamkufanyia utapeli ameshaumia,simu ashaporwa,ameshaaibika lol!
   
 9. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #9
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Mtambuzi mbona unajihami kabla ya watu kusema
  kwenye mabano (kumbe Mtambuzi unapenda dogo dogo eeehhh ole wako mama Ngina ajue kama hutahama chumba)
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #10
  Oct 30, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,633
  Trophy Points: 280
  Ha ha ha ha Mtambuzi nilidhani leo ni Al Ijumaaa...
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #11
  Oct 30, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,175
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  mshukiwa namba moja najua ni mimi!
   
 12. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #12
  Oct 30, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Hata kama ingekuhusu bado upo innocent kwa hiyo haina tatizo kwako. Lakini kiujumla maisha ndivyo yalivyo. Wakati mwingine yanapotokea yafaa kumshukuru tu Mungu maana hujui ni kwanini yametokea. Very sorry to him.
   
 13. Mgibeon

  Mgibeon JF-Expert Member

  #13
  Oct 30, 2012
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 7,441
  Likes Received: 9,090
  Trophy Points: 280
  Ha ha ha ha haa, unajua ukilizoea hili neno huwezi ku' comment bila kulitaja! Usiposema "mia" unajihisi kama umekula chakula kinono bila kunywa maji..! Mia
   
 14. M

  Magwero JF-Expert Member

  #14
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 28, 2011
  Messages: 243
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  Dah....
   
 15. Kichancheda

  Kichancheda Senior Member

  #15
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 29, 2012
  Messages: 142
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Niliwahi kuambiwa huko uswahilini pwani ,It is very rear kukuta bikra picha ya ndege!
   
 16. ram

  ram JF-Expert Member

  #16
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 6,203
  Likes Received: 905
  Trophy Points: 280
  Unanifurahishaga sana best, unajiwahigi mapemaaaa!

  Mpe pole jirani yako, alishaoa au ndo uchumba ulivyovunjika hakuwa na hamu tena ya kuoa

   
 17. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #17
  Oct 30, 2012
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Wee Mtambuz hiyo hereni ilikuwa ya dhahabu? Mpaka muhangaike kuitafuta?
   
 18. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #18
  Oct 30, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,226
  Trophy Points: 280
  afadhali huo uchumba ulivunjika.....mama ngina akapata nafasi...
   
 19. Bazazi

  Bazazi JF-Expert Member

  #19
  Oct 30, 2012
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 2,029
  Likes Received: 558
  Trophy Points: 280
  Alikuwa eneo baya katika muda mbaya. Verry sorry for him>

  Bazazi!
   
 20. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #20
  Oct 31, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,105
  Likes Received: 7,358
  Trophy Points: 280
  Jumba bovu.......!!!!
   
Loading...