Nijihadhari vipi ili kulinda akaunti yangu ya benki dhidi ya wadukuzi?

kibovu kichwa

Senior Member
May 17, 2019
145
106
Wakuu habari zenu,

Hivi mtu ukiwa na viakiba vyako vya kuunga unga benki. Kwanza natamani kujua Benki kuna usalama kiasi gani dhidi ya wezi wa kisasa wanaotumia teknolojia?

Pia nijihadhari na nini ninapokuwa nalink akaunti yangu na huduma mbalimbali za kulipia mitandaoni?

Karibuni tupeane maarifa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza hakikisha uwe na akaunti maalumu ya kufanya savings na fungua nyingine kwa ajili ya online transactions.

Usitumie akaunti yako ya savings yenye hela nyingi kwa ajili ya miamala ya mtandaoni. Hii ni tahadhari tu just in case wakakudukua online.
 
Ukishaweka vi sent vyako bank, suala la kuilinda ni kazi ya bank acha ushamba.
Ukiweka Pesa benki wewe na benki kila mmoja anasehemu yake ya kuwajibika katika pesa hizo,Benki wameinsure, lakini pia wameprotect saver zao, Wewe mwenye akaunti unatakiwa ujue namna ya kutunza kadi yako na Password yako.
Upande wa mitandaoni lazima uwe makini sana kwenye kulipia huduma mbalimbali inafaa kuwa na akaunti ya tofauti ambayo unahamisha na kutumia kiasi unachotaka tu.
 
Back
Top Bottom