Nigeria; Atiwa mbaroni kwa kuuza watoto pacha

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,237
2,000
Mwanamke mmoja nchini Nigeria amekamatwa na polisi baada ya kujaribu kuwauza watoto wake pacha wenye umri wa mwezi mmoja akidai kuwa chanagamoto za pesa zimemsukua kufanya kitendo hiko. Mwanamke huyo amekamatwa wakati akijaribu kuuza watoto wake kwa dola 980 kwa mnunuzi ambaye aliwajulisha polisi.

Hata hivyo tabia hiyo nchini Nigeria imekithiri kwa kiwango kikubwa na kwa muda mrefu nchini humo.

Mwaka 2013 wasichana wajawazito 17 na watoto 11 waliokolewa wakati polisi walipovamia “kiwanda cha watoto” katika jimbo la Imo. Miaka miwili baada ya sakata hiyo, mwanamke mwingine alishikwa alipokuwa akijaribu kumuuza mtoto wake kwa dola 90 katika jimbo la Cross River.

Nigeria ni nchi inayoongoza kwa uzalishaji wa mafuta lakini asilimia kubwa ya watu zaidi ya milioni 170 wanaishi kwenye umasikini.Dar 24
 

adden

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
5,244
2,000
Hata mi nahisi niliuzwa wakati nikiwa mdogo.maana sifanani na mtu yoyote ktk ukoo
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom