Nifate utaratibu upi ili niweze kutambuliwa kwa level yangu ya elimu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nifate utaratibu upi ili niweze kutambuliwa kwa level yangu ya elimu

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by fimbombaya, Dec 3, 2011.

 1. f

  fimbombaya Member

  #1
  Dec 3, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 47
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Naomba ushauri na muongozo katk hili. Mimi niliajiriwa km mwl. Wa shule ya msingi(gvt) na kuamua kujiendeleza hadi kufanikiwa kumaliza shahada ya uhasibu mwaka 2011,lkn ktk kipindi chote hicho muajiri wangu alikuwa hajui km nasomea fani tofauti na ualimu,na sabubu ya kumdanganya kuwa nasoma ualimu ilikuwa nikupata ruhusa ya kwenda kusoma kwan ilikuwa akikataa kuwaruhusu watu waliokuwa wanaenda somea kozi tofauti hasa walimu.sasa nimemaliza na ninahitaji mawazo yenu namna ya kufanya na kwautaratibu upi ntambulike na kutumikia ujuz wangu mpya pa1 na kupandishwa mshahara kwa elimu yangu.? Nisaidie muongozo pliz
   
 2. M

  Matungwa Member

  #2
  Dec 4, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu fimbombaya,
  Kwanza kabisa, nafikiri ulifanya makosa kumdanganya muajiri wako kwamba ulikuwa unasomea ualimu wakati ulikuwa unasomea kitu kingine tofauti. Sifahamu vizuri taratibu za serikali kuhusu watu waliosomea kozi tofauti na kazi zao lakin inawezekana muajiri wako alijua kuwa umemdanganya kwahiyo anasubiri useme ili achukue hatua za kinidhamu. Kama umepata shahada ya biashara, nafikiri kuna milango mingi itafunguka hasa katika sekta binafsi. Hata hivyo, bado kuondoka kwako kutaacha pengo kubwa ikizingatiwa kuwa nchi yetu ina uhaba mkubwa wa walimu.
   
 3. shizukan

  shizukan JF-Expert Member

  #3
  Dec 4, 2011
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 1,158
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Usijione kuwa umefanya dhambi kuuubwa kwa kusoma. Ilikuwa makosa kudanganya lkn sioni dhambi ya mtu kubadili fani. Kwa mfn: Wengi wa mawaziri na wabunge wetu wamenawa taaluma zao na kukimbilia kwenye siasa. Ndani yao wapo kina Lukuvi (walimu), Nkamia (habari), Mwakyusa (daktari) na wengineo wengi.

  Mimi nataka nikupongeze kwa kusoma ktk mazingira magumu ya kujificha, na nikukumbushe kuwa maisha hayako hapo ulipo tu. The so called UZALENDO hauwi implemented na wananchi tu huku viongozi wanaamini 'survival of the fittest'. Do the same, your first responsibility is your family, Tanzania comes next.
   
 4. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #4
  Dec 4, 2011
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,692
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 180
  Kama 'shahada ya uhasibu' uliyopata ni CPA wewe ni hot cake. Soma magazeti kuna matangazo chungu mzima ya kazi za uhasibu serikalini na kwenye sekta binafsi. Ukishapata kazi serikalini unaweza kuanza taratibu za kuhamisha ajira yako kwa mwajiri (lakini katika serikali hiyo hiyo). Kunaweza kuwepo mizengwe lakini inawezekana. Kama ni kwenye sekta binafsi utkachopoteza ni hako kapensheni kako serikalini. Lakini hilo linategemea wewe una umri gani. Kama bado kijana unaanza upya. Pensheni yako unaweza kuijenga wewe mwenyewe.
   
Loading...