Nikaribisheni ndugu zangu, mimi ni mwanachama mpya kwenye huu mtandao

Jameni msaada mie mgeni..nitawapataje hao moderators? naenda kwenye sehem ipi ili niwasiliane nawo?
 
Habari za muda huu marafiki zangu wakina kaka na dada poleni na shughuli za hapa na pale na stress za VYUMA kugoma kuachia ijapokuwa tumeshauliwa kutumia ati oil sjui grisi ilhali hata pesa ya kununulia hiyo grisi hakuna ni hatari sana

Basi ndugu zangu pasipo kupoteza muda naomba mnipokee kwa mikono miwili hivyo tutakuwa wote kuanzia sasa na kuendelea katika kubadilishana stress zetu humu jukwaani kwa kipindi chote hivyo naomba pale ntakapokosea nirekebishwe kiroho tuu pasipo kutumia lugha za maudhi maana mimi pia ni miongoni mwa memba ambao ni zao la mtandao wa facebook hivyo bado itikadi za kule zipo akilini.

Pia kabla ya kujiunga humu nilikuwa msomaji tuu ambapo kiukweli memba wengi sana humu ninawafahamu vyema kwa majina na hata haiba zao kupitia post zao kwani nimekuwa msomaji wa jf toka 2015 mpaka sasa kipindi hicho sijawa na SIMU JANJA(smart phone) kutokana na mwingiliano wa majukumu.

wenu memba mpya machachari kijana mzalendo zao la facebook,
[HASHTAG]#africanar[/HASHTAG]
c212c516ab6576288e88fec9b85fe6af.jpg
fb.
 
Back
Top Bottom