Nigeria: Fedha za rushwa za rais mstaafu zataifishwa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,499
9,279
f3a6715d3325d47e4a49353338061751

Zaidi ya Dola za Marekani 267 milioni (zaidi ya Sh600 bilioni) zilizofichwa na Rais wa zamani wa Nigeria, San Abacha katika benki moja katika kisiwa cha Jersey zimetaifishwa.

Fedha hizo zilipatikana kwa njia za rushwa wakati wa kipindi chake cha utawala miaka ya 1990, zikiwa chini ya kampuni feki iliyoitwa Doraville iliyofilisiwa kwama 2014.

Baada ya mitano ya kisheria kupita, fedha hizo zimetaifishwa na sasa zitagawanywa kati ya Jersey, Marekani na Nigeria, umeeleza mfuko maalumu wa mali zilizotaifishwa.

Mwanasheria mkuu wa Jersey, Robert McRae QC alisema utaifishaji huo umeonyesha nia ya dhati ya nchi hiyo katika mapambano dhidi ya uhalifu wa kimataifa wa kifedha na utakatishaji wa fedha.

San Abacha alikuwa madarakani kati ya mwaka 1993 hadi kifo chake mwaka 1998.

Haikufahamika mara moja ni kiwango gani cha fedha kila nchi itapata katika mgawo huo.

Maofisa wa idara ya sheria ya Jersey hawakutaka kuzungumzia mgao huo kwa sababu “wangeingilia mazungumzo yanayoendelea kuhusu suala hilo.”

Serikali ya Jersey ilisema iliwasiliana na marekani mwaka 2007 kuomba hatua za kisheria zichukuliwe katika mahakama za Marekani kuhusu utakatishaji wa fedha hizo.

Idara ya Sheria ya Marekani pia ilirejesha mamilioni ya dola nchini Nigeria, baada ya hukumu kuwa Abacha na washirika wake walikuwa wameyatakatisha kupitia benki za nchi hiyo.

Kupitia ushahidi uliokusanywa kwa kina katika nchi mbalimbali, fedha hizo zilitaifishwa na mahakama mwaka 2014 na baadaye kulipwa katika mfuko maalumu wa kutunza mali zilizotaifishwa Mei 31 mwaka huu.

Fedha hizo ni kiasi kigodo tu cha mabilioni ya dola yanayodaiwa kuibwa na kutakatishwa katika kipindi cha utawala wa Abacha nchini Nigeria.

Mwaka jana mamlaka za Uswisi zilirejesha Dola 300 milioni za Marekani (Sh675 bilioni) kwa Serikali ya Nigeria baada ya kubainika ziliibwa serikalini.

Fedha hizo zinaendelea kulipwa kwa raia 300,000 wa Nigeria kwa miaka sita ijayo.

Msemaji wa idara ya sheria ya Jersey alisema kutoka fedha hizo, ofisi yake ilipata msukosuko na rufaa kadhaa hadi Mahakama Kuu katika kesi mbadala, sambamba na ile iliyokuwa inaendelea katika mahakama ya Marekani.
 
Mabeberu bhwana sasa kwanini wagawane? Wao Kama benki si wachukue charge yao tu? Nigeria musikubali
 
Mtu amekaa miaka mitano tu ameiba pesa yote hio,halafu anaenda kuficha nje,anakufa watu wanagawana,mbaya zaidi ambao hata hawahusiki
 
Back
Top Bottom