Ufafanuzi na Mchanganuo Kuhusu Biashara ya Vipodozi na Urembo

Dah! Mkuu kwa huo mtaji ningeupata mimi ningefungua duka la vifaa vya ujenzi. Vipodozi ni biashara nzuri ila ina risk sana, hasa wakija wakaguzi na ujue pia asilimia 90 ya vipodozi vinavyouzika ni vile vilivyopigwa marufuku na mamlaka ya chakula na dawa Tanzania!

Wengi huletewa mzigo toka zambia na kongo na watu wenye mitaji mikubwa ,wanaojuana na wakubwa serikalini
ukitaka kufungua , jaribu kufanya utafiti na mwenge!

Nakutakia maamuzi yenye mafanikio mema!
Biashara ya vifaa vya ujenzi si inahitaji mtaji mkubwa sana au unaanza kuuza vile vya kawaida tu ebu toa maelezo kwa, mwenye mtaji mdogo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Salaam,

Natumai muwazima wa afya, yoyote atakae bahatika kuuona uzi huu basi asiache kutoa chochote kitu ambacho kitanisaidia sana kuongeza maarifa katika hii maada niliyo ileta kwenu nikiamini kabisa kuwa nyie ndio watu wa pekee wa kunipa msaada kimawazo

Natamani na napenda sana kufanya biashara ya vipodozi (cosmetics) nasikia tu kwa watu kuwa ina mslahi sana lakini changamoto ni kwamba Sina ufahamu mkubwa sana kuhusu biashara hii mfano nilishajiuliza maswali kama.

1. Ni kiasi gani cha mtaji kinahitajika (minimum amount of capital)
2. Ni vipodozi vya aina gani vyenye uhitaji mkubwa sana sokoni(consumer needs)
3. Ni vipodozi gani vina faida kubwa sana
4. Hasara ambazo unaweza pata
5. Sehemu ya kuweka duka (Matter of location)
6. Sehemu nzuri ambayo naweza fungasha mzigo kwa bei rahisi sana( iwe nje au hata ndani ya nchi hapa mkoa wowote ule)

Na vitu vingine vingi tu ambavyo watu huwa wanazingatia pindi wanapo amua kuanzisha biashara

NAOMBA MSAADA WAKO KATIKA HILI MWANA JF

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom