Niiombe wizara ya kazi ajira, hazina, na nssf mfanyie kazi ujumbe huu haraka!

thetallest

JF-Expert Member
Oct 21, 2017
8,256
9,085
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, naomba niende kwenye mada ili ieleweke kusudio la waraka huu kwa taasisi tajwa hapo juu.

Mwaka jana 2017 serikali katika nia yake ya kutaka kuona watanzania wananufaika na na raslimali za madini ilizuia mchanga wa madini kusafirishwa nje ya nchi, ili ipitie mikataba upya ya madini na makampuni wekezaji.

Niseme tu kwa ufupi, matokeo ya upitiaji wa sheria hizo umeleta mafanikio makubwa kwa nchi Kama ilivyobainishwa na waziri Palamagamba Kabudi alieongoza kamati ya majadiliano alipowasilisha report ya majadiliano kwa rais, naipongeza serikali kwa kazi hiyo, hasa rais Magufuli.
Wakati wa utekelezaji wa jukumu hilo ililazimu mgodi wa bulyanhulu Acacia kufungwa, sababu zipo wazi, rejeeni tovuti ya Acacia .

Katika kuufunga wafanyakazi wa mgodi huo waliachishwa kazi ghafla, hii iliwaathili kiuchumi, kwani sheria iliotumika kukokotoa mafao ya kuachishwa hakuzingatia usawa, hivyo wafanyakazi walilipwa kiduchu Sana, kwani wengi walikua na mikataba ya mwaka Mwaka na baadhi ya muda kidogo.

Wakati wa zoezi hili la kuachishwa kazi yalifanyika mabaraza ya wafanyakazi,management ya kampuni na mifuko ya Jamii, kwa maana ya nssf, ppf nk, kuona namna ya kusaidia wafanyakazi kulipwa mafao yao ili yaweze wasaidia kujikimu kabla ya miezi sita, majadiliano yalifanyika na minit za majadiliano zipo,
mifuko ikajikomiti kulipa ndani ya mwezi mmoja na siku kumi na tano baada ya kufungua Madai, ikumbukwe hii ni favor mifuko ilitoa kulingana na dharura ilojitokeza, wafanyakazi walipokea offer hiyo kwa furaha Sana.

PPf naona Kama wametekeleza ahadi kwa asilimia nzuri kiasi chake , hongera zao.

Upande wa nssf naona kuna shida baadhi wanakwenda mwezi wa tatu sasa bila kulipwa, wakiuliza wanaambiwa bado majina yanafanyiwa uhakiki.uhakiki ni mpaka lini na hii ni special case kwa wafanyakazi wa Acacia buly? ,naomba kitengo cha uhakiki wasilale usingizi ,wanaumiza raia husika.

Pesa hii ndo wafanyakazi wa buly wanategemea kupelekea watoto shule, mpaka sasa watoto wapo majumbani, ajira hakuna na pesa hiyo ndo tegemezi ya kufungulia miradi ya kujikimu, kusaidia Ada, matibabu na chakula.

Tusiwafanye wafanyakazi waliokua wa Acacia buly, marekebisho hayo yawe majuto Kwao .

Naiomba serikali hii sikivu ya Magufuli ifanyie kazi kero hii kwa haraka, wapewe malipo yao wakayaingize kwenye mzunguko wa kilimo, biashara, na mengineo mengi ya kiuchumi.

Ni imani yangu hili litafanyiwa kazi name wahusika kwa haraka, kuwaondelea vijana hawa usumbufu wa kua kila siku wanashinda ofisi za nssf ,wakiwa taabani hawajui hatima yao na siku zinazidi yoyoma.

wenu katika ujenzi wa taifa .


Nawasilisha
 
Miaka ya nyuma kidogo walikuwa smart kabla ya sheria kufuta FAO la kujitoa, kuna kazi nilikuwa nafanya nikaacha sikupata tabu ya kupewa pesa zangu
MI mwenyewe siku za nyuma hawakunisumbua nashangaa kwa sasa watu wanavyoilaumu, unajua pamoja na sheria, ubinadamu,busara,hekima vinatakiwa
 
Mwamba yaani hawa jamaa wanakatisha tamaa Sana, hawako active kabisa

Mkuu kwa utetezi huu nakuunga mkono 100%. Mimi najua hali anayokutana nayo mtu pindi anapopoteza ajira. Mkuu na wala usiishie hapa, andika barua/email kabisa kwa sehemu husika. Huku jukwaani tutaendelea kupiga msukumo kama kawaida yetu. Hapa umelitendea jukwaa na hao wafanyakazi haki.
 
Mkuu kwa utetezi huu nakuunga mkono 100%. Mimi najua hali anayokutana nayo mtu pindi anapopoteza ajira. Mkuu na wala usiishie hapa, andika barua/email kabisa kwa sehemu husika. Huku jukwaani tutaendelea kupiga msukumo kama kawaida yetu. Hapa umelitendea jukwaa na hao wafanyakazi haki.
Kiukweli mkuu jamaa wanahali mbaya sana, na yalikua makubaliano na mfuko kutokana na tukio lenyewe lilikua la ghafla.
Familia zinadhilika ,wototo Kama unavyojua shule za private, hawpokelewi bila ada, shule zimefunguliwa January, February hii bado kizungumkuti watoto wako stranded majumbani, huruma mkuu
 
Kiukweli mkuu jamaa wanahali mbaya sana, na yalikua makubaliano na mfuko kutokana na tukio lenyewe lilikua la ghafla.
Familia zinadhilika ,wototo Kama unavyojua shule za private, hawpokelewi bila ada, shule zimefunguliwa January, February hii bado kizungumkuti watoto wako stranded majumbani, huruma mkuu

Mkuu wacha tu, naijua hiyo hali na hasa ukizingatia waajiriwa wengi huwa hawana ujanja nje ya ajira na tena ukizangatia wamepoteza ghafla.
 
Back
Top Bottom