Nigeria yaiduwaza Ufaransa kwa ushindi wa 1-0 mjini St Etienne

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,147
Nigeria yaiduwaza Ufaransa kwa ushindi wa 1-0 mjini St Etienne

ST ETIENNE, Ufaransa

NIGERIA imeiduwaza Ufaransa baada ya kuilaza kwa bao 1-0 katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa juzi mjini hapa.


Kama ilivyokuwa kwa Senegal katika fainali za Kombe la Dunia mwaka 2002, Ufaransa chini ya Raymond Domenech imejikuta ikilala Jumanne kwa Super Eagles.


Bao la Joseph Akpala, 22 anayeichezea klabu ya Club Brugge, Ubelgiji, dakika ya 32 baada ya kupokea pasi murua ya Ikechukwu Uche na kugonga kwanza mwamba na kumchanganya kipa Steve Mandanda.


Mashabiki wa Ufaransa walikasirishwa na bao hilo na kuanza kuwazomea wachezaji wa nchi yao ambao walikuwa naye nahodha Patrick Vieira aliyekuwa majeruhi kwa muda mrefu na winga wa Chelsea, Florent Malouda.


Hata hivyo, si Vieira au Malouda aliyeng'ara katika mchezo huo, ingawa Vieira alionekana mzito na kushindwa kuchangamka katika mchezo wake wa107 akiichezea Les Bleus.


Kwa zaidi ya saa nzima, mashabiki wa Ufaransa walikuwa kimya na hatimaye walianza kuwataka wachezaji wao waamke na kuchangamka, huku Franck Ribery na Nicolas Anelka, peke yao waking'ara.


Loic Remy aliyeichezea nchi yake kwa mara ya kwanza alikaribia kuipa bao la kusawazisha baada ya mshambuliaji huyo wa Nice kugonga mwamba dakika ya 88 ya mchezo.


Kocha Domenech hakutarajia kukaribisha vizuri mjini St Etienne , mahali ambako anakumbukwa zama zaka wakati akiichezea wapinzani wa kihistoria, Olympique Lyon.


Hilo lilidhihirika wazi baada ya majina ya kikosi cha Ufaransa kutajwa kupitia vipaza sauti uwanjani likiwamo la Domenech na wachezaji wa zamani Lyon walizomewa na mashabiki. Wengi wao walieleza kusikitishwa na kuporomoka kwa kiwango cha timu hiyo.


Kwa dakika moja, mashabiki walitulia kimya kuwakumbuka abiria 228 wa ndege ya Air France waliopotea Jumatatu wakitokea Rio de Janeiro, Brazil kuelekea Paris.


Kesho, Ufaransa itakuwa na mchezo mwingine wa kirafiki dhidi ya Uturuki
 
Hi JF members!
Am a new mwmber, hoping to exchange ideas, information, knowledge, experience etc with JF members.
Regards
 
Hi JF members!
Am a new mwmber, hoping to exchange ideas, information, knowledge, experience etc with JF members.
Regards

UR WELCOME MAIRO.....HAPPY THURSDAY
 
Back
Top Bottom