Nifundisheni kiswahili tafadhali. Naomba majina ya hivi vitu kwa kiswahili

Samawia

JF-Expert Member
Dec 6, 2017
594
458
1: Kuna kitu Kama mvuke hivi au gesi kinachotoka unapokuwa unamenya chungwa chenza au limao au Hata ukikata kitunguu, kwa Kiswahili kinaitwaje?

2: Naujua upupu ni mmea ambao unawasha sana, lakini kuna majani pia ambayo sio upupu lakini yanawasha ,mfamo miwa mianzi mahindi nk ,je hicho kilichoko kwenye hiyo mimea niliyoita kinaitwaje?

3: Gari inapokuwa imepakia mzigo mzito inatoa sauti ambayo inaashiria kulemewa na huo mzigo, au mtu anapokuwa anasukuma haja ndogo au kubwa Kuna sauti inamtoka kooni, je hicho kitendo kinaitwaje?

4: Mke/mume anamwita mzazi wa mwenzi wake mama/baba mkwe, je baba/mama mkwe atamwitaje mke/mume wa mwanaye?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom