Nigeria: Magaidi wauana wao kwa wao

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,861
Wapiganaji wa Boko Haram ambao ni watiifu kwa Abubakar Shekau walivamia kambi moja ya kundi hasimu ya kundi linalojiita Dola la Kiislamu la Afrika Magharibi (ISWAP) na kusababisha makabiliano makali ya risasi ambayo yalisababisha vifo vingi

Mapigano makali ya kufyatuliana risasi kati ya makundi mawili ya itikadi kali kaskazini mashariki mwa Nigeria yamesababisha wapiganaji wengi kuuwawa

Wapiganaji wa Boko Haram waliishambulia kambi ya kijiji cha Sunnawa katika wilaya ya Abadam karibu na mpaka na Niger

Wanamgambo wa kundi la ISWAP awali waliwavamia Boko Haram katika eneo la Diffa lililoko jirani ya Nigeria ambako waliwateka nyara wanawake 13


Chanzo: DW
 
Waislamu kwa kutwangana wenyewe kwa wenyewe hawajambo.Somalia nako hivyo hivyo
 
Sasa kama makundi ya kigaid yanafantiana Ambushi na kambi zao zinajulikana selikali ya nigeria na jeshi lake yenyewe inakwama wapi kuwapiga msako na Ambush hawo magaid kwenye camp zao?

Au ndo akiri kumkichwa?

Sent using Jamii Forums mobile app
Alafu ni nchi yenye uchumi mzuri na miongoni mwaka nchi zenye Jeshi lenye nguvu Africa. Sijui serikali yao inakwama wapi magaidi wanateka wanawake na kuharibu vijiji daily
 
Sasa kama makundi ya kigaid yanafantiana Ambushi na kambi zao zinajulikana selikali ya nigeria na jeshi lake yenyewe inakwama wapi kuwapiga msako na Ambush hawo magaid kwenye camp zao?

Au ndo akiri kumkichwa?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata mimi huwa sielewi kwamba hawa watu wapo ndani ya nchi husika kuna jeshi, usalama, polisi, magereza, mgambo, wananchi watiifu, vifaru,mawasiliano kila kitu sasa kwa nini washindwe kufanya msako wa nguvu pori kwa pori, nyumba kwa nyumba, mlima kwa mlima, bonde kwa bonde, mto kwa mto, msikiti kwa msikiti na kanisa kwa kanisa mpaka kieleweke fagia wote weka masaa ya 24 ya hatari kwa miez yote 12

Kuna kipindi waliwateka sijui watoto karibia 300 wasichana kwa wavulana huku wakiwabaka kwa kweli kama ni kweli roho ilinichafuka sana nikawa najiuliza hakuna vyombo vya ulinzi huko?

Eti wanadai nigeria wana jeshi zuri kwa africa sasa kwa nini washindwe kukamaliza kakikundi kama hicho hakuna jeshi huko wapumbafu tu majigambo yanawasumbua

Nchi nyingi za africa wana majeshi ya kulinda viongozi tu kwenye mission hakuna kitu sasa huyo mkuu wa majeshi analala,kula na kunya bila wasiwasi wowote wakati ndani ya nchi kuna kikundi cha waasi kweli inaingia akilini

Wangelikuwa ndio JWTZ kwa kweli wangekuwa wanacheka na ndugu zao

Juzi wanamwonyesha Rais Buhari na baadhi ya maraisi wa africa wengine wanatoka east africa wanajadili sijui uwekezaji sijui ujinga gani yanacheka cheka kama mafala. Mikutano ya kujikomba komba hawaachi kwenda kwa nini wasiifanye hiyo mikutano ndani ya africa kwanza

Pongezi kwa Raisi wetu kutohudhuria mikutano ya mabeberu isiyoeleweka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nahisi ile ni biashara ya watu. Haiwezekani nchi yenye jeshi imara lenye vifaa vya kisasa kama Nigeria ishindwe kumaliza kikundi cha waasi cha Boko Haramu.
Alafu ni nchi yenye uchumi mzuri na miongoni mwaka nchi zenye Jeshi lenye nguvu Africa. Sijui serikali yao inakwama wapi magaidi wanateka wanawake na kuharibu vijiji daily

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom