Nifanye nini Mshahara uweze Usiishe

nashukuru mzima

JF-Expert Member
Jul 11, 2017
1,014
1,896
Habari za siku wakuu.

Mimi Ni kijana wenu baada ya miahangaiko ya Kutafuta Ajira Mungu mwema mwezi huu niliingia mkataba na shirika Fulani ambalo ni mkataba wa mwaka mmoja.

Sasa kwanini nimekuja kwenu naona Kichwa kishaanza kuwaka Moto lastly week nimepokea Mshahara lakini Hauwezi Kuamini Jumanne umeisha Wote.

Kuna mwanamke Ambaye natarajia aje kuwa mke wangu nimemuweza Kwa biashara,ndugu wa karibu nimeweza kuwapa Pia.

Naombeni Ushauri nifanyaje mshahara ukae maana naona Tunakoelekea mkataba unaweza kuisha na Hakuna Cha maana nilichopata.

Wakuu mnisaidie mdogo wenu

Basics ni kama 950K
 
Mshahara hautoshi hata upokee milioni ngapi kutokana utaishi kulingana na level ulinayo muhimu japo sijajua mkataba ni wa muda gani

1.muelekeze mwenzio kuwa kazi ni mkataba ukiisha inabid muwe
mshatengeneza kitu Cha kuwasogeza

2.punguza matumiz yasiyo ya lazima muhimu kula Kodi na balance ya kukusogeza mwezi uishe na emergency

3.fungua akaunt iwe kwaajili ya kuweka pesa pindi mshahara unapotoka hata km kidogo ifunge kwa muda wakat unafikiria njia nyingine ya kuongeza kipato Cha ziada

4.usikurupuke chunguza unachotaka kufanya weka malengo Ila kuwa na kipato Cha ziada ni lazima bila hivo hutoboi

5.kubali kipato ulichonacho ishi kulingana na malengo yako jibane utatoboa

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Mshahara ni calculated kwa ajili ya mtu mmoja na sio familia na una lengo la kumfanya mwajiriwa asife yaani amudu kufika kazini kutumika. Akifika miaka 60 anatupwa anaajiriwa mwenye nguvu kwa circle hio hio. Mwajiriwa ni SAwa na limao lina thamani kabla alijakamuliwa
 
Subiri kwanza upokee mishahara 6 ndo akili itakaa vizuri maana wenge la mshahara wa kwanza ni lazima ujidai ni mwema na unataka kusaidia kila mtu utajiona Elon musk kwamba unaweza kutatua umasikini wa ukoo.

Siku ukipokea mshahara na akili yako ikawa haiwazi tena kununua nguo na viatu na kila unaemsaidia hatosheki ndo ujue hapo akili imeanza kukomaa unaweza kufanya kitu Cha maana
 
Habari za siku wakuu.

Mimi Ni kijana wenu baada ya miahangaiko ya Kutafuta Ajira Mungu mwema mwezi huu niliingia mkataba na shirika Fulani ambalo ni mkataba wa mwaka mmoja.

Sasa kwanini nimekuja kwenu naona Kichwa kishaanza kuwaka Moto lastly week nimepokea Mshahara lakini Hauwezi Kuamini Jumanne umeisha Wote.

Kuna mwanamke Ambaye natarajia aje kuwa mke wangu nimemuweza Kwa biashara,ndugu wa karibu nimeweza kuwapa Pia.

Naombeni Ushauri nifanyaje mshahara ukae maana naona Tunakoelekea mkataba unaweza kuisha na Hakuna Cha maana nilichopata.

Wakuu mnisaidie mdogo wenu

Basics ni kama 950K
Hebu weka take home tuone ni ngapi na mchanganuo wa matumizi yako ndio tunaweza kukushauri vizuri. Umezungumza vitu too general. Mie nimeshindwa hata pakuanzia.
 
nashukuru mzima

Dah ok sawa, kama kijana mwenzako ambae pia niliwahi kupitia hali ya kuishiwa kabisa salary kabla ya date 10, wacha nikishauri kiasi.

1- kitu cha kwanza hakikisha watu na ndugu hawajui mshahara wako harisi (usiwaambie iwe siri yako), ila kama umeshawaambia then waambie mshahara umepunguzwa, kama take home ni 650, waambie take home sasa ni 450 then hiyo laki 2 ndio iwe pesa yako ya siri ambayo huitumii isipokua kuisave kila mwezi ambapo ukiwa serious in saving basi baada ya.mkataba wako kuisha utajikuta una 2.4M kama saving.

2-Na assume kama kijana wa Kiafrica lazima kuna matatizo mengine kufamilia (ni kawaida) ama pia sababu umepata kazi basi hata wazazi au mzazi atakutegemea kiasi flani, hapa fanya hivi, weka kiasi ambacho utakua unatuma nyumbani everymonth (only kama unajua mama yako anahitaji umsaidie kila mwezi) hapa nitakushauri elf 40.

3-Kwenye mahesabu yako fake ya 450k instead ya 650k utakua umebakiwa na 410k

*Kodi ya mahali unaishi.make sure haipiti 150 kwa mwezi.

*Nunua na lipia mahitaji muhimu ndani ya nyumba kama umeme, chakula (hapa nashauli chakula cha mwezi weka budget ya 70k na hii ikae kando kabisa ukishanunua mchele maybe 15kg, mafuta 5lt, unga 10kg, chumvi, maharagwe, inayobaki unaweka kwa ajili ya kubadilisha mboga na kubuy viungo.

4- hapo kwenye mahesabu yako fake utakua umebakiwa na 190k ama tuseme 180k sababu ya makato makato wakati wa kutoa pesa nk. sasa hii 190 ndio unaweza kutumia vile unataka ila kabla ya kuanza kutumia vile unataka make sure umeweka 70k kando kama nauli na food kazini. Hapo utabakiwa na 110k.

5-Hiyo 110k ndio sasa unaweza tumia matumizi yako, kuenjoy japo kidogo, voucher, kununua kitu umependa kama kiatu , nguo, kuhonga demu wako nk.

#So baada ya hayo yote kumbuka una ile saving yako ya 200k hii usiiguse, ila pia hii isikae tu kukonga umalize 12 Month,

Kama kijana mwenzangu nakushauri ingia vicoba, jiunge na vicoba , huko makazini kuna vicoba watu wanacheza, kuliko pesa yako ikae tu (pia ni risk sababu unaweza kuitumia muda wowote ukipata katatizo kadogo ama kuspend tu vibaya) hivyo ni bora kuiweka kwenye vicoba, huko utapata faida, pia huko unaweza kukopesheka hata ukafungua ka business ka maana kama side hussle, ama hata usikope just subiri tu mgawanyo baada ya kuvunja kikoba,

#Ushauri, hapa ingia vicoba ambavyo ni vya maana na watu wa kueleweka hasa wafanyakazo wa maofisini, usiingie vya waswahili mtaani sababu uaminifu mdogo, japo vicoba vingi sasa hivi vina uaminifi sana.

#Usiogope kucheza vicoba kudhani ni vya wamama, hapana, hata men tunacheza vicoba, watu wamejenga, wameanzisha biashara , wamenunua viwanja nk kwa pesa ya vicoba na wakati mshahara wake ni 300k per.month unashangaa anakiwanja , anakabiashara ni sababu ya vicoba, kama kijana unaeanza maisha na unakazi inakuingizia pesa, ingia vicoba utanishukuru after 11month iliobaki.

Shukrani. Japo nasisitiza, girlfriend hasomeshwi wala hafunguliwi biashara, kama unataka kumfanyia hayo yote mfanyr kwanza awe mke, hivyo kwenye nahesabu yako usihesabu kama mko wawipi hesabu uko peke ako ndio siri ya kufanikiwa, msaidie panapohitajika na mfanye ajue kua bado unahussle na mshahara ni kidogo, hakikisha unawaambia salary yako take hone ni 450 only, ingine ficha fanya savings kupitia vicoba. Mwakani utashangaa unasaving ya kutosha kuanzisga biashara nzuri ama kununua kitu cha thamani kama kiwanja etc kama Mungu atasaidia upate mkataba mwingine.

Sent from my vivo X6D using JamiiForums mobile app
 
Toa kwa wazazi tu utakuja nishukuru kama yupo mmoja jaribu kumpa kima chochote kwa mwezi demu fanyie mambo ya biashara either umemuoa au umemzalisha utakuja nishukuru

wengine chenga hata akikuambia kwa meseji mungu akubairiki haina matter ila wazazi ni jambo kubwa sna
 
Habari za siku wakuu.

Mimi Ni kijana wenu baada ya miahangaiko ya Kutafuta Ajira Mungu mwema mwezi huu niliingia mkataba na shirika Fulani ambalo ni mkataba wa mwaka mmoja.

Sasa kwanini nimekuja kwenu naona Kichwa kishaanza kuwaka Moto lastly week nimepokea Mshahara lakini Hauwezi Kuamini Jumanne umeisha Wote.

Kuna mwanamke Ambaye natarajia aje kuwa mke wangu nimemuweza Kwa biashara,ndugu wa karibu nimeweza kuwapa Pia.

Naombeni Ushauri nifanyaje mshahara ukae maana naona Tunakoelekea mkataba unaweza kuisha na Hakuna Cha maana nilichopata.

Wakuu mnisaidie mdogo wenu

Basics ni kama 950K
Jijenge wewe mwenyewe kwanza kiuchumi, ukija kufanikiwa utawawezesha wengine
 
Mshahara ni calculated kwa ajili ya mtu mmoja na sio familia na una lengo la kumfanya mwajiriwa asife yaani amudu kufika kazini kutumika. Akifika miaka 60 anatupwa anaajiriwa mwenye nguvu kwa circle hio hio. Mwajiriwa ni SAwa na limao lina thamani kabla alijakamuliwa
Duuuu,ngumu kumeza
 
Kuwa na roho ya ubahili, hakikisha laki 5 kwa mwezi unaweka akiba; zinazobakia tumieni kwa matumizi ya kila siku
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom