Sam Gidori
Senior Member
- Sep 7, 2020
- 165
- 414
Mwanasheria Mkuu wa Nigeria, Jenerali Abubakar Malami ameagiza kufunguliwa mashtaka mara moja kwa watu wote watakaokaidi agizo la serikali la kufungia mtandao wa kijamii wa Twitter.
Mapema jana, makampuni ya simu nchini humo yalisema kuwa yametii agizo la serikali la kufungia mtandao huo wa kijamii, ikiwa ni siku mbili tu baada ya mtandao huo kufuta chapisho la Rais Muhammadu Buhari kwa madai ya kuvunja sheria zake na kuifungia akaunti yake kwa muda wa saa 12.
Chama cha Watoa Huduma za Mitandao Waliosajiliwa nchini humo (ALTON) kimesema kuwa wanachama wake wamepokea maelekezo rasmi kutoka serikalini kuwataka kufungia mtandao wa Twitter nchini Nigeria. Mtandao huo unaweza kupatikana kwa watumiaji wanaotumia Virtua Private Network (VPN).
Wizara ya Habari ilitangaza siku ya Ijumaa kuwa serikali imesitisha kwa muda usiojulikana huduma za mtandao wa Twitter kutokana na mtandao huo kujihusisha na shughuli zinazohatarisha uthabiti wa taifa hilo. Taarifa hiyo haijaeleza chapisho la Rais Buhari lililofutwa wala akaunti yake kufungiwa.
Twitter, yenye zaidi ya wateja milioni 40 nchini Nigeria, imejitetea kuwa imechukua hatua hiyo kutokana na chapisho la Buhari kukiuka kanuni zake, na kueleza kuwa hatua ya Nigeria kusitisha huduma zake ni ya kusikitisha. Imeongeza kuwa inachunguza na itatoa maelezo zaidi pale itakapopata taarifa kamili.
Hatua ya Serikali ya Nigeria imekosolewa na watumiaji na wanaharakati wengi, huku baadhi yao wakitishia kuichukulia serikali hatua za kisheria kwa kuzuia Uhuru wa Kutoa Maoni.
Chanzo: Al Jazeera