...Nikamwambia nenda kwa Polepole akukopeshe

ashera

JF-Expert Member
Aug 3, 2020
500
1,029
Huyu ni rafiki yangu wa kitambo. Alikuwa Mwana-CHADEMAmzuri na mpigania haki kweli kweli. Basi likaja lile wimbi la wapinzani kununuliwa na CCM akasepea ccm kuunga juhudi. Nikawa namcheki tu

Uchaguzi umekuja akawa mstari wa mbele kuikandia chadema na kuipaka matope wakati ndiyo iliyomtoa jalalani. Akawa MwanaCCM machachari kuliko hata wenye chama chao. Nikawa namcheki tu

Basi uchaguzi umeisha anakuja kwangu analialia alivyofulia, maisha yalivyomuwia magumu maana wajumbe walimkatilia mbali, eti anataka nimkopeshe pesa walau akawanunulie Watoto Ugali

Sikumchelewesha nikampa makavu laivu, nikamwambia umeshiriki kuwadhurumu watanzania na kuikana kweli kisa vipande vya fedha

Umetema Big G kwa karanga za kuonjeshwa sasa nenda kwa hao kina Magu na Polepole wakukopeshe. Hata mwezi baada ya uchaguzi bado ushaanza kulia njaa? Akapikie Watoto Fly Over na Bombardier.

Nikamwambia sikukopeshi hata mia shubaamit na urafiki ufe

Dawa ya hawa wasaliti wa haki ni kuwafungia vioo. Walidhani watakuwa na bei zao special za cement, sukari nk, kumbe tunakuja kusota nao hukuhuku mtaani
 
Tusifike Huko,Zanzibar Haya Mambo Wakati Fulani Yaliwapa Tabu Sana Ikafikia Hatua Mbaya Mno
Mwanachama Wa CUF Alikuwa Hawezi Kumzika Wa CCM
Pia Ilikuwa Kuoa/Kuolea Na Mtu Wa Chama Tofauti Haiwezekani.

Mpaka Wakatafuta Maridhiano
 
Unauwezo mdogo sana wa kufikiri na maamuzi ya kipumbavu. Unawezaje kufanya maamuzi ya hovyo kiasi hicho kisa siasa? Hutakiwi kuendeleza milengo ya kisiasa hatà baada ya hayo kupata.

Mkuu, na wewe uliomba mkopo kitaa ukatimuliwa?
Naona ukiandaa text ya kumkopa barmaid mahali...!!
Pole bhana, zile buku 7 siku hizi zimeishia wapi!?
 
Unauwezo mdogo sana wa kufikiri na maamuzi ya kipumbavu. Unawezaje kufanya maamuzi ya hovyo kiasi hicho kisa siasa? Hutakiwi kuendeleza milengo ya kisiasa hatà baada ya hayo kupata.
Nyoo...kuna maamuzi ya kipumbavu zaid ya kuwaua wengine na kuwatishia uhai wao?? Yuko sahihi kabisaa..ashike adabu yakee..tena na urafik uishie hapo hapo..shikilia hapo hapo mzee baba..hakuna kukopesha hapoo..
 
Huyu ni rafiki yangu wa kitambo. Alikuwa mwanachadema mzuri na mpigania haki kweli kweli. Basi likaja lile wimbi la wapinzani kununuliwa na ccm akasepea ccm kuunga juhudi. Nikawa namcheki tu

Uchaguzi umekuja akawa mstari wa mbele kuikandia chadema na kuipaka matope wakati ndiyo iliyomtoa jalalani. Akawa mwanaccm machachari kuliko hata wenye chama chao. Nikawa namcheki tu

Basi uchaguzi umeisha anakuja kwangu analialia alivyofulia, maisha yalivyomuwia magumu maana wajumbe walimkatilia mbali, eti anataka nimkopeshe pesa walau akawanunulie watoto ugali

Sikumchelewesha nikampa makavu laivu, nikamwambia umeshiriki kuwadhurumu watanzania na kuikana kweli kisa vipande vya fedha

Umetema big g kwa karanga za kuonjeshwa sasa nenda kwa hao kina Magu na Polepole wakukopeshe. Hata mwezi baada ya uchaguzi bado ushaanza kulia njaa? Akapikie watoto fly over na bombardier...pumbav

Nikamwambia sikukopeshi hata mia shubaamit na urafiki ufe

Dawa ya hawa wasaliti wa haki ni kuwafungia vioo. Walidhani watakuwa na bei zao special za cement, sukari nk, kumbe tunakuja kusota nao hukuhuku mtaani
Muhuni huyo. Mpe za usoni. Wameiba kura kuturudishia madarakani akina spika dhaifu na wachungaji wanaobemenda kondoo "nileteeni gwajima". Hovyoo.
 
Back
Top Bottom