Nifanyeje ili niweze kusomea Kilimo baada ya kushindwa gharama za Engineering?

Poluyakhtov

JF-Expert Member
May 9, 2017
353
296
Habari za usiku wakuu.

Bila kupoteza muda,niende moja kwa moja kwenye mada.
Mimi ni kijana wa kiume ambaye nilihitimu kidato cha sita miaka 4 iliyopita lakini sikufanikiwa kwenda chuo kikuu kwani alama nilizopata hazikukidhi vigezo.(Nilipata DEE katika mchepuo wa PCM),ni sababu nyingi zilipelekea kufanya kwangu vibaya kwani niliugua sana,hivyo nilihudhuria Shule kwa miezi 10 pekee,nikakuta wenzangu wanafanya
marudio tu ya walichokisoma na aliyekuwa ananisomesha alisema kama nitakariri darasa atashindwa kunilipia ada(Mama ndiye alikuwa ananisomesha kwa kuchoma mkaa).

Basi baada ya janga hilo nikafanya vibarua ili nirudie mtihani,nikafanikiwa kuanza Tuition,ajabu walimu wangu hawakuweza kuamini kama nilifeli kweli mtihani kutokana na namna nilivyokuwa muelewa.Tatizo likaja kwenye usajili wa kituo cha kufanyia mtihani,nikakwama kabisa kwani nilipigiwa hesabu zaidi ya 100,000 kama ada ya kituo shule ya Makongo.Nilishindwa kujiandikisha kwani nilikuwa nafanya kazi ya kuuza gazeti tu.

Mwisho nikaamua kutuma maombi DIT na WI ili nijiunge na kozi mojawapo za Engineering (Civil kwa DIT na Water Supply kwa WI).
Nilichaguliwa vyuo vyote,lakini sikujisajili baada ya kuona mzigo wa ada.Nilikumbwa na msongo wa mawazo unaonisumbu mpaka hii leo.

Sasa ndugu zangu naomba mnishauri nifanyeje ili niweze kusoma hata kozi Kilimo au maendeleo ya jamii,kwani huko ada ni nafuu kidogo.

Ufaulu wangu kidato cha nne upo hivi:-

Basic Maths C

Engineering Science C

Chemistry B

English C

Civics C

Kiswahili C

Geography D

Surveying C

Building Construction D

Architectural Draughting D

Division II-20.

Ushauri wenu ni muhimu sana ndugu zangu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Daaah Pole Sana Ndugu,a
Vipi Mkopo Uliomba?
Umejaribu Kutafuta Wadhamini\mdhamin?
Kama Una Ndoto Ya Kuwa Injinia Kwa Nini Usome Out Of Your Dream?
 
Mkuu usikae poteza muda somea ualimu upate kwanza fani,kwa masomo yako na matokeo yako upo vizuri,kupata kazi shule private na huo unaweza kuwa mtaji wa wew kwenda kusomea kitu unachotaka koz ukihifadhi mshahara kwa muda wa mwaka na nusu unapata Ada ya miaka 3 engineering course.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sawa mkuu,nimekuelewa na Asante kwa ushauri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari za usiku wakuu.

Bila kupoteza muda,niende moja kwa moja kwenye mada.
Mimi ni kijana wa kiume ambaye nilihitimu kidato cha sita miaka 4 iliyopita lakini sikufanikiwa kwenda chuo kikuu kwani alama nilizopata hazikukidhi vigezo.(Nilipata DEE katika mchepuo wa PCM),ni sababu nyingi zilipelekea kufanya kwangu vibaya kwani niliugua sana,hivyo nilihudhuria Shule kwa miezi 10 pekee,nikakuta wenzangu wanafanya
marudio tu ya walichokisoma na aliyekuwa ananisomesha alisema kama nitakariri darasa atashindwa kunilipia ada(Mama ndiye alikuwa ananisomesha kwa kuchoma mkaa).

Basi baada ya janga hilo nikafanya vibarua ili nirudie mtihani,nikafanikiwa kuanza Tuition,ajabu walimu wangu hawakuweza kuamini kama nilifeli kweli mtihani kutokana na namna nilivyokuwa muelewa.Tatizo likaja kwenye usajili wa kituo cha kufanyia mtihani,nikakwama kabisa kwani nilipigiwa hesabu zaidi ya 100,000 kama ada ya kituo shule ya Makongo.Nilishindwa kujiandikisha kwani nilikuwa nafanya kazi ya kuuza gazeti tu.

Mwisho nikaamua kutuma maombi DIT na WI ili nijiunge na kozi mojawapo za Engineering (Civil kwa DIT na Water Supply kwa WI).
Nilichaguliwa vyuo vyote,lakini sikujisajili baada ya kuona mzigo wa ada.Nilikumbwa na msongo wa mawazo unaonisumbu mpaka hii leo.

Sasa ndugu zangu naomba mnishauri nifanyeje ili niweze kusoma hata kozi Kilimo au maendeleo ya jamii,kwani huko ada ni nafuu kidogo.

Ufaulu wangu kidato cha nne upo hivi:-

Basic Maths C

Engineering Science C

Chemistry B

English C

Civics C

Kiswahili C

Geography D

Surveying C

Building Construction D

Architectural Draughting D

Division II-20.

Ushauri wenu ni muhimu sana ndugu zangu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nenda chuoni utapata maelekezo jinsi ya kujiunga,ni rahisi tu ,wahi matokeo yako mazuri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu usikae poteza muda somea ualimu upate kwanza fani,kwa masomo yako na matokeo yako upo vizuri,kupata kazi shule private na huo unaweza kuwa mtaji wa wew kwenda kusomea kitu unachotaka koz ukihifadhi mshahara kwa muda wa mwaka na nusu unapata Ada ya miaka 3 engineering course.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ualimu tena .??
You serious .??
Mkuu usije ukachukua ushauri wa huyu jamaa you will loose big time.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom