Niimembusu dada wa kazi wa nyumbani kwangu, mke wangu nisaidie...

lolipo

JF-Expert Member
Apr 6, 2018
739
912
Ndugu zangu mimi nina ndoa ya miaka 12, na nina watoto wanne. Nina degree moja na mke wangu ana degree mbili. najitahidi kutimiza mahitaji ya Nyumbani kwa hiyo Mke wangu na mimi wote tuna magari na ninajitahidi sana kubeba majukumu yangu nyumbani vizuri. Nampenda mke wangu na kwa uelewa wangu, ni mwaminifu hana shida.

Matatizo ya mke wa

- Hapendi kupika kabisa.
- Ni mvivu, mara nyingi anaangalia tv chumbani, na tamthiliya.
- Tendo la ndo limekuwa kero kabisa, utahangaika sana na ukilipata anafanya kama wajibu.

Dada wa kazi:

- Anafanya kazi zote, kupika, kudeki, kufua na kuwaandaa watoto.
- Anaamka wa kwanza anaogesha watoto wanne, anawavalisha, anawapa chakula wawahi shule.
- Ananijali mno, mno, kuangalia sox, vest, kila kitu kiko sawa.

Nimekaa na huyu Dada kwa miaka 4, sikuwahi kumfikiri, kumtamani wala kumuwaza, ila kuna namna nimeanza kumpenda! Sijawahi kum cheat mke wangu, hata siku moja, kuna namna jana Dada wa kazi kanihudumia, na wakati natoka niliingiwa na kitu jichoni, kakitoa mpaka kikatoka, wakati ananipuliza puliza, mwili ukawa wanigusa, gusa, feelings, nikamkumbatia, mwishowe nikambusu.

Akabutwaa na akaonesha ushirikiano, nimeshtuka sana, na presha, ninajua mke hata leo nikitaka mapenzi anaweza akaleta longo longo, nikaamua nisirudi home kabisa, maana tunafanya ukaguzi Bagamoyo na ninaweza nisingizie kutokurudi Nyumbani!

OMBI: MKE WANGU BADILIKA, NAJUA UNAPITA HUKU, NIKIMUONJA HUYU DADA MIMI SIJUI NINI KITAENDELEA, MIMI SIJUI, USINICHUKULIE POA UUNGWANA WANGU. NIMESEMA IDADI YA WATOTO NA KILA KITU ILI ANGALAU UJUE NI MIMI!
 
Nina degeree moja anazo mbili.

Nina watoto wanne

Natimiza mahitaji.

Tuna magari ,

Najitahidi kubeba majukumu ya nyumban vzuri

Nampenda mke wangu.

Kwa uelewa wangu ni mwaminifu.

Nimesema na idadi ya watoto ili "angalau" unijue ni mimi.


Nimemkiss House girl ......mke wangu nisaidie !!??????????.
 
Wewe ni mwanaume suruali kweli si umface tu mkeo direct naona shetani wakuvunja ndoa yako kashabisha hodi mlangoni, angalia usiue ndoa yake
 
Nimeishi naye miaka 12, nina watoto 4, mpaka nimefika hapa, ujue nimejaribu sana kumihi. Imetosha sasa.
Hata wewe utakuwa na mapungufu yako anakuvumilia usimpe ibilisi nafasi ka mumeishi 12 years ukiona hata atakuwa hana hamu, maana njia za uzazi hufanya wanawake wasiwe na affection. Pia jaribuni kutoka out sehemu tofauti tofauti, huyo kakuzalia watoto wa 4 so kumfikiria tofauti ni kosa ongea naye vzuri, usivunje ndoa kwa tamaa ya beki Tatu aisee wanawake huwa wana mengi yanayo ua hisia za Ku do.
 
Back
Top Bottom