Nigeria: Watu 24 wa familia moja wafariki kwa kula sumu

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,813
4,545
Watu 24 wa familia moja wamefariki dunia baada ya kula chakula kinachohisiwa kuwa na sumu Kaskazini Magharibi mwa Nigeria katika jimbo la Sokoto.

Kamishna wa Afya wa jimbo hilo, Ali Inname amewaambia waandishi wa habari kwamba familia hiyo ilitumia kimakosa kemikali ya mbolea ambayo ilionekana kama chumvi wakati wa kuandaa chakula.

Inname amesema wahudumu wa afya walijaribu kuokoa maisha ya wahanga hao bila mafanikio.

Hata hivyo watu wawili wa familia hiyo ambao walionja tu chakula hicho wanaendelea kupata matibabu hospitalini.
Baada ya tukio hilo, maofisa wametoa wito kwa watu kuweka vitu vyenye sumu mbali na maghala ya chakula kwa sababu za usalama
 
Back
Top Bottom