Nifanyeje kuondoa adha ya kukabwa na wachawi?

Korozoni

JF-Expert Member
Oct 24, 2016
264
105
Habari za muda huu wanajukwaa,

Kama kichwa kinavyojieleza,nimekuwa nikikabiliwa na tatizo la kukabwa na wachawi karibu kila usiku kwa wiki mbili sasa,na hali hiyo hutokea mara mbili au zaidi kwa usiku mmoja.

Naomba mawazo yenu nifanyeje kuwazuia hawa wanga?kila siku naamka nimechoka sana akili!

Lengo la mchawi kuendesha ukabaji ni lipi hasa?
Wataalam wa uchawi na uganga nasubiri mchango wenu.
Nawasilisha!
 
Habari za muda huu wanajukwaa,

Kama kichwa kinavyojieleza,nimekuwa nikikabiliwa na tatizo la kukabwa na wachawi karibu kila usiku kwa wiki mbili sasa,na hali hiyo hutokea mara mbili au zaidi kwa usiku mmoja.

Naomba mawazo yenu nifanyeje kuwazuia hawa wanga?kila siku naamka nimechoka sana akili!

Lengo la mchawi kuendesha ukabaji ni lipi hasa?
Wataalam wa uchawi na uganga nasubiri mchango wenu.
Nawasilisha!

Uwe unakula nyama ya nguruwe mara kwa kwa mara.Majini na wachawi na nguruwe ni vitu viwili tofauti.Ukila unakuwa na harufu ya nguruwe hawasogei
 
ndugu yangu mpe yesu maisha yako yeye ndio ngome na ulinzi wetu,mimi kabla sijaokoka nilikuwa nakabwa, naota ndoto niko makaburin, naota nakimbizwa na watu,nafanya mapenz na watu nisiowajua Lakin baada kukiri yesu ndio mwokozi wa maisha yangu na Kuacha dhambi nalala vizur sana Kwa sababu huwa naomba na ku so ma biblia kabla ya kulala na ninapoamka.ndugu yangu mungu ni mwaminifu ukizitubu dhambi zako yeye anasamehe na anasema hatazikumbuka, Fungua moyo wako aingie hautojuta kamwe atakufanya huru na kukutoa gizan na kukufungua vifungo vyote vya shetan, wachawi na mamlaka zote za giza.NEEMA YA KRISTO iwe juu yako mtumishi ubarikiwe
 
Wataaelam wa uchawi na uganga nasubili mchango wenu. Samahani mm sijui uchawi wala uganga ila nina jibu la tatizo lako. Sisi wanadam tuliumbwa na kupewa uwezo wa kuishi pande mbili (Ulimwengu wa Mwili na Ulimwengu wa Roho) ingawa maisha yetu yanategemea sana Ulimwengu wa mwili, sasa kuna binadana wachache wanao lijua hilo nao na kutafuta msaada kutoka Falme 2 kati ya Ufalme wa Mwenyez Mungu muumba wa kila kitu na Ufalme wa shetani. Hizi ni mamlaka mbili pekee zinazo tawala dunia na zenye uwezo na mamlaka ya kumuwezesha mwanadam aweze kuishi katika ulimwenyu wa Roho na ulimwengu wa Mwili. Wachawi wamepata uwezo wa kukukaba wewe usiku kutoka kwa Shetani kwa hiyo ukitaka kupona inabidi na wewe uchague upande mojawapo wa utawala utakao kupa ulinzi ukichagua upande wa giza ujue kesho na wewe utaanza kutupa kelo ya kutukaba wenzio usiku kwa ushauli wangu nakuomba umchague Mungu muumba wako fuata na shika Amri zake. Wachawi kwako itakuwa istoria pia kupitia wewe hata nduguzako watapona kwani utawala wa Yesu ndio utawala wenye nguvu kupita tawala zote hapa ulimwenguni Ole Ole wako ukijidanganya kutumia ndumba ukizani kuna msaada utakuwa umebugi ndugu hao wote bosi wao mmoja wote wamepewa kaz ya kukualibia tu
 
Ndugu ktk Bwana.

Napenda nikupe dondoo ya jinsi ya kuondoka na tatizo hili ingawa naweza kutofautiana na wengine.

Umesema tatizo unalo kwa wiki mbili sasa.

Tatizo ulilinalo laweza kuwa linatokana na mfumo wa uvutaji hewa sio Nzuri au una ugonjwa wa wasiwasi. Ni kawaida Ubongo ukikosa oxygen utapata maruweruwe, kukabwa, na mambo yanayojulika kama uchawi. Na tatizo hili LA Ubongo kukosa hew inategemea na unavyolala. Nakushauri ulala kwa ubavu na hasa ubavu wa kushoto na si vinginevyo. Kama unatumia feni inayokuface mojakwa moja usoni jaribu kuigeuza ieekee ukutani au dirishani. N ikitokea umekabwa na ukaweza kujinasua unashauriwa ukae kitako kwa DKK kadhaa, ikiwezkana kunywa maji au hata kusoma andiko. Hii itakuwezesa kuridisha oxygen kwenye ubongo. Suala LA wasiwasi linatokana na style yetu ya maisha au urithi. Kama kuna ktk nduguzo yupo mwenye ugonjwa wa akili nakushauri ukafanye checking na update ushauri kwa wataalamu ya akili. Ni hayo kwa sasa uiiweza kufafanua hayo naweka kupata picha halisi na kushauri
 
MKUU NAKUPA JANJA ....KUANZIA LEO LALA TAA ZOTE ZA NYUMBA ZINAWAKA NA KAMA UMEPANGA HAKIKISHA TAA YAKO YA NDANI HAIZIMWI ....WACHAWI WANAOGOPA MWANGA NDO MAANA HAWALOG MCHANA ..HII NISABABU KWWNYE MWANGA ANAWEZA AKAWA HAONEKANI LAKINI "" KIVULI CHAKE ATA AFANYEJE KINAONEKANA "" KWA IYO WANAOGOPA KUKAMATWA .....SO ANAWEZA KUJA AKAISHIA NJE TUUU AU AKAISHIA KISEHEMU CHENYE GIZA ........Mfano mzuri nikwamba ukiwa kijijin unaweza ukashangaa chemli inazima usiku nawakat mafuta yamejaa nakila ukijaribu kuiwasha kidogo inazima .....LAKINI MCHAWI HANA NGUVU YA KUZIMA TAA ZA UMEME ......SO FANYA IVO ......HUU NI UTAALAM WA MISIRI .
 
bas
Uwe unakula nyama ya nguruwe mara kwa kwa mara.Majini na wachawi na nguruwe ni vitu viwili tofauti.Ukila unakuwa na harufu ya nguruwe hawasogei
i na mie ni jini hahahaha nikisikia nyama ya nguruwe inanuka naweweseka mbaya
 
Back
Top Bottom