ichenjezya
JF-Expert Member
- Sep 26, 2013
- 1,010
- 1,119
Habari, naomba kujua taratibu na vigezo vya kujiunga na Uber kwa sasa vikoje, nina kagari kangu nataka nijiunge huko, msaada kwa anaejua alie na current information.....asanteni!
======
======
1.Gari lako liwe limetengenezwa kiwandani kuanzia mwaka 2001,aidha iwe sedan au hatchback itapendeza zaidi,na liwe na uwezo wa kubeba abiria wanne.
2. Utahitajika kubadilisha usajili wa gari lako kutoka kuwa private car hadi commercial car hivyo kadi ya gari lako itabidi ukabadili ikiwa ni pamoja na number plate kuweka nyeupe.
3. Kama utaendesha gari wewe mwenyewe inabidi uwe na driving licence with class A B C1 C2 C3 D na E pamoja na hati ya kipolisi ya tabia njema,"police clearance certificate" inayotolewa makao makuu ya polisi.
4. Uwe na smartphone.
5. Uwe ni mkazi wa jiji la dar.
6. Ukishakuwa na vigezo vyote hivyo karibu sana ofisini Viva tower kila siku za wiki Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 3 asubuhi mpaka saa 9 alasiri