Nifanye nini ili mpenzi wangu aniamini.....

simba29

Senior Member
Jun 22, 2011
193
67
Nampenda sana huyu msichana <mwanamke> lakini kila ninachofanya naona yeye hana imani na mimi............nimemvisha pete,lakini bado anahsi nitamuacha.....tatizo ni kuwa ANAHISI IPO SIKU NITAMUACHA NA KUWA NA MPENZI MWINGINE...
Nifanye nini wajameni....i lv this gal...
 
isije ikawa mapenzi ya upande mmoja .. tatizo wengi tunaamini kwa kusema au kumwambia mwenzi wako nakupenda lakini mara nyingi maneno yake hayaendani na uhalisia wa mapenzi .. sana sana utatamka maneno yote matamu lakini nia na madhumuni ya hayo maneno ni kumvua chupi mwanamke na ukimaliza hata maneno hupungua
 
Kama kweli unampenda kwa dhati, piga chuo mjomba hana imani na wewe akitokea mwingine akamuamini utaisoma namba!!!!
 
Kama kweli unampenda usimchezee kabla ya ndoa na jitahidi umuoe mapema iwezekanavyo.
 
Amekwishakuwa mtu mzima sasa,kwa nini hataki kujiamini?Hebu mwabie ajiamini na akiamini kile unachokisema!Ila na wewe pia jaribu kumaanisha sio kuigiza.
 
keshaumizwa sana huyo ssa hv hata nyasi anahisi nyoka, mhakikishie unampenda kwa kumwondoa wasiwasi
kuwa nae muda mwingi na mambo ya simu yale uwe free, yaan unaweza hata kumpa simu ukaenda kuoga
kama mmekaa mahali mnapata hata dinner mpe simu maana mambo yote siku hz simu tu
 
Pete kitu gan bwana. Watu wanaoana leo kesho wanaachana. Kama hakuamin mpe ukweli kwa sababu huwez kuwa mtu wa mashaka daily . Kama anaendelea tafuta mwingine mabinti wapo wengi mkuu
 
Kumvisha pete sio kigezo cha kuaminiwa,unavisha pete miaka inakata ya nn sasa,wengi wamevishwa na wameachwa hawakuolewa na mwingine juzi kati kaachwa baada ya send-off,cha msingi kama unampenda kweli funga naye ndoa apate haki miliki ya mume na mapenzi yenu na pia atakuamini tu!matapeli wamekuwa wengi siku hizi.
 
Hey jalibu kuwa naye karibu karibu na kumpa v2 anavyopenda na kumcare kwa umakin sn atakuamin sn na atakupenda na ata kuamin hey fanya ivyo utawin
 
Kumvisha pete sio kigezo cha kuaminiwa,unavisha pete miaka inakata ya nn sasa,wengi wamevishwa na wameachwa hawakuolewa na mwingine juzi kati kaachwa baada ya send-off,cha msingi kama unampenda kweli funga naye ndoa apate haki miliki ya mume na mapenzi yenu na pia atakuamini tu!matapeli wamekuwa wengi siku hizi.

Cantalisia umenikumbusha mbali sana...........kuna njemba alifanya madudu ya kumvisha mtoto wa watu kibati halafu akakaa miaka..............binti wa watu akaja kumshtukia.........................akadai hivi huu uchumba wa kuvishwa kibati ndiyoharusi au vipi...............alipotokea njemba ambaye yupo makini binti akamrushia njemba kibati chake akaishia na jamaa yake mpya kusikojulikana.........
 
Afadhali na ww umeliona, pete tu sio ishu kbs cku hizi,mtu ukiamua funga ndoa ueleweke basi!
 
Kumvisha pete sio kigezo cha kuaminiwa,unavisha pete miaka inakata ya nn sasa,wengi wamevishwa na wameachwa hawakuolewa na mwingine juzi kati kaachwa baada ya send-off,cha msingi kama unampenda kweli funga naye ndoa apate haki miliki ya mume na mapenzi yenu na pia atakuamini tu!matapeli wamekuwa wengi siku hizi.

umeona eeh! A friend of mine alivishwa pete, mara akagundua jamaa ana mtoto nje na akuwahi kumwambia, bidada akaona hakuna shida maana mtoto alizaliwa kabla hawajawa wapenzi. Heee!, baada ya muda akagundua katoto kengine tena hako kalizaliwa wakati penzi lao lipo moto moto. Dah, wanaume wabaya jamani.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom