Nigeria: Mamlaka yakosolewa baada ya kisa cha utekaji nyara wa Wanafunzi 70

Shadow7

JF-Expert Member
Sep 28, 2020
13,766
20,154
Jitihada zinaendelea kujaribu kuwaachilia zaidi ya wanafunzi 70 wa shule ya upili waliotekwa nyara Jumatano katika jimbo la Zamfara, kaskazini magharibi mwa Nigeria.

Kisa hiki cha utekaji nyara wa wanafunzi 73 kutoka shule ya upili ya Kaya na watu wenye silaha ni miongoni mwa mlolongo wa visa vya utekaji nyara vilivyolenga shule katika miezi michache.

Tangu wakati huo usalama umeimarishwa katika kijiji cha Kaya na viunga vyake ili kuzuia mashambulizi zaidi. Wengi wanasema jitihada hizo, zimekuja zikiwa zimechelewa.

Tangu kisa hicho cha utekaji nyara, mamlaka katika Jimbo la Zamfara imeweka vizuizi vya kusafiri usiku na wamefunga kwa muda shule za msingi na sekondari. Lakini hii haitoshi kutuliza hasira za wakaazi wa jimbo hilo, ambao hukosoa serikali kwa kutowajibika.

Hasa wakati shule hiyo ya upili ambapo wanafunzi walitekwa nyara inapatikana kilomita chache tu kutoka makao makuu ya serikali za mitaa huko Maradun.

Kwa miezi kadhaa, visa vya utekaji nyara shuleni vimekuwa vikiongezeka katika majimbo ya kaskazini na kati ya nchi. Karibu wanafunzi 1,000 wametekwa nyara tangu kuanza kwa mwaka huu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom