Nigeria ya Sani Abacha inanikumbusha mbali jinsi alivyotaka kummaliza Abiola akatangulia yeye

Mwemary

JF-Expert Member
May 25, 2016
330
340
Nigeria ni miongoni mwa Nchi zilizokumbwa ghiriba nyingi kisiasa.Ikiwa ni mapinduzi ya mara kwa mara yaliyosababisha kimwagika kwa damu na mangine kwa njia ya Amani.

Katika mapinduzi hayo yalifanikiwa kumuweka madarakani General Sani abacha baaada ya kumpindua general baba ngida (niko tayari kukosolewa kama nimekosea).

Katika utawala wa abacha yeye ndio alikuwa final sayer wakila kitu.Aliliteka bunge na mahakama na zikawa hazina maaamuzi mpaka yeye apigiwe simu.

Baraza la mawaziri yeye ndo alikuwa anamaamuzi ya mwisho na hakutaka kupingwa ulikuwa ukimpinga tuuu yatakayokukuta wewe familia
wengine hawatothubutu.

Bunge ( baraza la seneti) lilifanya maamuzi yake kwa kurusiwa na Raisi. mfano kuuunda baraza la seneti liliunda kamati za kwa kuangalia raisi anataka nini.

Mfano kuonyesha kwamba yeye anamaamuzi aliwahaidi waaandishi wa habari kwamba watanyongwa na kweli mahakama iliwahukumu kunyongwa mpaka kufa.

Ni kweli walinyongwa mpaka kufa ingawa dunia ilipiga kelele wasinyongwe .Nchi ili wekewa vikwazo.Pia alijaza ndugu zake na kabila la benki kuu ya Taifa hivyo kufanya upolaji mkubwa wa rasimali za nchi.

Na ni miongoni mwa marais wakiafrika ambao walijilimbikizia mali nyingi mpaka kabila na ndugu zao waliongoza kwa kuwa na ukwasi usio na kifani. mwaka 1997 uliitishwa uchagu wa kidemokrasi kama wa huku kwetu kati ya abacha na abiola.

Abacha alishindwa na abiola baada ya kuona ameshindwa akamfunga gerezani abiola na kumpulizia sumu ya kumuuwa tarratibu. lakini bahati mbaya yeye ndo alianza kufa kifo dhalili akiwa gesti na mademu wawili wa kihindi huku akimuacha abiola gerezani ambapo baaadae nae alifariki.

General Abdulsalam abukari alishika usukani kuongoza nchi kwa mda na baadae uliitishwa uchaguzi wa kidemkrasia na yeye hakugombea.

MY TAKE:
1.Haya mambo tulikuwa tunayasoma na kuyasikia nchi za watu sasa hivi yametukuta na sisi.Watu kujaza makabila yao kwenye nafasi nyeti za serikali huku baadhi wengine wakiachwa.

UNyanyasaji unaofanywa sasa hivi matunda yake yataonekana baaadae kwanini tusiijenge nchi yetu kwa kushirikisha mawazo yote uwe unayapenda au uyapendi.

Hoja hujibiwa kwa hoja sio risasi kaka bashite hakuna mtu bora zaidi ya muingine.

kwa taarifa ambazo si rasmi bashite anaandaliwa kuwa waziri wa mambo ya ndani kwa hiyo tujiandae kwa uasi zaidi utakaofanywa dhid ya wapingaji wa baba yake.

Mimi naomba aliyeumba Mbigu na Ardhi waliouwa viongozi wetu kibiti na waliompiga Risasi Tundu lissu Awaadabishe.

Bashite na baba yake waendeshe nchi vizuri sio kwa kukamata na kumiminiana Risasi
 
Ukabila hauta kuja kuisha mpaka mwisho wa dunia. Ulaya kuna undugu na ukabila katika kazi zote na ndio maana mataifa kama ujerumani waliamua kuwaua waisrael maana sehemu za akili walikuwa wayahudi. Cha Msingi katika hii dunia mtu unatakiwa utumie akili zaidi katika maisha kuliko kubembeleza kuonewa uruma. Dunia aipo kwenye kuoneana huruma, ndio maana wazungu wanavyokuja kuiba madini Africa hawajui kama sisi waafrika inatuuuma.
Kila mwenye uelewa na akili anajua sekta kalibia zote apa Tanzania zimekaliwa na makabila gani? Kitendo cha makabila hayo kutumbuliwa kunaleta kwamba kuna kuonewa.
 
Mkuu mleta mada punguza uoga. Nigeria ilianza na ukabila na uchifu, matokeo yake mpaka leo hii mgawanyiko ni mkubwa.

Igbo anamkejeli Yoruba, Hausa fulani anamchukia Igbo, lakini msingi wa hayo ya Nigeria kwa hapa kwetu ulisagwasagwa kupitia maono ya Hayati Julius Nyerere aliyezipiga marufuku mbwembwe za uchifu.

Kuingia madarakani kwa Abacha kunatofautiana sana na kuingia madarakani kwa JPM. Na hayo mambo ya ukabila na urafiki yapo Afrika nzima kuanzia kusini mpaka kaskazini.

Kumbuka namna ambavyo watu wa kabila fulani walivyokuwa na ushawishi enzi za mzee Benjamini, kwa sababu tu alioa kwao. Kumbuka enzi za Mwinyi watu fulani walivyokuwa na nguvu mpaka kutaka kuanzisha chama cha kisiasa ingawa wao msingi wao ulikuwa ni chama cha mapinduzi.

Hivyo yanayoendelea wala yasikutishe, ni sehemu za changamoto za uhai wa mwanadamu akiwa bado anapumua.
 
Kama RC Makonda anaandaliwa kuwa waziri wa mambo ya ndani basi tuombe mungu iwe hivyo maana ni mchapakazi sana anastahili (he deserve)
 
Ukabila hauta kuja kuisha mpaka mwisho wa dunia. Ulaya kuna undugu na ukabila katika kazi zote na ndio maana mataifa kama ujerumani waliamua kuwaua waisrael maana sehemu za akili walikuwa wayahudi. Cha Msingi katika hii dunia mtu unatakiwa utumie akili zaidi katika maisha kuliko kubembeleza kuonewa uruma. Dunia aipo kwenye kuoneana huruma, ndio maana wazungu wanavyokuja kuiba madini Africa hawajui kama sisi waafrika inatuuuma.
Kila mwenye uelewa na akili anajua sekta kalibia zote apa Tanzania zimekaliwa na makabila gani? Kitendo cha makabila hayo kutumbuliwa kunaleta kwamba kuna kuonewa.
Kuna makabila yanatumbuliwa au kuna mtu anaweka watu wa kabila lake kila sekta nyeti akianzia na hazina?
 
Umekumbusha Mbali kiasi
Mwandishi alienyongwa aliitwa Ken Sarowiwa jumla walikuwa 18

Sani Abacha hakugombea na Mashoud Abiola bali alifuta Matokeo na kutawala kijeshi

Nigeria ilizuiwa kushiriki Kombe la Africa lililofanyika 1996 Nchini Africa kusini kwa kunyonga Waandishi na Matokeo yake ikawezesha Bafana bafana ichukue Kombe kwa kuwafunga Tunisia mbili bila

Abacha alikufa kwa kutumia Viagra kupita kiasi

Mashoud Abiola ndio aliekuwa akidhamini Mashindano ya Kombe la CAF ambalo Simba ilifika Fainali 1993

All in All sote ni wapitaji hapa Duniani Tujisahihishe na tuwe Fair kwa Qur an inasema tutaulizwa kwa kila Jambo tunalofanya Duniani liwe la kheri au laa cha Msingi tujue We are Liable kwa Mungu kwa Matendo yetu
 
Back
Top Bottom