Nikaishi wapi Dar hii, nikimbie hizi foleni?

Al Zagawi

JF-Expert Member
Mar 17, 2009
2,461
1,446
Swali lijamvini
Mawazo nisaidieni
Nimezidiwa wajameni
Hili jambo laniudhi

Kila upitapo watu kibao
Kila uendako watu kibao
Hakukosea aliyeimba hivyo
Mchizi Mox heshima kwako

Hospitalini foleni
Sokoni foleni
Barabarani foleni
Nitajie pasipo foleni

Pesa zangu zibenki
Nikizitaka kwa foleni
Nakaishi wapi Dar hii
Nikimbie hizi foleni

Foleni zanikuta
Kwa kuwa nashi Dar
Hapa foleni imezaliwa
Mikoani imezikwa

Najua foleni ni sawa
Uungwana kwa waloendedelea
Kwani watu si wanyama
Foleni huleta usawa

Lakini foleni ikizidi
Uvumilivu huwa majaribuni
Na hatari iliyopo
Ni watu kuwa kama Popo

Naomba niishie hapa
Muda wangu umeisha
Niendako ni mbali
Wacha niwahi foleni
 
Bunju na kazi yako iwe ni kulima matikiti maji na sisi wakulima tuwe tunakuja kununua huko shambani kwako!
 
foleni mbaya DAR uwe unaishi Mwenge kisha ukajichanganya unatokea Buguruni ukapita MANDELA Rd, halafu iwe week days, unakutana na foleni kuanzia external, na kwambia si chini ya dakika 70 utasimama kwenye hilo eneo, mpaka ukivuka , utakua umetukana matusi yote dhidi ya trafiki wa pale mataa.
 
Kumbe ndio maana madogo wa UDSM waishio mabibo hua wanaamua kuua winga tu. Hahahaha
 
utakua umetukana matusi yote dhidi ya trafiki wa pale mataa.
matusi hayasaidii kwani foleni imeshakutengeneza tu! wahi kutoka home asbh mapema na kurudi home chelewa kiasi, pitia gym au nenda gymkhana!
 
matusi hayasaidii kwani foleni imeshakutengeneza tu! wahi kutoka home asbh mapema na kurudi home chelewa kiasi, pitia gym au nenda gymkhana!
Wote tukifanya hivyo si tutahamisha muda wa foleni......??? FANYA KAZI POSTA, MWENGE, MASAKI, HALAFU UNAISHI KIGAMBONI. Asubuhi na jioni unapishana na foleni
 
matusi hayasaidii kwani foleni imeshakutengeneza tu! wahi kutoka home asbh mapema na kurudi home chelewa kiasi, pitia gym au nenda gymkhana!
Pape,
unajua tatizo la kile kivuko cha morogoro Road na MANDELA, Kuna trafic wenye mawazo ya hovyo kabisa, wanaamini kuwa Mandela rd ni njia ya maroli na watu wasiokuwa na kazi, maana mtu alioko magomeni ama Kimara anavuka pale, wewe wa Riverside umekwamishwa na yeye tu.
suluhu ni kuziacha taa ziwake, maana kunawakati taa nzima tu, ila wenyewe wameng'ang'ana kuongoza magari,
jiji limetoa pesa nyingi kununua taa zile wakati hazitumiki.
Ndo maana wakazi wengi wa maeneo hayo walichekelea kupigwa kwa askari TRAFIKI NA MWANANAJESHI WA JWTZ.
 
au kitunda kabisa ajiwekee na facilities zote nyumbani kwake
utafikaje Kitunda kirahisi, wakati Dakika 45 unaweza kutumia kuvuka kati ya air port maarufu kama Posta hadi banana...
labda kama baada ya kuwa na facilities zote unaanzisha mradi wa kuku....
 
utafikaje Kitunda kirahisi, wakati Dakika 45 unaweza kutumia kuvuka kati ya air port maarufu kama Posta hadi banana...
labda kama baada ya kuwa na facilities zote unaanzisha mradi wa kuku....

hahaaa sasa kuku nao kuwaleta sokoni...tunarudi pale pale
 
au kitunda kabisa ajiwekee na facilities zote nyumbani kwake
ARE YOU SERIOUS......??? KITUNDA.....!!!!!!!!! Hakiyanani tena waleee jamaa wata-WIPE familia yako............. YAANI WEWE UNA FACILITIES ZOTE HALAFU YEYE AHANGAIKE NA MAYAI..............
 
hahaaa sasa kuku nao kuwaleta sokoni...tunarudi pale pale
ndo maana naamini kuwa , Dar inabarabara ambazo zimeshindwa kabisa kukidhi ongezeko la wakazi wake.!
kwa ufumbuzi wa muda mfupi ni lazima Trafiki waache taa zifanye kazi, wao wawepo kwenye makutano hayo incase of dharula, na kukatika kwa umeme.
unless mkuu wa kikosi hicho , afukuzwe kazi yeye na wasaidizi wake, kwa misingi kuwa hana ubunifu, wala mawazo mapya , namna gani ataweza kutatua tatizo hili, lazima ukiwa kiongozi uwe na uwezo wa kuwa many steps aheads your mates, katika kufikiri, kinyume wewe ni ghalasa, hufai.
 
Hizi ndio gharama za kuwapa watu wasio na akili wawe viongozi wetu. Tumeikubali system yetu mbovu ya utawala na sasa tunakula matunda yake. Kama tungekuwa tunao mfumo wa kuongozwa na wataalamu badala ya wanasiasa (ambao kimsingi hawana technical abilities za kutatua matatizo ) tungekuwa at least a middle class society with promising future.

As I see it now, makazi holela yanaongezeka, miundombinu hakuna, hii ni ground for further creation of slums. Inashangaza nchi yenye ardhi kubwa kaa Tz inakuwa na slums kana kwamba tu Rwanda ua Urundi with land shortages and highest population densities. THIS IS CRAZY and shows our STUPIDITY.

Nway, inasikitisha kuwapo ktk dying nation like TZ. 100% hopeless.
 
ni masikitiko kwamba hakuna sehemu utakayoishi kuepuka foleni kwani hata ukiishi city center bado utahitaji kwenda hospitali au sehemu nyingine na kote waweza pata foleni except usiku mnene

mipango miji bado... tunasubiri kubomoja 10 year from now kama kawa

sasa usiombe viongozi wakiwa wanapita humo mabarabarani, utaona rangi zote
 
Hasa mzee ruksa.........
 
Hizi ndio gharama za kuwapa watu wasio na akili wawe viongozi wetu. Tumeikubali system yetu mbovu ya utawala na sasa tunakula matunda yake. Kama tungekuwa tunao mfumo wa kuongozwa na wataalamu badala ya wanasiasa (ambao kimsingi hawana technical abilities za kutatua matatizo ) tungekuwa at least a middle class society with promising future.

As I see it now, makazi holela yanaongezeka, miundombinu hakuna, hii ni ground for further creation of slums. Inashangaza nchi yenye ardhi kubwa kaa Tz inakuwa na slums kana kwamba tu Rwanda ua Urundi with land shortages and highest population densities. THIS IS CRAZY and shows our STUPIDITY.

Nway, inasikitisha kuwapo ktk dying nation like TZ. 100% hopeless.
kuna mipango miji wa kila wilaya, tangu uhuru, hakuna vision ktk kazi zetu, kama mipangowangetimiza wajibu wao tangu baada ya UHURU bila shaka, leo watu wakipawa wasingekua kwenye udhalili wa kiwango kile, watu wakigamboni wasingefikia hapo walipofikishwa leo.
nakubaliana nawe kuwa kuna mengine ni ya kitaalamu, tatizo yanaamuliwa kisiasa zaidi.
hatuna sera ya pamoja ya taifa katika kutimiza wajibu wetu, kila mtawala anakukuja na porojo zake.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom