Nifikishieni Salam kwa KAKA Mkubwa!!

Haya yote 9. Ila Kaka anajua kweli anachokifanya ni shida na mbaya kwa TZ ya sasa? Au ndio bado anawasingizia washauri?
Washauri wako hawamshauri vyema
hawamshauri kupunguza safari za nje ambazo hazina tija
Hawamshauri kuwa uchumi wanaomwambia unapaa kwa kasi ya rocket mwendo wake ni wa konokono na wanamchi hali zao ni mbaya
Yeye mwenyewe hajui ni kwa nini wadogo zake ni maskini ilahali wana kila kitu
hawamshirikishi kumwambia kuw alile kapu linaloingiza misaada limetoboka na kuna watu wanaingiza mikono yao kuiba kila kinachoingia na wanasingizia ni vijicent tuu wala sio nyingi
 
Ukweli hata hicho kisamvu sasa kitakuwa ni anasa kukipata na huo mhogo utatumia pesa za kigeni kuununua
Jiandae kulima utalima wewe ila wengine watavuna na kuja kukuuzia
Sasa utakuwa unashindia majani na maji ya kweney dimbwi
na ndo hivyo hata yule kijana wako ambaye anafanya kazi kwenye NGO's moja mjini ameambiwa mafao yake atayapata baada ya kufikisha miaka 55 sijui bado kama wewe mzazi wake utaendelea kuishi ili uje uyafaidi
Kama ulitegemea ayachukue mafao yake aje akujengee kakibanda sahau kabisa ndo imetoka utaishi kwenye banda lako la udongo na kuenzekwa kwa nyasi maisha yako yote
 
bado unamatumaini na huyo kaka yako mkuuu!??
achana naye jifanye kama ni marehemu!
samahani gfsonwin unaona huu ya mkuu Henge hapa ni moja ya kile nilichokuambia sometimes kinaheal siunaona hii huku jukwaa la siasa tena japo nafikiri nimekuingiza kule ubungo nyuma garage kule ila angalia tu hii
 
Last edited by a moderator:
huyu kaka yako angekuwa anatoka ukoo mmoja na mimi tungekuwa tushakaa kikao cha pamoja ili kumtenga maana hatufai, ila kwa kuwa umetujulisha unayodhani kuwa ni mazuri lakini kwetu sie majirani tunaona ni ya hovyo, basi tutakusaidia ifikapo 2015 kaka yako na ndugu zake tutakuwa tumewafukuza wote hapa mtaani kwetu
 
huyu kaka yako angekuwa anatoka ukoo mmoja na mimi tungekuwa tushakaa kikao cha pamoja ili kumtenga maana hatufai, ila kwa kuwa umetujulisha unayodhani kuwa ni mazuri lakini kwetu sie majirani tunaona ni ya hovyo, basi tutakusaidia ifikapo 2015 kaka yako na ndugu zake tutakuwa tumewafukuza wote hapa mtaani kwetu

Kaka bado anamdanganya bibi. Akija kututembelea anampa PIPI ya kijiti (Miradi ya Maji). Akileta chakula anasema amepata tabu kweli kukitafuta wakati baba ameshakufa na alishasema kuwa yeye kaka ndio kichwa cha familia (Wajibnu wa Serikali).
 
jiunge katika vikundi au SACCOS ili ujumuike na wenzako muweze kupata mikopo ujiletee maendeleo.


hii tabia ya kulalamika na kuishia kulaumu haitusaidii kama taifa.

Tamuchungu!
Kweli wewe ni Juha Kama Jakaya Mrisho Kikwete! Sasa Kama mishahara ni kidogo ukijiunga Saccos hiyo michango na marejesho utalipa kwa kutumia Masburi au Cameroon?

The problem is huo mshahara ambao ndilo pato halali hautoshi kulipa your basic needs like kodi ya Nyumba , chakula, umeme na hata maji then how do you go about it?

Upumbavu wa CCm unawashauri watu wa kawaida waende kuokopa but VAT unawakata 18% bado RIBA ambayo in the most attractive Saccos could be a minimum of 15% sasa Watz unakopa 100 halafu 33% unachia watu how would you manage to pay back and come up alive . Hii misemo ndiyo inazalisha rushwa in and out and when added with Grand corruption the pill becomes more bitter . Kwa hiyo wewe chizi Tamuchungu and people of your thinking should go to hell very fast?...? When we change sides itakuwa chungu kweli kweli.
Kwa Watz wote let us draw a line on the sand and stand to it! Mpaka kieleweke CCM has to go and it's henchmen dead or alive?? Tell your KAKA mkubwa redemption is coming soon and they have nowhere to hide hata kwa hao EU and the Americans ???
 
Kaka, Ulisema hari mpya nguvu mpya na kasi mpya kaka, kwetu ni bala kasi yako hatuiwezi. Kaka kasi yako ni kali mno nadhani zaidi ya speed 220Km/H.
Kaka ulisema hali ya maisha itakuwa good kwa vijana na ile ahadi ya ajira 1m kwa mwaka. Hilo ni balaa yaani umetugeuka hata hizi ajira 40 kwa mwaka nazo unakaba? Kaka kufika 55yrs ni balaa. Sheria ndio inataka hivyo ila kwanini msituandae na kutushirikisha wafanyakazi wenyewe? Kwani zile hela zenu kaka?
Kaka hivi ni kweli huijui Richmond mbona we ndo kila kitu hapa bongo. Ukiamua hata mimi nisiende toilet kweli naweza nisiende ndani ya mins tu. Tuambie basi wale ni kina nani vile?
Vipi kuhusu wale mafisadi na siku 90 mulizowapa? Wadogo zenu tunasubiria kuona action mpaka leo picha halinogi. Hafi Jambazi kuu wala steringi picha la kihindi afadhali. Kule migodini mbona hali ni Mbaya sana wakati kila siku ndege zinakwenda south direct kutoka migodini. Kusoma sijui kabisa ila pale nadhani picha naiona kwani mungu kanijaalia macho.
Ile mikataba ya gesi mbona tunaisikia juu juu tu. Sio Richmond nyingine kweli? Mbona hatuwekani wazi jamani wakati sisi ndugu mmoja?
Kaka watu wanapiga si mchezo. Eti wanasema we dhaifu hata ukigundua utawachekea na kuwahamisha vituo. Huku TRA ni balaa hela mbele rushwa kama kanuni. Kule THA ndio kabisa, tunauza magari yetu pale pale port. Halmashauri ndio kabisa hata mawizarani ndio usiseme.
Nadhani yapo mengi ila kaka BIBI yangu na Shangazi hapa kwetu Pangani wanashukuru mungu kwa kuwapatia mti wa mhogo kuliko WEWE kaka. Yaani asubuhi uji wa muhogo na muhogo, saa kumi na mbili ni ugali wa muhogo na kisamvu cha chumvi hio ndio mpaka kesho tena. Msaidie basi kidogo japo ale maharage? Ila bibi anakumbuka kuwa alikupa KURA yake na sasa analaani kwani hata kwenda mjini hawezi tena nauli hana. Sio kama anafanya kazi hapana ila ungempatia ile VOUCHER ya mbolea akalima kidogo ingemsaidia. Sasa zile voucher washkaji zako wamepiga na msemo wao kuwa huwezi kuwafanya lolote wewe ni DHAIFU…

My Take:-Najua hupitagi hapa JF ila najua wewe rafiki yake unaesoma hii kitu utamwelekeza japo kidogo aachie maana tait mno.

Duh!!! hapo kwenye bold nimecheka sana sio kwa kufurahi... ni kicheko cha kusikitika...
Inasikitisha sana lakini kwa jinsi navyomuona rais huyu hasikii wala haoni... Sijawahi kuona uongozi wa juu mbovu kama wa kipindi hiki... !! huko TRA kwa sasa ulaji njenje.. yaani kila mtu anachota kwa nafasi yake...... Mipango yao usiku na mchana ni jinsi ya kupambana na CHADEMA!!!!!!! nothing more!!!!!!!!!!!
 
Vuta tu muda October 2015 sio mbali, si unaona vikao vinaendelea, mwambie bibi avumilie pia, hatapata tena pipi ila atapata kiwanda cha pipi

Kaka bado anamdanganya bibi. Akija kututembelea anampa PIPI ya kijiti (Miradi ya Maji). Akileta chakula anasema amepata tabu kweli kukitafuta wakati baba ameshakufa na alishasema kuwa yeye kaka ndio kichwa cha familia (Wajibnu wa Serikali).
 
Vuta tu muda October 2015 sio mbali, si unaona vikao vinaendelea, mwambie bibi avumilie pia, hatapata tena pipi ila atapata kiwanda cha pipi


Bibi haelewi kashachoka (Mtz) alichokosea kaka alimletea TV mapema so analiona BUNGE Live. Anasikitika pia hajui maana ya DIGITAL kwani mwezi wa kumi na mbili atakuwa haoni tena FTA Channels.
 
Bibi haelewi kashachoka (Mtz) alichokosea kaka alimletea TV mapema so analiona BUNGE Live. Anasikitika pia hajui maana ya DIGITAL kwani mwezi wa kumi na mbili atakuwa haoni tena FTA Channels.
Bibi si wa miaka hii, ametoka mbali, amekwepa mishale mingi (uonevu na dhuruma) hadi sasa, basi avumilie kidg tu, mwanga ninauona, akikata tamaa yeye hata hapo 2015 sie tutaumia zaidi
 
Bibi si wa miaka hii, ametoka mbali, amekwepa mishale mingi (uonevu na dhuruma) hadi sasa, basi avumilie kidg tu, mwanga ninauona, akikata tamaa yeye hata hapo 2015 sie tutaumia zaidi

Nitamweleza bibi. Ila watamficha mengi kwani hajui lini atakuwa na king'amuzi baada ya sa 6 na DK 1 ya tarehe 31 Dec 2012.
 
  • Thanks
Reactions: bdo
Nitamweleza bibi. Ila watamficha mengi kwani hajui lini atakuwa na king'amuzi baada ya sa 6 na DK 1 ya tarehe 31 Dec 2012.

Kwa hilo hata mimi nina mashaka, maana tulishaachana na habari za kusikiliza redio kwa mwenyekiti wa kijiji/kata, sasa nipo pamoja na bibi kuwa na mashaka, naamini aliruka mishale mingi ila najua kwa hili hawezi kurudi nyuma tena na kuanza upya kwa kukumbuka enzi
 
JK: Tumegundua mtandao wa kuuza binadamu


na Christopher Nyenyembe, Mbeya

amka2.gif
RAIS Jakaya Kikwete amesema kuwa Tanzania kwa kushirikiana na nchi nyingine zimefanikiwa kugundua mtandao wa biashara haramu ya binadamu wanaosafirishwa kupitia mpaka wa Malawi kwenda nchi za Ulaya na kuuzwa kwa lengo la kupatiwa uraia na kazi.

Kikwete amedai kuwa kundi linalofanya biashara haramu ya binadamu limejikita kila nchi ambako huwapokea wananchi wa Ethiopia na Sudan Kusini na kuwapitisha kwenye njia za panya hadi Malawi.

Rais Kikwete alisema hayo juzi jioni Ikulu ndogo mjini hapa, alipokuwa akijibu baadhi ya maeneo ya taarifa ya mkoa huo iliyowasilishwa na Mkuu wa Mkoa, Abbas Kandoro ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ikihusu kuongezeka kwa kundi la wahamiaji haramu wanaopita katika mkoa huo kila wakati na kunaswa.

Kandoro alisema tatizo hilo linazidi kukua siku hadi siku huku kukiwa na idadi kubwa ya wahamiaji haramu kutoka Ethiopia wanaonaswa mara kwa mara na idara ya uhamiaji wakisafirishwa ndani ya malori na kuvushwa kwenye mpaka wa Kasumulu kuelekea nchi jirani ya Malawi ambako huko nako upo mtandao unaowapokea.

Akiizungumzia hali hiyo kwa kina, Kikwete alisema kuwa mtandao huo si kwamba ni wa wahamiaji haramu tu isipokuwa umegundulika kuwa unafanya bishara haramu ya binadamu, na kwamba kila anayefanikiwa kumvusha mtu mmoja hulipwa kati ya dola 10 na kuendelea.

“Hii biashara si ndogo kama mnavyofikiri; inawahusu watu wazito na wenye fedha ambao wakifanikiwa kuwafikisha watu huko Marekani, wanapatiwa uraia wa kuishi na kutafutiwa kazi za kufanya.

“Tulipowahoji tuliowakamata Dodoma wanasema hapa Tanzania wanapita tu na sisi hatuwezi kuruhusu wapite, tukiruhusu tutakuwa tunapingana na mkataba wa Umoja wa Mataifa wa kupiga vita biashara haramu ya binadamu,” alisema Rais Kikwete.

Hata hivyo alisema kuwa idara ya usalama inafanya kazi kubwa ili kubaini mianya inayotumiwa na wafanyakazi wasiokuwa waaminifu walioko mipakani ambao nao kwa namna moja au nyingine wanajihusisha na usafirishaji huo.

“Hivi ninapoongea na ninyi wengine wako hapa hapa wananisikiliza,wanapuuza ninachokisema kwa kuwa nao ni miongoni mwa watu wanaofanya biashara hiyo haramu.

“Hili tunalifanyia kazi na kama mna habari tumefanikiwa kumkamata mtu mmoja anayefanya biashara hiyo hali iliyotusaidia kutambua kwa undani mtandao mzima,” alisema Kikwete.

Hata hivyo, Kikwete aliwaomba wananchi mipakani wasaidie kuwafichua watu wanaofanya biashara hizo na kuacha kuwapokea na kuwahifadhi watu wasiowajua majumbani mwao ili waweze kupata chochote kwa kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha sheria za nchi.

Alisema kuwa umaskini kwa kiasi kikubwa unawafanya watu wafikie mahali pa kuuzana ili tu mtu apate dola 10 kwa siku na kusisitiza kuwa wale watakaobainika wakijihusisha na biashara haramu za binadamu wenzao watakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria ili Tanzania isiwe nchi inayolaumiwa kwa kosa hilo.

Aliiagiza Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huo chini ya Mwenyekiti wake, Kandoro, kuhakikisha kuwa inafanya kazi ya ziada ili kukomesha biashara hiyo hasa katika mipaka ya Kasumulu na Tunduma na kwamba serikali imechukua hatua ya kuondoa vizuizi vya barabarani kwa kuwa vilikuwa vikiwanufaisha zaidi watumishi wa umma waliopewa kazi hiyo na kushauri mbinu zaidi za kiintelijensia zitumike.

Chanzo: JK: Tumegundua mtandao wa kuuza binadamu

My take:
Inawezekanaje Rais wa nchi anatamka wazi kuwa hapo alipo wapo wahalifu wanamsikiliza na kupuuza juu ya uhalifu anaozungumzia na wahalifu hao wanaachwa bila kuchukuliwa hatua yoyote. Mkuu wa nchi anapoongea maneno kama hayo anataka asaidiwe vipi ama anatoa ujumbe gani kwa wananchi ilhal vyombo vyote vya dola viko chini yake?. Kweli Tanzania tumekwisha labda ashuke malaika kuikoa nchi yetu!!

Si alishaambiwa kuwa Mkuu wa kituo kule kigamboni anafahamu vya kutosha kuhusu hiyo Biashara si angemkamata tu fasta huu ni udhaifu mwingine... Kuna uzi humu ulisharushwa kuhusu wanaofanya biashara ya kuvusha watu huwa wanaingia kupitia kigamboni na polisi huwasindikiza na kuwaacha waendelee na safari zao... hili la waliokufa ndio wanajifanya kuwa watakuwa makini lol
 
Si alishaambiwa kuwa Mkuu wa kituo kule kigamboni anafahamu vya kutosha kuhusu hiyo Biashara si angemkamata tu fasta huu ni udhaifu mwingine... Kuna uzi humu ulisharushwa kuhusu wanaofanya biashara ya kuvusha watu huwa wanaingia kupitia kigamboni na polisi huwasindikiza na kuwaacha waendelee na safari zao... hili la waliokufa ndio wanajifanya kuwa watakuwa makini lol


Wanasema KAKA Mkubwa ni dhaifu bora mdogo wake aliefukuzwa nyumbani kufuta aibu ya kaka kumwozesha dada kinyemela.. nadhani umenipata.
 
Kaka yako kaziba masikio huku akidanganya watu yeye ni msikivu. Kaka yako analeta dhuluma za waziwazi sasa TRA na Fore , NSSF du. Omba kuvunja undugu tu huna kaka.
 
Back
Top Bottom