Nifanye nini kwa mwalimu huyu ninayemdai laki 4?

UMASIKINI BWANA

JF-Expert Member
Oct 17, 2013
942
566
Habari zenu wana jf!

Jamani nipeni mawazo nifanye nini kwa huyu Mwalimu wa shule ya msingi, mkoa na wilaya nahifadhi. Namdai laki 4 tangu mwez wa 3 nilimkopesha aende hospital huko Moshi, karudi kapona ananipiga tarehe.

Namheshimu naogopa kumuaibisha lakini nimesikia Waziri Mkuu atakuwa na ziara mkoa wa huyu mwalimu. Nimeamua nitamwambia majaliwa deni langu kwani hali ngumu sana na hanilipi au mwasemaje?

Afisa elimu wake kaniambia nimalizane nae yeye hana uwezo wa kumlipia.
 
Fungua kesi ya Madai Mahakama ya Mwanzo, usumbufu na haibu atakayopata mwenye atakulipa pamoja na gharama za kesi, najua kwako pia ni usumbufu lakini ni muhimu utaratibu kama huu uwepo wakati fulani. kumbuka hilo ni jambo binafsi hivyo usishitaki kwa watu ambao si wenye uwezo kisheria akiwemo Waziri Mkuu au Mkuu wa Mkoa.
 
dah we jamaa kwani haupo Tanzania? hujui hali ilivyo mbaya kwa wafanyakazi? hebu vuta subra kwanza ulimkopesha hela ya matibabu kwanini usisamahe tu!!

Mzee Magufuli hebu sikia hii, ile inkriment inahusika Hapa watu walipe madeni.
 
Kama mliandikishiana sehemu akatia na sahihi fanya kufuata sheria atakulipa lakini kama mlipeana vichochoroni hapo sahau kabisa!
 
Kama mliandikishiana sehemu akatia na sahihi fanya kufuata sheria atakulipa lakini kama mlipeana vichochoroni hapo sahau kabisa!
umemueleza jambo la msingi sana kama hamkuandikishiana mdai polepole tu manake anaweza kukuwahi mahakamani kuwa unamdhalilisha kisa amekataa kukupa penzi (sorry sijajua jinsia zenu lakini) na wale wa haki za binadamu wanaingilia unapotezwa usicheze na mwalim wewe
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom