Al Zagawi
JF-Expert Member
- Mar 17, 2009
- 2,461
- 1,447
Swali lijamvini
Mawazo nisaidieni
Nimezidiwa wajameni
Hili jambo laniudhi
Kila upitapo watu kibao
Kila uendako watu kibao
Hakukosea aliyeimba hivyo
Mchizi Mox heshima kwako
Hospitalini foleni
Sokoni foleni
Barabarani foleni
Nitajie pasipo foleni
Pesa zangu zibenki
Nikizitaka kwa foleni
Nakaishi wapi Dar hii
Nikimbie hizi foleni
Foleni zanikuta
Kwa kuwa nashi Dar
Hapa foleni imezaliwa
Mikoani imezikwa
Najua foleni ni sawa
Uungwana kwa waloendedelea
Kwani watu si wanyama
Foleni huleta usawa
Lakini foleni ikizidi
Uvumilivu huwa majaribuni
Na hatari iliyopo
Ni watu kuwa kama Popo
Naomba niishie hapa
Muda wangu umeisha
Niendako ni mbali
Wacha niwahi foleni
Mawazo nisaidieni
Nimezidiwa wajameni
Hili jambo laniudhi
Kila upitapo watu kibao
Kila uendako watu kibao
Hakukosea aliyeimba hivyo
Mchizi Mox heshima kwako
Hospitalini foleni
Sokoni foleni
Barabarani foleni
Nitajie pasipo foleni
Pesa zangu zibenki
Nikizitaka kwa foleni
Nakaishi wapi Dar hii
Nikimbie hizi foleni
Foleni zanikuta
Kwa kuwa nashi Dar
Hapa foleni imezaliwa
Mikoani imezikwa
Najua foleni ni sawa
Uungwana kwa waloendedelea
Kwani watu si wanyama
Foleni huleta usawa
Lakini foleni ikizidi
Uvumilivu huwa majaribuni
Na hatari iliyopo
Ni watu kuwa kama Popo
Naomba niishie hapa
Muda wangu umeisha
Niendako ni mbali
Wacha niwahi foleni