Nifanye nini..?!

Mtile

Senior Member
May 25, 2013
126
87
Mimi nina mchumba wangu(kike), na tunapendana sana, lakini hivi karibuni amepata kazi huko mbugani serengeti kwenye hoteli fulani ya kitalii na inamlipa vizuri sana.
Ila tatizo lililopo ni kwamba, mimi naishi DSM, na masharti ya kazi yake ni kwamba, atapata likizo kila baada ya miezi sita, ina maana ni mara mbili tu kwa mwaka, na kila likizo ni wiki tatu tu.
SASA Nachanganyikiwa, je mwenzangu ataweza kuvumilia vishawishi wakati wote akiwa huko mbugani(kazini).
Je, uhusiano na mapenzi yetu yatadumu kwa mfumo huu wa maisha.

TAFADHALI wana MMU NISHAURINI....
 
wewe je utaweza kuvumilia vishawishi?
hapo sasa inabidi kila weekend uwe unafunga safari serengetiiii ili mwenzio asishawishike!!
 
Itawezekana kwa kuomba ulinzi wa MWENYEZI MUNGU ILA NAWE UNATAKIWA KUWA MWAMINIFU.
 
kwanza kakudanganya,haya mahoteli ya kitalii hayalipi vizuri hata kidogo,yani yanalipa ule mshahara wa kima cha chini kilichopangwa na serikali kwa sekta ya huduma za kitalii.Hapo mkuu fifty fifty kama uhusiano wenu utadumu.Watu wanedna na pochi zimeshiba haswa na kama mtoto ni bomba sahau
 
mhh..acha kumtisha mwenzio!
 
Lah??!!
Unajua maisha ya mbugani au unayasikia tu??

Nakushauri Mrudishe na atafute kazi sehemu nyingine, la sivyo.........
 
wewe je utaweza kuvumilia vishawishi?
hapo sasa inabidi kila weekend uwe unafunga safari serengetiiii ili mwenzio asishawishike!!

Daahh... Hiyo Bajeti Ya Dar - Arusha Ntaimudu Kweli??
Mbona Mwaka Huu Nimepata Mtihani.
 
Pole kwa kuwaza hayo,kama unampenda kwa dhati utaweza kuvumilia,kama kuna uwezekano wa kupata kazi maeneo ya karibu fanya ivyo kumtafutia..ila mapenzi ya siku izi kama unawaza kuna kiumbe anakuibia basi jua ni kweli
 
1st jiulize na ujibu mwenyewe,Unaweza kumtimizia mahitaji yake akiacha hiyo kazi!?,Coz mlipokubaliana kuanza kazi huko porini hukumuuliza mwana JF yeyote why now keshaanza kazi ndo uanze kuwa na wasiwasi nae?.Tulia Mtoto apige kazi bhana.
 
kwanza kakudanganya,haya mahoteli ya kitalii hayalipi vizuri hata kidogo,yani yanalipa ule mshahara wa kima cha chini kilichopangwa na serikali kwa sekta ya huduma za kitalii.Hapo mkuu fifty fifty kama uhusiano wenu utadumu.Watu wanedna na pochi zimeshiba haswa na kama mtoto ni bomba sahau

La Haula..!! Na vile alivyo nona, ww acha tu, ndio maana nashindwa kuamua aidha nimrudishe au aendelea na kazi...?? ila ngoja ni test miezi hii miwili ya mwanzo, then nitakuwa kwenye position sahihi ya maamuzi...
 
^^
Haya mapenzi ya mbali wakati mti haujatoa matunda,,ni kama ka tangazo kadogo ka kuachana ambako hakajalipiwa
^^
 
Unamhofia yeye tu, wewe haujionei wasiwasi? Muache afanye kazi huku mnatafuta mahali pengine. Meanwhile kuonyesha unajali kiasi gani, hebu tuanze mipango ya ndoa basi.

Hata Mm Pia najihofia, ndio maana nikahoji MAHUSIANO NA MAPENZI YETU YATADUMU KWA MFUMO HUU WA MAISHA??
Pia mipango ya ndoa imeshaanza, ndio maana ni WACHUMBA.
 
Yani miez 6 roho juu juu.. What kind of life it iz?? Hicho ndo kipimo ujue kama nyie ni waaminifu or ndo viruka njia mnao tumia mwamvuli wa ndoa
 
La Haula..!! Na vile alivyo nona, ww acha tu, ndio maana nashindwa kuamua aidha nimrudishe au aendelea na kazi...?? ila ngoja ni test miezi hii miwili ya mwanzo, then nitakuwa kwenye position sahihi ya maamuzi...
Kumbe ndiye huyu alieanza kazi hapa kama wiki mbili zilizopita? Kwa jinsi wazungu wanavyokata dola hapa kwa hawa wanawake wa kiafrika, sidhani kama ndani ya mwezi mmoja atakukumbuka tena. Andika maumivu.
 
daaah inamana hao jamaa hawatambui mahusiano? yani hiyo ni kali sijawahi kuona. kwani hawaruhusu ww kumtembelea? kama wanaruhusu jitahidi uwe unaenda hata kila mwezi tofauti na hapo hako ni kekundu mana yake kubali matokeo umeliwa.
 
Back
Top Bottom