Nigeria: Klabu ya Plateau yagoma mchezo wake dhidi ya Simba Sc unaweza usiruke 'Live'

Mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa kati ya Plateau United dhidi ya Simba ambao utapigwa baadae leo uwanja wa New Jos huko Nigeria, hautaonyeshwa mbashara

Imeelezwa kuwa maafisa wa Plateau United wamegoma mchezo huo kurushwa mbashara licha ya juhudi kufanywa na Ubalozi wa Tanzania nchini Nigeria kuomba Azam TV wapewe haki ya kuonyesha mchezo huo

Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Dk Benson Bana amesema Plateau United wamegoma mchezo huo kurushwa mbashara hivyo amewataka Watanzania kuiombea Simba iweze kufanya vizuri kwenye mchezo huo

Uongozi wa klabu ya Simba umethibitisha kuwa mchezo huo hautakuwa mbashara kwenye kituo chochote cha televisheni

"Kwa masikitiko tunawajulisha Wanasimba na Watanzania wote kwamba mchezo wetu wa kesho dhidi ya Plateau United hautaonyeshwa mbashara baada ya wenyeji wetu Plateau kuzuia matangazo ya moja kwa moja ya mchezo huo"

Hakuna chombo chochoto kitakachoonyesha mkuu...
Mhh, inawezekana Simba ndio hawataki uonekane mubashara kwa kuogopa aibu.
 
mkuu hujajibu swali lililoulizwa
 
This is africa my friend! Cuf nao wamekaa kimya katika hili. Kama kila timu ikifanya hivi haya mashindano yatakuwa ya kijinga kabisa kupata kutokea.
Unaulizwa sababu ni zipi unatoa malalamiko. Mechi huwa hairushwi tu kienyeji bila kununua haki ya matangazo kwa timu husika. Sasa kwanini tunatanguliza kauli za kuhujumiwa badala ya kuletwa humu ni kwanini Plateau wamekataa mechi isioneshwe live. Tunatanguliza imani ya hujuma pasipo kutaka kujua sababu zao ni zipi.
 
Wazee wa tano tano ugenini wanaogopa aibu kuwaona wakilambwa live. Janja yao imewekwa wazi. Plateau hawana issue kabisa.
 
Nafkiri wakija bongo wanaweza kupelekwa gesti za kwa tumbo na umeme utakatwa ghafla huku gesti hiyo ikifungwa milango yote hadi siku ya mechi ikifika ndo wanafunguliwa wakacheze mpira na simba
 
Back
Top Bottom