Nifanye nini kuepuka tatizo la kutokujiamini na kushindwa kujieleza mbele za watu

Hii hali ipo kwa watanzania wengi sana na inachangiwa na utamaduni wetu. Tunafundishwa unyenyekevu na kujazwa inferiority angali watoto mwishoe tunakuwa followers tu na si leaders kwenye kila kitu.

Kwenye nchi za Magharibi college huwa kuna soma la Public Speaking kuwajengea wanafunzi uwezo wa kujenga hoja na kujileza mbele ya watu sina hakika kama bongo hili somo linafundishwa vyuoni.

Kutatua tatizo lako, maadam tayari unajua una hilo tatizo anza kupitia materials zinazohusu public speaking kuna machapisho na videos nyingi online kuhusu hilo, na jitahidi kuwa mchangiaji kwenye mazungumzo na watu wako wa karibu badala ya kuwa msikilizaji tu itakujengea uwezo na ujasiri wa kuongea mbele za watu.
Asante sana
 
Asante ndugu kufundisha ndo kipaji ambacho nilinyimwa maana huwa siwezi kurudia kitu kilekile mara mbili au tatu hasira zinanipanda
Ndugu hakuna anaependa kwenda hositali ila ni maradhi tu ndo hutupeleka huko.
Mi mwenyew kufundisha nlikuwa siwezi ila ndo ivo shida zikizid utafanya lolote hata kama hujui/hutaki.
Then ukishakuwa na madarasa yako mada utakayo fundisha leo sio utakayofundisha kesho.
 
naamini kama changamoto uliyonayo ni matokeo ya muda mrefu ambayo kwa sasa ndo inaonekana kama imepevuka ila nakushauri kama usikate tamaa, kwani mbuyu ulianza hata mchicha. Fuata njia zifuatazo zinaweza zikakusaidia
1.Amini kama unaweza kwa kile unachokwnda kukifanya mbele ya kadamnasi, mfano kama unakwenda kwenye interview jione kama ni mmoja wa wanaosailiwa pale na hakuna ugeni kati ya wewe na wao wanaokusaili
2.usihamishe mada nje ya kile ulichoiotiwa, kama umekwenda kwenye interview iaminishe akili yako kwamba hapa ni usaili tu na baada ya muda usaili unaisha na maisha yanaendelea.
3 Soma sana vitabu vitakuongezea confidence nakujifunza mbinu mpya za kuongea mbele za watu, ondosha haya kabisa kwani hazitokusaidia na zaidi zitakufanya uonekane kituko m bele ya jamii hii ya utandawazi
4.unapomwangalia mtu machoni usitathmini amekuangalia kwa jicho gani kwani kuna wengine hata akimwangalia mtoto huwa analia, sasa isiwe mtu anakuangalia kwa jicho baya ukaona kama anakuona unaongea pumba kumbe anakushangaa jinsi unavyomwaga materials ambayo pengine alishayasahau
5.kuwa halisi wewe ni wewe, usiongee kitu ambacho hukijui katika taaluma yako, sikiza swali kwa kituo kisha jibu kwa ufasaha

kila lakheri ndugu yangu ni vizuri pia ukawa unafuatilia kurasa za wanasaikolojia [pamoja na kujichanganya sehemu ambazo zinakuwa na watu wengi angalau kuzoea hadhira kwa kuanzia kabla ya kuanza kumwaga nondo kwa wasaili
 
Ukishasoma vitabu on public speaking, anza na yafatayo:-
  • Anza kuwa active jumuiya, kwenye vikao vya harusi au vya familia, kwenye ubishi vijiweni, kwenye kumbi za kuangalizia mpira, kwenye meetings za ofisini nk. Means kama kuna unachokijua hakikisha unakiwasilisha, mwanzoni ni shida ila unaanza hivyo hivyo
  • Usiwaze kuhusu uwezo wa wale unaowaelezea jambo, jiamini, elezea unachokijua.
  • Epuka kuongea huku ukiwaza kama hadhira imekuelewa au la, usiangalie reactions za wasikilizaji maana unaweza jikuta umeongezea vitu unnecessary.
Michango ya wadau wote ipitie, iko vyema sana ukiifanyia kazi.
 
Ukishasoma vitabu on public speaking, anza na yafatayo:-
  • Anza kuwa active jumuiya, kwenye vikao vya harusi au vya familia, kwenye ubishi vijiweni, kwenye kumbi za kuangalizia mpira, kwenye meetings za ofisini nk. Means kama kuna unachokijua hakikisha unakiwasilisha, mwanzoni ni shida ila unaanza hivyo hivyo
  • Usiwaze kuhusu uwezo wa wale unaowaelezea jambo, jiamini, elezea unachokijua.
  • Epuka kuongea huku ukiwaza kama hadhira imekuelewa au la, usiangalie reactions za wasikilizaji maana unaweza jikuta umeongezea vitu unnecessary.
Michango ya wadau wote ipitie, iko vyema sana ukiifanyia kazi.
Hakika nitafanyia kazi
 
Mimi nilikuwa na tatizo kama lako ila baada ya kusoma vitabu vinavyohusu maswala haya nikajua chanzo cha tatizo langu. Tatizo langu lilikuwa naongea kwa speed kali na inapelekea na kuwa na kigugumizi cha kutotamka maneno vizuri na kupoteza confidence.
Wajuzi wa Public Speaking wana kamsemo chao cha kimombo "if you speak slowly, the stammering goes away" .

Kama mpenzi wa Movie, tafuta Movie inaitwa ``The King`s Speech" inayohusu kiongozi wa England's Prince Albert (Colin Firth) alikuwa na tatizo la kutokuwa na Confidence na kushindwa kutoa Speech kwa wananchi wake, tatizo linalofanana na lako na jinsi alivyoweza kulikabili na kufanikiwa.
 
Huna Tofauti na Nilivyokuwa Mimi hapo mwanzoni..! Najipang ila Nikipewa fursa ya Kuongea yote nayasahau..!
Ila Mm nilikuwa mtu wa Kujitenga sana na Watu.
Kikubwa ndg jaribu Kujichanganya Na Vijana wenzio Mtaani, kwenye Draft au bao, Michezo mpilani, Jiunge na Jorging za Mtaani kwako.
i.Unawez Ukatumia watt kujijengea Ujasiri wakusanye baadhi arafu Ujitahidi kuongea nao kwa kuwafundsh kwa masimulizi ya hadithi au Matukio...
ii. Ukifanikiwa kwa watt watafute watu wa watoti hata wa Sekondari Jaribu kuwa fundisha kitu kuhusu maisha..
iii.Jikubali, Kuwa na Ujasiri, Ukiwa unaongea Usiwe unafikiri yale maneno yako, Thubutu.
Ukifanikiwa hatua hizi Jaribu siku Moja hata Kanisani kama ni Mkristo kwenda mbele kutoa Shukrani Kwa MUNGU kwa jambo lolote,..
3. Ukiwa Unaongea mbele za watu husiwaangalie watu husoni Unawez ukawa unatumia sekunde chachechache ukiwaangalia Vichwa vyao tu, Kingne ukiwa unaongea mbele za Watu husiangalie kama kila unachoongea kinawagusa au wanakiielewa, husimtafute sura ya Mtu unayemjua ukiwa unaongea.


Sent using Jamii Forums mobile app
Airwing amesema vizuri. Ukweli sio tatizo lako pekee hata mimi tatizo hili lilinitesa sana hadi nilipogundua kuwa linatokana pia na kutokuwa na exposure ya kuzungumza mbele za watu. Unajua watu wengi wanafikiri kuzungumza mbele za watu ni rahisi, mpaka upate exposure kama hujawahi ni vigumu sana.

Pia wanadamu tunatofautiana kwenye awareness zetu. Jifunze taratibu "kujisau" unapokuwa mbele za watu na ku-concentrate kwenye mazungumzo. Usijiweke wewe kama center of attention. Usiwaangalie sana watu usoni kila wakati, tumia mda mfupi kuwaangalia wachache, mda mrefu angalia kwa jumla jumla tu mfano juu kidogo ya vichwa.

Anza kujenga kujiamini na hadhira ndogo. Mfano watu wa chini ya umri wako. Jua kwamba uwezo wa kuzungumza mbele za watu unahitaji training kama vile kucheza mpira, kuruka sarakasi, nk huwezi kuruka sarakasi kwa kufikiri tuu kichwani inabidi uruke ndio utajua ni namna gani ya kufanya hadi unapata staili yako.

Kamwe usiige namna ya mtu mwingine ya kuongea, itakuwa ngumu sana, tafuta ile namna yako ya asili na itumie hiyo.
 
Habari zenu wana JF

Nimekuwa na tatizo la kushindwa kujieleza mbele za watu hasa watu ambao sijawazoea pia inaniwia vigumu kuongea na mtu ambae sijamuzoea.

Hili tatizo ninalo toka nijitambue pia nashindwa kujiamini sehemu muhimu kama kwenye usaili kitu ambacho kinanifanya nakosa nafasi za kazi kwa kutojiamini na kutojieleza vyema japokuwa ninauelewa na kazi husika.

Hii hali imekuwa ikinitesa sana kiasi kwamba kuna muda nikifikiria ninavojieleza mbele za watu mi mwenyewe napata aibu

Tafadhali naombeni msaada kama kuna mtu mwenye uelewa na hili tatizo linalo nikabili.

Natanguliza shukrani zangu
Ungejaribu kuwaona wana psychology watakusaidia kubuild self-confidence yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nje ya box

Hapo wakubwa tu ndo tunaelewa jamaa yetu shida yake kubwa ni nini !!

"shikamoni wanawake wote duniani#

cityzen chairman am here
 
Back
Top Bottom