Nifanyeje ili niwe na uwezo mkubwa wa kufikiri?

Soma , Cheza.. Mengine yote ni assumption tu. Chakula kina upa ubongo wako capacity au potential ya kuwa critical thinker. lakini kuwa critical thinker unahitaji tu kusoma vitabu na kucheza michezo. hii ni kwa sababu kusoma ni kupata maarifa. na kucheza ni kutumia maarifa. kwahiyo ukisoma tu bila kucheza michezo au kufanya ubongo wako uchambue na kuunganisha maarifa uliyo nayo kutatua matatizo ni bure.

Kwa kifupi niseme ukitaka kuwa na uwezo mkubwa wa kufikiria, Basi Fikiria sana.
 
Watu wengi wamechangia kuwa ili uboreshe uwezo wako wa kufikiri kinachohitajika kwa kiasi kikubwa ni kuufanyisha ubongo wako mazoezi kama vile kusoma vitabu vingi ili kuongeza maarifa na hata kucheza michezo inayokufanya ufikirie. Wengine wamechangia kula vyakula vya nafaka zisizo kobolewa na wamesisitiza unga wa dona kwa kiasi kikubwa, wenye uelewa na vyakula tofauti na nafaka watuorodheshee ili tupate mbadala wa nafaka kwani kula nafaka muda wote zinaweza kukukinahi.

Kuboresha uwezo wako wa kufikiri kunahitajika kwa kiasi kikubwa kutokana na maisha ya sasa yanavyo kwenda, ushindani umeongezeka, migogoro, fursa zilizopo kuwa na ushindani, harakati za kuongeza vipato, n.k. Haya yote yanahitaji uwezo mkubwa wa kufikiri ili kukabiliana nayo, wenye uelewa njoni na data zilizokamilika ili tuelimishane vya kutosha kwani tunanufaika wengi!
 
OK mimi ninauelewa ili kuongeza uwezo wako wa kufikiri kwanza unatakiwa ujitambue wewe ni nani na unafanya nini kwa manufaa ya nani kwa muda gani, mpaka hapo utakuwa umeanza kuiumiza akili itoke nje ya boksi halafu anza kufikiria unakabiliwa na changamoto gani? chanzo chake ni nini? utazimalizaje? Utatumia njia gani? hapo pia itakusaidia kuanza kuwa na mawazo chanya. Pia penda kuwa unakaa na watu wa tofauti na kiwango chako cha maisha kwa maana ya juu yako hawa mara nyingi watakusaidia jinsi ya kufanya mambo kwa namna na kiwango chao itakupa changamoto na utakuwa unaendelea kukua siku hadi siku.

Mengine usile bila mpangilio kula kwa-

NB: WATU WENGI HUCHUKULIA MATATIZO YAO NI KAMA MIKOSI AU HAYATAKIWI KUJA KWAO, MATATIZO YAPO NA LAZIMA YAJE, CHUKULIA KILA TATIZO NI CHANGAMOTO SIO TATIZO .
 
Soma vitabu vya ma great thinker kama kina aristotle,smith,kiyosaki pia soma magazeti yenye kuelimisha zenye makala nzuri achana na magazeti ya rangi rangi upe mazoezi ubongo kwa kureason reason vitu utakavyoviona n.k
 
Nashukuru kwa michango yenu wakuu! Lakini, watu wa vijijini wanakula sana nafaka zisizokobolewa lakini uwezo wao bado ni mdogo hata kuweza kuzitambua fursa zilizopo katika mazingira yao ziwakwamue katika umasikini ulio kithiri inakuwa bado ni shida, hii inakuwaje? Waliochangia na kusisitiza nafaka zisizo kobolewa naomba waelezee kidogo kuhusu hili jambo.

Naungana na mkuu Pasco...Mshua is not true bona fide genuine tha man can think otherwise asinge kuwa ana argue namna hii...
 
kuwa na akili ya kutambua vitu na kukabiliana navyo ninaweza kusema ni 1]kipaji
2]mazingira
3]changamoto
4]Elimu
Nilibahatika kusoma vitabu vya dini kimojawapo ni cha hekima ya sulemani
kina mapana sana,
kwa mfano huyu sulemani aliletewa kesi ya akina mama wawili walikuwa wanabishana[wakimgombea mtoto
kila mmoja akisema ni wa kwake. hiyo kesi ilipofikishwa kwa sulemani akawaita wale akina mama, akamchukua yule mtoto akawauliza ni nani mama wa huyu mtoto?
kila mama akasema ni wa kwake.
kwa haraka haraka na kwa kuwa sulemani hakujua ni nani mwenye uhalali wa yule mtoto akawaambia, ni sawa kila mmoja anadai kuwa mtoto ni wa kwake na mtoto ni mmoja, sasa mimi nitampasua katikati kila mmoja wenu achukue kipande kimoja. baada ya sulemani kusema hivyo yule mama ambaye mtoto hakuwa wa kwake akasema ni sawa.
kwa sababu hakuwa na uchungu naye na hakuwa mtoto wake. lakini yule ambaye alikuwa mama halali wa mtoto akasema hapana usimpasue mtoto, ni bora mimi nimkose apewe huyo mama aliyetaka mtoto apasuliwe vipande viwili awe wa kwake. hapo sulemani akamtambua mama wa mtoto kuwa ni yule aliyekuwa na uchungu naye. nina maana sulemani hakusoma ila alikuwa na kipaji cha kufikiri kwa haraka na kutoa maamuzi ya haki.
ninaungana na wachangiaji kuwa unaweza kusoma sana lakini usiwe na maarifa. ni mara ngapi wasomi wetu tuliowaamini wanashindwa hata kuingia mikataba mizuri na wawekezaji? badala yake wanaingia mikataba mibovu ya kutugharimu maisha yetu yote?

Mkuu nashukuru kwa ushauri wako, naomba unipe falsafa moja tu nianze kuufanyia kazi ushauri wako kwa kuitafakali hiyo falsafa iwe kama mwanzo wa utekelezaji wa ushauri ulionipa.

"Unaweza kudanganya watu wote kwa wakati fulani, na unaweza kudanganya watu fulani wakati wote lakini huwezi kudanganya watu wote wakati wote" wadau watakusaidia kujua ni mwanafalsafa gani huyo, wewe ifikirie kwanzan hiyo kama ina maan kwako
 
Mm jana nilikwenda kumpa pongezi mzazi aliyejifungua,mtoto alikuwa hata hajatimiza masaa 24,nikapata udadisi wa kujua huyu mtoto kwa sasa ubongo upo vp,unavyofanya kazi and the like. Nikaingia intaneti nikasoma. Ukiwa na mawazo haya inasaidia sn.
 
kuna wakati nami niliwaza kama wewe, watu wa karibu walionipa ushauri ni kwamba nisome vitabu nami nafanya hivyo ilakiukweli maandishi mengi yenye kugawa maarifa yapo katika lugha ya kiingereza, so anza kujifunza kiingereza kwanza.
 
OK mimi ninauelewa ili kuongeza uwezo wako wa kufikiri kwanza unatakiwa ujitambue wewe ni nani na unafanya nini kwa manufaa ya nani kwa muda gani, mpaka hapo utakuwa umeanza kuiumiza akili itoke nje ya boksi halafu anza kufikiria unakabiliwa na changamoto gani? chanzo chake ni nini? utazimalizaje? Utatumia njia gani? hapo pia itakusaidia kuanza kuwa na mawazo chanya. Pia penda kuwa unakaa na watu wa tofauti na kiwango chako cha maisha kwa maana ya juu yako hawa mara nyingi watakusaidia jinsi ya kufanya mambo kwa namna na kiwango chao itakupa changamoto na utakuwa unaendelea kukua siku hadi siku.

Mengine usile bila mpangilio kula kwa-

NB: WATU WENGI HUCHUKULIA MATATIZO YAO NI KAMA MIKOSI AU HAYATAKIWI KUJA KWAO, MATATIZO YAPO NA LAZIMA YAJE, CHUKULIA KILA TATIZO NI CHANGAMOTO SIO TATIZO .

Mkuu kwa hili jibu nimekukubali! Nilikuwa nahitaji jibu kama hili, yaani kufikiria ili uweze kutatua changamoto zinazo kukabili kwa wakati huo. Ni njia nzuri ingawa inategemea na tatizo lenyewe aidha linahitaji majibu ya papo kwa papo au ya muda mrefu. Pia inategemea na maamuzi yako aidha ya haraka au ya polepole. Thanks!
 
Nimekua nikisikia kuwa watu waliosoma sana ndio wenye uwezo mkubwa wa kufikiri. Je mimi ambaye nimekomea darasa la saba, nifanyeje ili niboreshe uwezo wangu wa kufikiri ilihali sina uwezo wa kuendelea na masomo zaidi ya hapo?

Endelea kufikiri!
 
Soma vitabu vya ma great thinker kama kina aristotle,smith,kiyosaki pia soma magazeti yenye kuelimisha zenye makala nzuri achana na magazeti ya rangi rangi upe mazoezi ubongo kwa kureason reason vitu utakavyoviona n.k

Mkuu nashukuru kwa ushauri wako, vitabu nimeanza kuvikusanya na nimevipata kama 9 hivi toka humu humu JF, nitaanza na hivyo!
 
Kwa kifupi niseme ukitaka kuwa na uwezo mkubwa wa kufikiria, Basi Fikiria sana.

Nimeipenda hii sana. Vile vile kuanzia leo kila analowaza aweke kwenye maandishi, kila akiota ndoto asubuhi aiandike kwenye kadaftari afu atafute ndoto na fikirio vinavyoungana ili apate habari iliyombele yake!
 
Kula sana mayai

Mkuu mayai yanamadhara hasa yale ya kuku wakisasa, wanasema yana-chemicals ambazo si nzuri kwa afya. Pia, ukila mayai mara kwa mara yatakufanya unenepe sana. Ukinenepa sana mwili utakuwa mzito na badala yake utakua vulnerable na magonjwa mengi. Kwanza kusinzia sinzia hovyo, mvivu, magonjwa ya moyo, kisukari n.k. Hii ni kutokana na uzoefu wangu pia sayansi kimu niliyosomaga miaka ileeeee! Waliosoma hivi karibuni wanaweza kuweka vitu vipya vinavyoonyesha uwiano uliopo kati ya kula yai na kuongeza uwezo wa kufikiri!
 
kuwa na akili ya kutambua vitu na kukabiliana navyo ninaweza kusema ni 1]kipaji
2]mazingira
3]changamoto
4]Elimu
Nilibahatika kusoma vitabu vya dini kimojawapo ni cha hekima ya sulemani
kina mapana sana,
kwa mfano huyu sulemani aliletewa kesi ya akina mama wawili walikuwa wanabishana[wakimgombea mtoto
kila mmoja akisema ni wa kwake. hiyo kesi ilipofikishwa kwa sulemani akawaita wale akina mama, akamchukua yule mtoto akawauliza ni nani mama wa huyu mtoto?
kila mama akasema ni wa kwake.
kwa haraka haraka na kwa kuwa sulemani hakujua ni nani mwenye uhalali wa yule mtoto akawaambia, ni sawa kila mmoja anadai kuwa mtoto ni wa kwake na mtoto ni mmoja, sasa mimi nitampasua katikati kila mmoja wenu achukue kipande kimoja. baada ya sulemani kusema hivyo yule mama ambaye mtoto hakuwa wa kwake akasema ni sawa.
kwa sababu hakuwa na uchungu naye na hakuwa mtoto wake. lakini yule ambaye alikuwa mama halali wa mtoto akasema hapana usimpasue mtoto, ni bora mimi nimkose apewe huyo mama aliyetaka mtoto apasuliwe vipande viwili awe wa kwake. hapo sulemani akamtambua mama wa mtoto kuwa ni yule aliyekuwa na uchungu naye. nina maana sulemani hakusoma ila alikuwa na kipaji cha kufikiri kwa haraka na kutoa maamuzi ya haki.
ninaungana na wachangiaji kuwa unaweza kusoma sana lakini usiwe na maarifa. ni mara ngapi wasomi wetu tuliowaamini wanashindwa hata kuingia mikataba mizuri na wawekezaji? badala yake wanaingia mikataba mibovu ya kutugharimu maisha yetu yote?

Mkuu umeleta hoja nyingine 'kufikiri haraka na kwa maamuzi sahihi', hii ni zaidi ya kusoma vitabu, na calculations pia! Nashukuru kwa kuja na mtazamo tofauti!
 
Njia ya asili na rahisi sana kopa hela popote pale iwe nyingi au kidogo halafu zitafune kisha anza kudaiwa,

Lazima akili ikukae sawa!
 
Mkuu kwa hili jibu nimekukubali! Nilikuwa nahitaji jibu kama hili, yaani kufikiria ili uweze kutatua changamoto zinazo kukabili kwa wakati huo. Ni njia nzuri ingawa inategemea na tatizo lenyewe aidha linahitaji majibu ya papo kwa papo au ya muda mrefu. Pia inategemea na maamuzi yako aidha ya haraka au ya polepole. Thanks!

Pia, ni muhimu wewe mwenyewe kung'amua Mazingira uliyopo na Nyakati zilizopo katika eneo lako, kisha tambua WAJIBU wako kulingana na Nyakati na Mazingira mahususi! Sasa pima kila uonacho, kusikia, kutenda, kula, kuhisi, kuwaza, n.k Je, VINA NAFASI GANI KATIKA KUTIMIZA/KUTEKELEZA WAJIBU WAKO? HOJI! Usipokee tu kila kitu vile kinavyokuja, bali KIPIME NA NAFASI YAKE KATIKA KUTEKELEZA WAJIBU WAKO KWA JAMII YAKO! Kamwe usitende jambo lolote pasi kumfikiria jirani yako. HUSIANISHA MIFUMO, SERA, MAZOEA, ITIKADI, IMANI, MITAZAMO, n.k na WAJIBU WAKO KATIKA JAMII. Pima kama hayo yote yana-guarantee WAJIBU wako ama yanakiuka! Hivyo, hatua muhimu na bora ni KUTAMBUA WAJIBU WAKO KATIKA JAMII. Kwa ziada, soma vitabu vya Fasihi kwa wingi!
Mungu wetu yu tayari kutupigania vitani. Anaita sasa!
 
"Unaweza kudanganya watu wote kwa wakati fulani, na unaweza kudanganya watu fulani wakati wote lakini huwezi kudanganya watu wote wakati wote" wadau watakusaidia kujua ni mwanafalsafa gani huyo, wewe ifikirie kwanzan hiyo kama ina maan kwako

Mkuu kama falsafa ndiyo ziko hivi ni hakika ukizisoma mara kwa mara uwezo wako wa kufikiri utaongezeka maradufu, sababu inabidi uzisome mara mbili mbili ndipo uelewe. Nili-google siku moja nikakutana nazo za ma-great thinker kama martine luther king, darwin na wengine....., zilibadiri hisia na mtazamo wangu ki fikra. Nashukuru kwa falsafa yako na kwa jinsi nilivyojaribu kuitafakari nimeona inaukweli ndani yake. Na kama kweli ukibobea kuwa mwanafalsafa, ni wachache sana katika jamii ya sasa watakao kuwa wanakuelewa. Mfano mzuri ni mkanda wa Yesu, alikuwa hana kauli za moja kwa moja alipokuwa akijibu maswali, alio wajibu iliwabidi wafikirie mara mbili mbili, kama vile "ni vigumu kwa ngamia kupenya tundu la sindano, kuliko mwanadamu kuuona ufalme wa mbinguni". Nashukuru kwa mchango wako!
 
Mm jana nilikwenda kumpa pongezi mzazi aliyejifungua,mtoto alikuwa hata hajatimiza masaa 24,nikapata udadisi wa kujua huyu mtoto kwa sasa ubongo upo vp,unavyofanya kazi and the like. Nikaingia intaneti nikasoma. Ukiwa na mawazo haya inasaidia sn.

Mkuu nashukuru kwa techniques zako, yaani kuwa mdadisi kwa kile unacho kiona kwa kukifanyia utafiti japo kidogo. Thanks!
 
Back
Top Bottom