Nifanyeje ili niwe na uwezo mkubwa wa kufikiri?

1.jishughulishe na mambo ya kufikirisha!
2.tumia muda wako mwingi na watu walio kuzidi uwezo kifikra!
3.acha kujishughulisha na mambo ya kipuuzipuuzi!


Nashukuru kwa ushauri mkuu. Dah! Kumbe inabidi uwe siriazi sana ili kukuza uwezo wa kufikiri, ikiwezekana hakuna kucheka na mtu. Nimekusoma mkuu!
 
jifunze kwanza kiingereza ili uweze kusoma vitabu vyenye maarifa..
pia
Mkubwa naomba nikuunganishe na hawa watu wakupe mambo.. EMT, Pasco, Kiranga..pia Mzee Mwanakijiji.. Wakusaidie zaidi!!


Mkuu asante kwa ushauri, English Course niliwahi kusoma ndio maana najua hata kupost uzi hapa jamii forum. Hao watu uliowataja hapo juu natumaini wakichangia kwenye huu uzi tutapata majibu mengi yatakayo kidhi haja!
 
Last edited by a moderator:
Nimekua nikisikia kuwa watu waliosoma sana ndio wenye uwezo mkubwa wa kufikiri. Je mimi ambaye nimekomea darasa la saba, nifanyeje ili niboreshe uwezo wangu wa kufikiri ilihali sina uwezo wa kuendelea na masomo zaidi ya hapo?


Kuna uzi mwingine kama huu upitie watu walijaribu kuelezea mengi. Bofya hapa: https://www.jamiiforums.com/jamii-intelligence/138113-naweza-kuongeza-uwezo-wa-kufikiri.html

Epuka kusoma au kusikiliza habari ambazo zinazungumzia upande mmoja tuu. Kwa mfano, nimeona LumumbaDAR akikushauri ujiunge na Chadema kama vile tayari anajua wewe ni mfuasi wa chama kingine. Ni lile lile tatizo la kufikiria kila kitu kwa kutumia siasa.

Siyo yote yanayosemwa na Chadema ni sahihi na siyo wote walioujiunga na Chadema wana uwezo mkubwa wa kufikiri. Na kwa siasa zetu hizi za maji taka sidhani kama kuna lolote la maana la kujifunza.

Kwa hiyo, jitahidi na usiruhusu ubongo wako ufungamane na upande wowote ule. Hata kama unafungamana na upande mmoja, uwe huru kuangalia au hata kukubaliana na upande mwingine wa hoja pale inapolazimu. Hii itakusaidia kupanua uelewa wako kwenye mambo mengi.

Usikubali au kumkataa mtoa hoja, bali kubali au pinga hoja yake kwa kujaribu kuja na hoja yako. Kama huna hoja unaweza kukopa hoja ya mtu mwingine kusizitiza unachokisema. Usiwe unakubaliana na hoja moja kwa moja. Kuwa na desturi ya kutaka kuhoji. Hata kama unakubaliana na hoja yake, uwe na sababu za kufanua hivyo. Usikubaliane au kukosoa hoja kwa vile tuu imetolewa na mtu fulani.

Naelewa Tanzania kuna tatizo la mtu kuonekana mhaini pale unapohoji jambo. Mwanasiasa anaweza kusema kitu, ukaanyoosha mkono na kuuliza swali la kuhoji alichosema, baada ya hapo utajikuta umepigwa "Tanganyika jeki". Hatuna desturi ya kukubali kuhojiwa bali tunataka kukubaliwa na kila kitu tunachokisema hata kama siyo sahihi. Ukifanikiwa kuepuka hilo utakuwa na uhuru wa fikra.

Jaribu kusoma mara kwa mara. Hapa utakumbwa na tatizo maana vitabu vingi vimeeandikwa kwa Kiingereza. Hata hivyo, mababu zetu hawakusoma sana na wanatoa hoja nzuri sana kwa kutumia busara na hekima zao.

Huitaji uwezo mkubwa sana kuelewa au kuhoji mambo. Tumia uelewa na ujuzi wa kawaida ambao kila mtu anao (common sense) hata kama hajaenda shule. Kwa mfano, kama LumumbaDAR anakushauri ujiunge na Chadema ili uwe na uwezo mkubwa wa kufikiri mhoji kwani wote walioko Chadema wana uwezo mkubwa wa kufikiri? Au wale wooooote wasio Chadema hawana uwezo mkubwa wa kufikiri? Vipi wale ambao hawapo upande wowote ule?

Jibu atakalokuja nalo utagundua kuwa pamoja na yeye labda kuwa na elimu ya chuo kikuu na wewe kuwa na elimu ya darasa la saba, wala hamjapishana sana katika kufikiri na kuhoji. Tumia busara, hekima, na common sense (uelewa na ujuzi wako wa kawaida ulionao).

Tatizo la watu ambao hawajaenda shule wanaamini kuwa walioenda shule wana akili sana. Hata hivyo, wengi hawakufanikiwa kwenda shule kwa sababu mbalimbali. Na kama wale walieonda shule wana uwezo mkubwa sana wa kufikiri, basi nchi yetu isingekuwa hapa ilipo. Si inaendeshwa na "first class economists" (wasomi waliofaulu vyuo vikuu kwa alama ya "A")?
 
Mkuu nashukuru kwa ushauri wako, naomba unipe falsafa moja tu nianze kuufanyia kazi ushauri wako kwa kuitafakali hiyo falsafa iwe kama mwanzo wa utekelezaji wa ushauri ulionipa.

Nikupe mimi tena!!! kasome!! soma kwenye vitabu, kwenye magazeti, kwenye mitandao!! Ua labda unatania huna lengo la kujifunza unataka kujaribu watu...ungebadilisha namna ya kuuzliza sasa!
 
Nimekua nikisikia kuwa watu waliosoma sana ndio wenye uwezo mkubwa wa kufikiri. Je mimi ambaye nimekomea darasa la saba, nifanyeje ili niboreshe uwezo wangu wa kufikiri ilihali sina uwezo wa kuendelea na masomo zaidi ya hapo?
Mkuu Mshua's, japo "graphology" yangu inaniambia you are not "bona fide genuine!" ila tuendelee.
Kwanza sii kweli kuwa waliosoma sana ndio wenye uwezo mkubwa kufikiri!, ma great thinkers kibao, wavumbuzi, wagunduzi na magenius kibao sio watu waliosoma sana!.

Kusoma sana ni jambo moja,
Kuwa na akili za darasani ni jambo jingine,
Kuwa genius ni jambo jingine,
na uwezo wa kufikiri ni jambo jingine kabisa!.

Mababu zetu hawakusoma hata darasa moja na walikuwa na uwezo mkubwa sana kufikiri!.
Na tunashuhudia ma profesa kibao ni Ph.D za ukweli and yet hawana uwezo wowote wa kufikiri!.

Ili kuboresha uwezo wako wa kufikiri, kula vizuri vyakula vya raw protein in nature, fanya mazoezi, pata muda wa kutosha kupumzika/kulala au ku meditate, then soma vitabu kuongeza maarifa, kama ni Mkristu, anza na Biblia Takatifu, akianzia na kitabu cha Mithali, then Mhubiri, na vingine, soma huku ukitafakari. Then kasome maandishi ya ma GT hata wa humu jf, uwezo wako wa kufikiri utaimprove!.

Pasco.
 
1. Tumia bhangi, walau mche mmoja kila unapotaka/ unapoamua kufanya jambo la kufikirisha.

2. Kunywa walau kiroba kimoja kwa siku.

Tehe tehe! Kufikiria ni kipaji can never be created or destroyed.
 
1. Tumia bhangi, walau mche mmoja kila unapotaka/ unapoamua kufanya jambo la kufikirisha.

2. Kunywa walau kiroba kimoja kwa siku.


mbona kuna jukwaa la jokes ina maana hujaliona au kuza ufaham mwana
 
kaka uciamn kila aliyeko chuo ana uwezo mkubwa wa kufikiri ila wanakuzidi tu kwa kujua vingi hata ww uwezo unao soma sn vitabu halafu neno cwezi futa katika fikra zako tumia sana akili kuweza kila kitu ni kigumu kwa upande wake halaf soma methali sn
 
pendelea kucheza chess na sio draft,itakufanya ufikirishe bongo na ambayo ndio mazoezi yenyewe ya kufikiria,meditation pia inasaidia,na kusoma vitabu mbalimbali vya hadithi,riwaya,majarida ya kisayansi itakuongezea maarifa na uelewa
halaf usipende kubishana pendelea kujadiliana na uwe tayar kujifunza kitu kwa mtu mnayejadiliana nae
 
asiipende ccm hata kwa kusikia, awe tayari kufa kwa ajili ya cdm, km hana kadi ya cdm akaichukue, nimefanya hivyo na nimefanikiwa!

Usiwasikilize hawa (LumumbaDAR & UNDENIABLE). Kuchagua vyama ni habari nyingine ambayo utaifanya wewe mwenyewe na kumbuka UZALENDO kwanza SIASA baadae.
Jaribu kusoma vitabu vingi haswa vya psychology.....
Utakuwa na uwezo mkubwa wa kumake hard decisions and to cope with others.....
 
Nashukuru kwa michango yenu wakuu! Lakini, watu wa vijijini wanakula sana nafaka zisizokobolewa lakini uwezo wao bado ni mdogo hata kuweza kuzitambua fursa zilizopo katika mazingira yao ziwakwamue katika umasikini ulio kithiri inakuwa bado ni shida, hii inakuwaje? Waliochangia na kusisitiza nafaka zisizo kobolewa naomba waelezee kidogo kuhusu hili jambo.
 
Nashukuru kwa michango yenu wakuu! Lakini, watu wa vijijini wanakula sana nafaka zisizokobolewa lakini uwezo wao bado ni mdogo hata kuweza kuzitambua fursa zilizopo katika mazingira yao ziwakwamue katika umasikini ulio kithiri inakuwa bado ni shida, hii inakuwaje? Waliochangia na kusisitiza nafaka zisizo kobolewa naomba waelezee kidogo kuhusu hili jambo.

mkuu kuwa na uwezo mkubwa wa kufikiri ni issue inayohusisha vitu vingi kwa mf vyakula ambavyo ndivyo vinaupa ubongo nishati,vile vile ni suala la mazingira je ni mazingira gani umekulia je mazingira uliyokulia yalikufanya uwe na tabia ya udadisi au kutaka kujua na kujifunza vitu vingi tofauti tofauti ambavyo vinakujenga akili yako,pia ni suala la genes za intelligence ulizopata kutoka kwa wazazi wako ambalo nafkiri ndilo lina play part kubwa katika hili suala so nafkiri hii issue ni inborn
 
Asante kwa wachangiaji wanaojua huu ni moja ya uwanja wa ku-expand huo uwezo wa akili.Intelligence ya mtu ipo aina mbili(1)natural by born(2)self make.hizi akili za asili(natural by born) SIO ZA KURIDHI KWA NAMNA YOYOTE ILE hazihusu uchaguzi wa mzazi wala mtoto na saa zingine mtoto kama huyu anazaliwa familia maskni yenye karaa nyingi lakini mara nyingi intelligence capacity zao hu-survive.adhari za mazingira na situation zingine kama elimu na malezi ndo hu-result watakavyokujakutumia intellgence zao,uzingatie matapeli,majambazi,wezi wa mifikoni,magaidi ni ma brilliant intelligent by born wakubwa ila situation nlizotaja zikawa-lead kuwa walichokua.Self make:Malezi bora yanachangia kwa kiasi kikubwa ila wengine wanawezapata hayo malezi bora in term ya lishe ila wasiwe ntelligent kivile au anatokea baridi tu kabisa kama lishe hazikulengwa kuushuulika na ubongo na kuelekezwa kwenye vitu kama mazoezi n.k.Tool kubwa kabisa ya self make ni kujitambua na kujifunza procedure kwa %99 haishindikani.
 
Kwanza kama huwa unatabia ya kuamka saa moja asubuhi badala la ya saa 11asubuhi au 12 ubongo utakuwa ulisha ulemaza chamsingi kama unatabia hiyo tafuta mtu kila inalofika saa12 kama bdo ume lala basi akumwagiye maji na ukiendelea na tabia hiyo awe kala unapo pitiliza akuchape fimbo 5kila unapo pitiwa asubuhii hii itasaidia ku boost ubongo wako ukisha weza kuamka bila shida saa11asubuhi nitakujulisha nini kingine chakufanya ndio mchango sahii na dawa mbadala
 
Nimekua nikisikia kuwa watu waliosoma sana ndio wenye uwezo mkubwa wa kufikiri. Je mimi ambaye nimekomea darasa la saba, nifanyeje ili niboreshe uwezo wangu wa kufikiri ilihali sina uwezo wa kuendelea na masomo zaidi ya hapo?

Naomba ufahamu kuwa kufikiri kwa mazoea hujenga tabia ya kufikiri. Ukishakuwa na tabia ya kufikiri na usomasoma kwa dunia ya leo elimu iko wazi katika vitabu, katika internet nk nk. Kwa hiyo ndugu yangu jijengee tabia ya kusoma na kufikiri mwisho wa siku utatisha.
 
Back
Top Bottom