Nifuate utaratibu upi ili kudai damu yangu kutoka kwa mke wa mtu?

Melki the Storyteller

JF-Expert Member
May 3, 2022
5,700
9,778
Napitia kipindi kizito sana ndugu zanguni. Miaka mitano iliyopita nilikutana na binti ambaye niliingia nae kwenye mahusiano ya kimapenzi. Miezi miwili baadae binti alidai kuwa anahitaji kumbukumbu yangu. Hivyo nimpatie japo ujauzito wangu

Kutokana na hali yangu ya kiuchumi niliyokuwa nayo nilimkatalia, lakini aliendelea kulazimisha kwa ahadi ya eti malezi ya mtoto atashughulika nayo yeye mwenyewe. Basi bhana, akina Awa wana nguvu sana, nikajikuta nauza mechi mara kwa mara

Mwisho wa siku binti akapata kibendi. Ujauzito ulipofikia umri wa miezi minne ndipo kuja kugundua kuwa binti kaolewa, tena ni kwa ndoa halali ya kitanzania. Nilimlahum sana na kumkaripia niwezavyo. Binti akafunguka na kusema kuwa mumewe ana tatizo, hawezi kutungisha ujauzito, ingawa ukweni walidhani kuwa yeye ndiye mwenye matatizo, hivyo akaamua kuja kwangu ili a-test kama kweli yeye ndiye mwenye shida au la!

Alidai hawezi kuachana na mumewe kwa kuwa anampenda, akaongezea kwa kusema kuwa akiwa kwa mumewe anapata mahitaji yote anayoyataka. Tukakubaliana iwe siri. Baada ya kujifungua, akawa ananiletea mwanangu kwa siri kisha anamrejesha kwa baba yake wa mchongo. Baada ya miaka mitatu, tukaamua kupanda mbegu nyingine, binti akajifungua. Kwa sasa ninao wawili kwa huyo mwanamke.

Juzi kati tumetoka kuzozana, huyu mwanamke akanikaripia na kukana kuwa hao watoto hawanihusu na si damu yangu. Kwa sasa wana mpango wa kuhama na kwenda mbali na mimi. Naogopa! Nahisi nitawapoteza wanangu. Kwa sasa huyu shetani keshabadili namba ya simu. Msaada niliobaki nao ni wa kupajua kwake tu.

Nifanye nini kuokoa damu yangu? Au niende mahakamani. Naanza kwa kufuata utaratibu upi?

Msaada
 
Napitia kipindi kizito sana ndugu zanguni. Miaka mitano iliyopita nilikutana na binti ambaye niliingia nae kwenye mahusiano ya kimapenzi. Miezi miwili baadae binti alidai kuwa anahitaji kumbukumbu yangu. Hivyo nimpatie japo ujauzito wangu
Andika wosia mapema lkn pia tafuta member mnayeivana hapa JF jenga urafiki naye siku ukivuta atuletee mrejesho wa RIP ili tutoe pole zetu.

Huyo mwanamke atakuondoa haraka sana usichukulie poa tena kaa kwa kutulia
 
Tatizo la watanzania kama ni watoto akili yako inakuambiwa watakuja kukusaidia usiwaache kabisa..

Ukweli mtupu pambania maisha yako huyo mwanamke utamuharibia ndoa yake hamna lingine kama watoto temana nao.
 
Nakupa mbinu ambayo nina uhakika itafanya kazi,

Mpige mkwala huyo Mwanamke kua akileta ujinga utavujisha siri kwa mumewe,hapo atakua mpole tu,ila uwe na uhakika kua hao watoto ni wako.
 
Mimba ya kwanza ulimlaumu huyo binti kua kwanini hakukwambia kua ameolewa? ila ukaja ukampa mimba nyingine tena! Sasa zile lawama zako za mwanzo kwake zilikua na maana gani?

Hii kama sio Chai ya tangawizi basi utakua na matatizo upstairs.
Kwa kuwa nilikuwa tayari nishakosea, nikaona si vyema nikamkatalia kwenye mimba ya pili. Bila hivyo angebeba damu za kila rangi i.e Awe na damu ya Melki, awe na damu ya Juma, awe na damu ya John, awe na damu ya.... Huoni hali hiyo ni hatari kwa afya boss wangu!!!?
 
Tatizo la watanzania kama ni watoto akili yako inakuambiwa watakuja kukusaidia usiwaache kabisa..

Ukweli mtupu pambania maisha yako huyo mwanamke utamuharibia ndoa yake hamna lingine kama watoto temana nao.
Mkuu,huyo Mwanamke hafai kua kwenye hiyo ndoa,ni msaliti wa ndoa yake,huyo ni adui mkubwa kwa mumewe.
 
Kwa kuwa nilikuwa tayari nishakosea, nikaona si vyema nikamkatalia kwenye mimba ya pili. Bila hivyo angebeba damu za kila rangi i.e Awe na damu ya Melki, awe na damu ya Juma, awe na damu ya John, awe na damu ya.... Huoni hali hiyo ni hatari kwa afya boss wangu!!!?
Sasa wewe baada ya kujua kua ni mke wa mtu kwanini hukutemana nae? hata kama angebeba damu za kila rangi,wewe inakuhusu nini?
 
Napitia kipindi kizito sana ndugu zanguni. Miaka mitano iliyopita nilikutana na binti ambaye niliingia nae kwenye mahusiano ya kimapenzi. Miezi miwili baadae binti alidai kuwa anahitaji kumbukumbu yangu. Hivyo nimpatie japo ujauzito wangu

Msaada
Kwani wakilekewa huko unapungukiwa Nini wakisoma vizurii malezi mazurii unapoteza Nini jaribu kutafakarii lakini pia ukimvunjia ndoa yake unafaidika Nini kikubwa tu watoto wasome vizurii wapate maisha mazurii basi hivyoo vingine ni chuki tuu utafurahia huyo binti akiwa single mother watoto wakawa wanateseka tu kisa ulimtoa kwenye ndoa yakee
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom