Nifanye nini Mume wangu aache pombe na sigara? Hakuwa hivyo zamani

Kwa pombe kuwekewa mkojo wa punda

Atatapika sana kisha hatokunywa tena

Kwa sigara sijui
Kuna jamaa aliwahi kuniambia hiyo formula ya kuacha pombe. Daaah vitu vichafu lakini akasema ndio anatapika kila akinywa pombe, na ataacha tu.
 
Sio ajabu wewe ndio chanzo cha yeye kuwa mlevi, wewe jitathmini Kama kuna mahali umebadilika ndio na yeye kabadilikia hapo hapo
 
Usemalo lina ukweli mkuu bt ushawahi fikiria au kupitia maumivu ya kuona ndani huna mahitaji ya kutosha ila unajinyima mumeo asitoke ndani hana kitu mfukoni? Na kidogo hichohicho unachomsupport ndo anaenda kunywea pombe? pia isitoshe mnamtoto mdogo ila huoni support ya baba yakutosha
Mimi nimekuelewa mama ake.

Kutokana na maelezo yako (kama ni kweli), bado unampenda mumeo na unataka yaliyo mema kwa ajili ya familia yako.

Jamaa inaonekana amejikatia tamaa kabisa baada ya kupoteza kazi na ameshindwa kabisa kujirudi na kuwa baba na mume mwema kama hapo mwanzo.

Jamaa anasumbuliwa na depression. Hapo akifikiria kuwa anashindwa kuihudumia familia yake kama hapo mwanzo ni lazima asiwe sawa.

Mmejaribu kuwashirikisha wazee wenu? Wasimamizi wenu wa ndoa? Rafiki yake anayeheshimiana naye labda?

Pia jaribuni kupata huduma ya kitabibu kwa kuwaona therapists na watu wa psychology.
 
Back
Top Bottom