Nigeria yaanza kuwaondoa raia wake walioko Afrika Kusini

miss zomboko

miss zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Messages
2,164
Points
2,000
miss zomboko

miss zomboko

JF-Expert Member
Joined May 18, 2014
2,164 2,000

Watu zaidi ya 12 waliuawa katika ghasia zinazotokana na chuki Afrika Kusini.

Nigeria imeanza zoezi la kuwaondoa raia wake waishio nchini Afrika Kusini, ambao wameoredheshwa kwenye ubalozi wa nchi hiyo nchini Afrika Kusini.

Watu 640 ndio wanatarajiwa kusafirishwa kutoka Johannesburg kwenga Nigeria.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na wizara ya mambo ya nchi za nje ya Nigeria kwenye ukurasa wake wa twitter inakadiriwa kuwa idadi ya raia 313 watachukuliwa kutoka Afrika Kusini katika awamu ya kwanza na waliosalia watasafirishwa siku za Alhamisi na Ijumaa wiki hii.

Serikali ya Nigeria tayari iliwaonya raia wake waliopo Afrika Kusini wasisafiri ama kuelekea kwenye maeneo ambayo ghasia hizo zimeshamiri mpaka pale hali itakapotengemaa.

Wizara ya mambo ya Nje ya Nigeria ilisema mmliliki wa Shirika la Ndege la Air Peace yupo tayari kuwasafirisha bure wale wote watakaotaka siku ya Ijumaa.

Awali waziri wa Mambo ya Nje wa Nigeria Geoffrey Onyeama aliwaambia wanahabari siku ya Jumatano wiki iliyopita kuwa kulingana na taarifa zilizowafikia, hakuna raia wa Nigeria aliyepoteza uhai kwenye ghasia zinazoendelea.

Rais Muhammadu Buhari alisema kuwa anamtuma mwakilishi wake kwenda Afrika Kusini kueleza 'ghadhabu' zao juu vurugu zinazoendelea.

Hatua hiyo inakuja wakati uhusiano kati ya nchi hizo mbili umeanza kuwa mzuri, baada ya kukumbwa hali ya sintofahamu kwa wiki moja iliyopita .

Baada ya mvutano wa siku kadhaa, Abuja ilimtuma mjumbe wake kwenda Afrika Kusini na ikasema kwamba inataka kutafuta suluhisho na Pretoria. Na wakuu wa nchi hizi mbili wanatarajia kukutana mapema mwezi Oktoba nchini Afrika Kusini.

Mvutano kati ya nchi hizi mbili zenye nguvu kiuchumi barani Afrika unaweza kusababisha athari kubwa. Wiki iliyopita, Nigeria ilisusia Mkutano wa Uchumi wa Dunia uliofanyika jijini Cap, nchini Afrika Kusini.

Mtu mwengine aliuawa Johannesburg, mwishoni mwa wiki hii iliyopita na kufikia 12 idadi ya watu kutoka nchi za kigeni ambao wameuawa katika ghasia zinazochochewa na chuki dhidi ya wageni zilizozuka tangu wiki iliyopita nchini humo.
 
Hawachi

Hawachi

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2018
Messages
7,332
Points
2,000
Hawachi

Hawachi

JF-Expert Member
Joined Nov 25, 2018
7,332 2,000
Wameamua jambo la msingi.
 
N

Nyanjomigire

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2013
Messages
4,050
Points
2,000
N

Nyanjomigire

JF-Expert Member
Joined Jan 28, 2013
4,050 2,000
Afadhali wameliona hilo.
 
J

jumamwaki

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2017
Messages
233
Points
250
J

jumamwaki

JF-Expert Member
Joined Dec 4, 2017
233 250
Ngoja na sisi tuanze kuwasafirisha wa Africa kusini🙄🙄
 
T

Tissaphernes

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2018
Messages
2,017
Points
2,000
T

Tissaphernes

JF-Expert Member
Joined Mar 27, 2018
2,017 2,000
Nimeona wameondoka na kesho wanaondoka wengine pia
 
P

Pohamba

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2015
Messages
21,027
Points
2,000
P

Pohamba

JF-Expert Member
Joined Jun 2, 2015
21,027 2,000
Tuiache South Africa ipumue wafaidi Nchi yao

Wamepambana kuondoa Wavamizi wa Kidachi kwa zaid ya karne 4 kuanzia 1652 mpaka 1994 then hata hawajapumzika Tunaanza kuvamia tena Nchi yao!

Sie hapa tunalalamika wachina na Wakenya wanachukua ajira zetu lakin tunalaumu Wa South wakilinda ajira zao
 
Mtafiti77

Mtafiti77

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2011
Messages
787
Points
1,000
Mtafiti77

Mtafiti77

JF-Expert Member
Joined Oct 31, 2011
787 1,000
Ninadhani mnaorudi mtakuwa na mtazamo mwingine sasa kuhusu maisha. Poleni sana!
 
jiwekuu770

jiwekuu770

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2015
Messages
1,495
Points
2,000
jiwekuu770

jiwekuu770

JF-Expert Member
Joined Feb 12, 2015
1,495 2,000
Tanzania sijui

Watu zaidi ya 12 waliuawa katika ghasia zinazotokana na chuki Afrika Kusini.

Nigeria imeanza zoezi la kuwaondoa raia wake waishio nchini Afrika Kusini, ambao wameoredheshwa kwenye ubalozi wa nchi hiyo nchini Afrika Kusini.

Watu 640 ndio wanatarajiwa kusafirishwa kutoka Johannesburg kwenga Nigeria.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na wizara ya mambo ya nchi za nje ya Nigeria kwenye ukurasa wake wa twitter inakadiriwa kuwa idadi ya raia 313 watachukuliwa kutoka Afrika Kusini katika awamu ya kwanza na waliosalia watasafirishwa siku za Alhamisi na Ijumaa wiki hii.

Serikali ya Nigeria tayari iliwaonya raia wake waliopo Afrika Kusini wasisafiri ama kuelekea kwenye maeneo ambayo ghasia hizo zimeshamiri mpaka pale hali itakapotengemaa.

Wizara ya mambo ya Nje ya Nigeria ilisema mmliliki wa Shirika la Ndege la Air Peace yupo tayari kuwasafirisha bure wale wote watakaotaka siku ya Ijumaa.

Awali waziri wa Mambo ya Nje wa Nigeria Geoffrey Onyeama aliwaambia wanahabari siku ya Jumatano wiki iliyopita kuwa kulingana na taarifa zilizowafikia, hakuna raia wa Nigeria aliyepoteza uhai kwenye ghasia zinazoendelea.

Rais Muhammadu Buhari alisema kuwa anamtuma mwakilishi wake kwenda Afrika Kusini kueleza 'ghadhabu' zao juu vurugu zinazoendelea.

Hatua hiyo inakuja wakati uhusiano kati ya nchi hizo mbili umeanza kuwa mzuri, baada ya kukumbwa hali ya sintofahamu kwa wiki moja iliyopita .

Baada ya mvutano wa siku kadhaa, Abuja ilimtuma mjumbe wake kwenda Afrika Kusini na ikasema kwamba inataka kutafuta suluhisho na Pretoria. Na wakuu wa nchi hizi mbili wanatarajia kukutana mapema mwezi Oktoba nchini Afrika Kusini.

Mvutano kati ya nchi hizi mbili zenye nguvu kiuchumi barani Afrika unaweza kusababisha athari kubwa. Wiki iliyopita, Nigeria ilisusia Mkutano wa Uchumi wa Dunia uliofanyika jijini Cap, nchini Afrika Kusini.

Mtu mwengine aliuawa Johannesburg, mwishoni mwa wiki hii iliyopita na kufikia 12 idadi ya watu kutoka nchi za kigeni ambao wameuawa katika ghasia zinazochochewa na chuki dhidi ya wageni zilizozuka tangu wiki iliyopita nchini humo.
 
Forum statistics

Threads 1,335,176
Members 512,245
Posts 32,498,030
Top