Nifanyeje na yeye ameshaujua udhaifu wangu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nifanyeje na yeye ameshaujua udhaifu wangu

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Hashpower7113, Oct 30, 2012.

 1. Hashpower7113

  Hashpower7113 JF-Expert Member

  #1
  Oct 30, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 452
  Likes Received: 387
  Trophy Points: 80
  Jamani naomba mnishauri me ninampenz wangu na nampenda sana mpaka mwenyew anajua sasa amekuwa mtu wa kunifanyia visa kibao haswa pale alipogundua nampenda, anakunywa pombe sana na akilewa huwa mkorofi ananitukana matusi ya nguoni kama **** la mama angu, ****** malaya wa kisukuma, maana me kabila langu ni msukuma, kwa ufupi nampenda but matendo yake yamenichosha na kila nikijitahid kumuacha nashindwa wakati mwingine ninaamua hivyo but nikikumbuka mapenzi yake nashindwa na kujikuta naanza mwenyewe kumpigia simu or kumtumia sms kama za kumtania kama vile mimi ndio mwenye makosa wakati inatakiwa yeye ndio aniombe msamaha, na kibaya zaidi hata anaponikosea huwa hawezi kunipigia simu eti mpaka mimi nimuanze na nikimpigia simu hapokei au ananikatia kabisa basi mimi ntaendelea kumbembeleza mpaka atakapoamua kuzungumza na me na kunisamehe nisaidieni jamani nitumie njia gani niweze kumsahau na kuachana nae? Na je huyu ananipenda kweli?

  Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
   
 2. Mgibeon

  Mgibeon JF-Expert Member

  #2
  Oct 30, 2012
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 7,441
  Likes Received: 9,088
  Trophy Points: 280
  Hakuna mapenzi hapo...!!! Trust me huyo mtu ana mpenzi mwengine ambae anampenda na kumnyenyekea! Najua inakua ngumu kupokea ukweli kwakua unauma! Ila huo ndo ukweli wenyewe! Hata mkiwa ktk ndoa utajikuta mtumwa wa mapenzi... BORA KUUMIA SANA MARA MOJA KULIKO KUUMIA KIDOGOKIDOGO Sikuzote za Maisha yako duniani
   
 3. Nicole

  Nicole JF-Expert Member

  #3
  Oct 30, 2012
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 4,284
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  salute kwako mkuu!
   
 4. kbm

  kbm JF-Expert Member

  #4
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 5, 2012
  Messages: 4,964
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Dada yangu pole. Kama hamjafunga ndoa au kuwa na watoto, vunga vioo, huyo hakupendi. Katulize akili kwanza.
   
 5. Mgibeon

  Mgibeon JF-Expert Member

  #5
  Oct 30, 2012
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 7,441
  Likes Received: 9,088
  Trophy Points: 280
  Ikurudie na wewe pia mkuu..!
   
 6. m

  mbalapala Member

  #6
  Oct 30, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 53
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 15
  Jamani! Kweli mapenzi ni upofu lkn kwa hapo shosti unapotea.Lkn huwa kuna kajimsemo eti ukiona umependwa jua kuna **** katendwa and vice versa.Hivi kina mahaba niue bado mpo mpaka karne hii??
   
 7. elmagnifico

  elmagnifico JF-Expert Member

  #7
  Oct 30, 2012
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 7,913
  Likes Received: 7,455
  Trophy Points: 280
  Kitendo cha kujua we dhaifu kwake basi we si dhaifu tena. Kilichobaki ni kupiga moyo konde maumivu uyashinde na umfungie vioo mazima ndipo atajua na ataimba I want it all back kama chris brown
   
 8. Fixed Point

  Fixed Point JF Bronze Member

  #8
  Oct 30, 2012
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 11,321
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Kuna kakangu aliwahi kuniambia mtu akikuambia jambo serious akiwa amelewa ujue alikusudia kukuambia ila alikuwa Anaona noma......... Hayo matusi na vurugu anavificha tu kwenye pombe, ndo alivyo.........
  mbona kuna uwezekano wa kulewa na kukimbilia kitandani kwa Amani?
  kama unataka kumpenda, regardless, endelea.......lakini ujue hakuna kitakachombadilisha
   
 9. Hashpower7113

  Hashpower7113 JF-Expert Member

  #9
  Oct 30, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 452
  Likes Received: 387
  Trophy Points: 80
  Inawezekana unachosema ni kweli, maana hata ikitokea siku nikaamua kumshtaki kwa watu wake wa karibu ambao yeye huwa anawaheshimu basi matokeo yake nitaambulia kipigo, nateseka mwenzenu na kinachoendelea kuniuma nimejitolea sana katika maisha yake tofauti na nilivyomkuta, maana nilimkuta wanawake aliokuwa anaishi nao walikuwa wamemfilisi na kumfanya aonekane kama kibabu kizee but me nilimbadilisha sana kuanzia ndani kwake mpaka mwilini kwake, alikuwa anafanya kazi nzur na mshahara wake mzur sema hakuwa na mtu wa kumsaidia jinsi gani ya kupangilia mpangilio wa matumiz ya pesa akawa anavaa vizur analala pazuri na wafanyakaz wenzie wakaanza kumsifia na kumwambia kwamba uliompata usimuache na wengine wakathubutu kuniambia hadi mimi mwenyewe kwamba nisimuache ndugu yao na niendelee kumtunza, jaman mpaka naamua kuilete hii mada humu kiukweli naumia na inaniuma sana nimekosa nini mpaka nastahili malipo haya ya aibu na fedhea

  Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
   
 10. BRO LEE

  BRO LEE JF-Expert Member

  #10
  Oct 30, 2012
  Joined: Dec 25, 2011
  Messages: 580
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  Nilipokuwa nasikiliza wimbo wa TEJA WA MAPENZI wa Lady JD niliona ni jambo la kufikirika 2, kumbe wapo!!...

  Dada, hakuna wa kukupa njia ya kujitoa katika huo utumwa wa mapenzi ni wewe mwenyewe kusema imetosha.
  Unafahamu madhara ya kumng'ang'ania asiye kupenda? usiombe yakukute.

  'Mwenzio alisema bora arudi kwao kijijini akaendelee kuchoma mkaa, maisha hayawezi bara arudie yake enzi....'we unasubiri kupewa njia wakati ndo unateseka?.
   
 11. Hoshea

  Hoshea JF-Expert Member

  #11
  Oct 31, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 3,837
  Likes Received: 1,541
  Trophy Points: 280
  pole sana nmekuonea huruma, huyo hakupendi bana wachana nae tu, jisogeze pembeni panga maisha bila yeye, shit happens. Kama ulimtenda vema hivyo atakutafuta tu nawe usije mkubalia, anza kuwaza life bila yeye then take actions next week, amua tu mwenyewe hutoshindwa, ukitaka company tupo wala usiwaze.
   
 12. kibol

  kibol JF-Expert Member

  #12
  Oct 31, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 3,135
  Likes Received: 378
  Trophy Points: 180
  either to love too much or to hate too much is blindness,inavyoonekana kama jamaa hajali hisia zako vile na anafanya hivyo kwasababu anajua huna pa kwenda,unampenda sana,huwezi kumuacha nk.ushauri wangu tafuta siku mtoe out umueleze vile unavyojisikia kutokana na yale anayoyafanya,mueleze na wewe una moyo wa nyama unaoumia pia,ikishindikana jaribu kuwashirikisha rafiki zake wa karibu sana au ndugu/wazazi wake,ikishindikana kubadilika hapo huyo si wa kwako inabidi uachane nae though utaumia mwanzoni but you shall be healed by the passage of time.
   
 13. Mbimbinho

  Mbimbinho JF-Expert Member

  #13
  Oct 31, 2012
  Joined: Aug 1, 2009
  Messages: 6,027
  Likes Received: 2,866
  Trophy Points: 280
  Pole mwayego. Imeshanitokea pia, kila kosa unajipa wewe ili tu kumfanya asikasirike.
  But one thing you should know, once u decide to let him GO, he'll GO for real and he wont be taunting you anymore.
   
 14. Bitabo

  Bitabo JF-Expert Member

  #14
  Oct 31, 2012
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 1,896
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Hakupendi anasingizia pombe fanya mamuzi magumu utaumia kwa mda tu then utasahau maisha yataendelea na utapa mwingine kupenda si dhambi bt unampendaje asopendeka livue penzi bana sepa atakumiza huyo utakoma mtose mapenzi hayana shule bana utampata anaeyajua zaidi yake usiwe mjinga we wa,wapi.

  Nayanda.
   
 15. bhikola

  bhikola JF-Expert Member

  #15
  Oct 31, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 457
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 45
  pole sana binti wa kisukuma, "kinehe mayo", usilete uvumilivu wa kisukuma kwenye mapenzi, maana hapo bado mko wapenzi je itokee muishi wote c ndo hapatatosha?!!!
  kimsingi hakuna mtu ambaye atakupenda halafu aku-abuse haiwezekani kamwe katika mapenzi, trust me! hasa mwanaume kumpiga kwa mfano mpenzi wake daaaaaaaaaaah, wanigeria ndo wanaposema "its an abomination", so kama anaweza kuwa na huo ujasiri, uwe na uhakika hata kwenye mambo yetu we unabakwa tu maana siamini kama huwa mnakubaliana au ku-compromise, atakuwa akifika akataka mechi ni lazima apige, so what love is that?!
  ni kweli, bora shetani unayemjua kuliko malaika usiyemjua, lakini pia lazima utambue kuwa thamani ya kitu huonekana baada ya kukipoteza, we mmwage jamaa ndo utagundua kuwa ulikuwa wa muhimu sna kwake, na atarudi akikusihi, zaidi ya hapo jiandae kuumizwa (broken hearted)
   
 16. mathcom

  mathcom JF-Expert Member

  #16
  Oct 31, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 1,402
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Usikate tamaa unaonekana wewe ni mwanamke mwema na mwenye muelekeo kwenye maisha! achana na huyo jamaa
  tulia utafute mwengine atakae kuliwaza na mkafarijiana! wengi walipitia huko2 kwenye shida hatimae wakapata wenye
  upendo wa kweli.

  Kila la kheri ...
   
 17. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #17
  Oct 31, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  dah, hata kama ni 'ndoho tabu', hebu gangamala kidogo.

  Mtu akithubutu kumtukana mzazi wako, amebakiza nini sasa?

  Huna lako hapo
   
 18. mathcom

  mathcom JF-Expert Member

  #18
  Oct 31, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 1,402
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Pamoja na yote hayo mimi si amini kwamba mwanaume ukimpenda sana ndio anakufanyia visa! hii ni dhana mbaya
  kwa akina dada. ukitaka kujua mwanamme kama nakupenda sana basi mpende sana ukiona anakufanyia visa basi
  huyo hakupendi tafuta mwengine.
  Ila anaekupenda basi hana atakacho fanya zaidi ya kukuzidishia mapenzi na kukupeti2

  Wadada msiwe waoga na wanaume onyesheni mlionayo moyoni, muangalie mwenendo wa wapenzi wenu.
   
 19. Mgibeon

  Mgibeon JF-Expert Member

  #19
  Oct 31, 2012
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 7,441
  Likes Received: 9,088
  Trophy Points: 280
  Dah, pole sana! Acha nikwambie jambo fulani, binadamu ni wasahaulifu sana! Huyo mpenzi wako keshayasahau yote na ulimpotoa! Hakuna kitu kibaya kama furaha yako ishikiliwe na mtu hasa asiyejali hisia zako, pole sana kwa kupoteza muda, nguvu najua na pesa included..! Binafsi naamini japo pekee lisilowezekana ktk ulimwengu huu ni kurudisha uhai wa binadamu ambae amekufa, mengine yote including kutoka katika kifungo cha minyonyoro ya penzi la upande mmoja INAWEZEKANA..! Piga moyo konde.. Funika kombe mwanaharamu apite! Kwanini binadamu mwenzio akunyanyase?? Kwanini ukose furaha na amani maishani mwako kwaajili ya mtu asie na huruma hata kidogo! Let him go., atapita and U will get someone who deceives you! Muombe Mungu akupe ujasiri wa kufanya maamuzi magumu! FURAHA ni kitu nyeti kuliko hata nyeti tulizonazo! Fanya maamuzi, then jipe muda then tathimini matokeo yake, .Kila la kheri mdada
   
 20. georgeallen

  georgeallen JF-Expert Member

  #20
  Oct 31, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 3,758
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  limbwata kazini. Au unashindwa kumuacha kwa sababu ya weupe wake? Wasukuma mna mambo, mbona wanawake weupe wapo wengi tu.
   
Loading...