Nifanyeje kabla ya kulala ili nikiota ndoto usiku wa manane niwe nusu nimelala nusu niko macho?

kufanakupona

JF-Expert Member
Jun 18, 2015
522
417
Utakuta unaota unaambiwa jambo la maana na mtu unayemfahamu au usiyemfahamu, kabla hajamaliza kukusimulia, mara anatoweka au ndoto inakatika. Pengine ungekuwa nusu macho, hii ndoto isingekatika.
Kwahiyo wakuu, mtu ufanyeje ili unapoota ndoto uwe nusu uko usingizini na nusu uko macho?
 
hizo ni karama mkuu.

mm kuna kipindi naotaga halafu najiambia kabisa si ndoto hapa naomba wala sio kweli.
au naota nataka labda kupatwa na kitu kibaya.. nacontrol lile tukio nalirudisha nyuma ,halafu nalipeleka nnavyotaka mimi.

Yani kwa kifupi nacontrol ndoto mbaya ...80%
 
Hongera kwa kuwa na karama. Karama ni zawadi kubwa sana ambayo kila mtu anatamani kuwa nayo, bila kujalisha ni karama ya aina gani.
Karama siyo lazima uzaliwe nayo, ukifosi kuspecialize kwenye jambo fulani, basi wewe automatically unakuwa na karama kwenye hilo jambo ulilolifanyia bidii sana.
Tukija kwenye swali langu, kuota nusu uko umelala nusu uko macho haihitaji karama, ni maandalizi tu wakati unapoanza kulala, haihitaji mdalasini wala ubani Makka, ni maandalizi ya KIAKILI tu, mimi nataka nijue hayo maandalizi ya kisaikolojia unafanyaje?
 
Bora yako wewe unalala na remote control
 
Wahenga wanasema ndoto huwa haifiki mwisho. Ikifika mwisho unakufa hapo hapo! This is unproven theory but it sounds true.
 
Mh!
Mbona mimi nimeshaota ndoto mpaka mwisho mara nyingi tu?
Mwisho wa ndoto ni nini? Mwisho wa ndoto sio ndoto kuisha, bali ni hitimisho (conclusion). Ndoto nyingi tunazoota huwa hazina hitimisho (conclusion) yani zinaishia hewani-hewani. That is the 'what next' part of a dream remain unclear!
 
Mwisho wa ndoto ni nini? Mwisho wa ndoto sio ndoto kuisha, bali ni hitimisho (conclusion). Ndoto nyingi tunazoota huwa hazina hitimisho (conclusion) yani zinaishia hewani-hewani. That is the 'what next' part of a dream remain unclear..!
Kusingekuwa na hitimisho(conclusion) ya ndoto, watu wasingekuwa wanaota jambo halafu linatokea, huwezi kuota jambo likatokea mpaka ndoto yako iwe na hitimisho. Kwahiyo wapo wanaoota ndoto zenye hitimisho.
Au wewe unamaanisha hitimisho lipi la ndoto?
Fafanua kwa mfano.
 
Hongera kwa kuwa na karama. Karama ni zawadi kubwa sana ambayo kila mtu anatamani kuwa nayo, bila kujalisha ni karama ya aina gani.
Karama siyo lazima uzaliwe nayo, ukifosi kuspecialize kwenye jambo fulani, basi wewe automatically unakuwa na karama kwenye hilo jambo ulilolifanyia bidii sana.
Tukija kwenye swali langu, kuota nusu uko umelala nusu uko macho haihitaji karama, ni maandalizi tu wakati unapoanza kulala, haihitaji mdalasini wala ubani Makka, ni maandalizi ya KIAKILI tu, mimi nataka nijue hayo maandalizi ya kisaikolojia unafanyaje?
mh waulize kina Mshana mm binafsi sifahamu. ila nnachokijua nikitakaga kuota ndoto za maono ndio nakua nusu nusu tena mara nyingi zinakuaga za kutisha, labda mtu anakuja kukukaba,kukuchoma na kitu, ambapo unakua unaona mfano kama labda mnaishi family, labda mwenzio unamwita haitiki,unamshika hashikiki, na ukishtuka unajikuta kama umechomwa na kitu pale ulipochomwa panauma na kila kitu kipo kama ulivokua unaota.
 
Post yako inashabihiana na jina lako
Hahaha!!!!
Kufa=Usingizini
na
Kupona=Macho
Kwahiyo,
kufanakupona=nusu usingizini nusu macho.
Hiyo ID usiitilie maanani mkuu. Nimeichagua kutokana na lifestyle ninaloishi mtaani, yaani bila kupambana mpaka tone la mwisho, nitakuwa nimewaangusha wote wanaonitegemea.
 
mh waulize kina Mshana mm binafsi sifahamu. ila nnachokijua nikitakaga kuota ndoto za maono ndio nakua nusu nusu tena mara nyingi zinakuaga za kutisha, labda mtu anakuja kukukaba,kukuchoma na kitu, ambapo unakua unaona mfano kama labda mnaishi family, labda mwenzio unamwita haitiki,unamshika hashikiki, na ukishtuka unajikuta kama umechomwa na kitu pale ulipochomwa panauma na kila kitu kipo kama ulivokua unaota.
Kutokana na maelezo yako, ndoto unayoota nusu uko usingizini nusu uko macho, maana yake ni ndoto ya maono, si' ndiyo?
Maelezo ya mwisho kabisa sijayaelewa.
Mr. Mshana Jr njoo huku.
 
Ndiyo mkuu, tunazungumzia mambo ya ndoto.
Najua wewe ni mhenga, unaweza kutusaidia pa' kuanzia, tunajadili "ufanye maandalizi gani wakati unapoanza kulala ili usiku wa manane unapokuwa unaota uwe nusu usingizini nusu macho?"
 
Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom