yahoo.com? Mmmh
Wana jamvi naomba anayejua procedure za kufungua Microfinance Company anisaidie
WanaJF me ni mjasiriamali ambaye baadae nina malengo yangu mengi moja wapo ni kuanzisha Microfinance yangu ila nahitaji kujua natakiwa kuwa na capital kisasi gani ili niweze kufanya hii BUSINESS, ASANTENI
Habari,ni vyema mkaweka dondoo za msingi mf,minimum unatakiwa uwe na kiasi gani?Au ni vitu gani vya msingi unatakitiwa kwanza kuwa navyo,thanks
1 - Ni lazima ufungue na kusajili limited company.
2 - Uwe na mtaji wa kutosha ili kuweza kukopesha. ( milioni 50 na kuendelea)
3 - Uwe na ofisi na watendaji wenye uzoefu.
4 - Uandae taratibu na kanuni utakazotumia ktk kutoa huduma hiyo.
5 - Anza kujitangaza na kutoa huduma.
NB: Katika kusajili, unaanza BRELA , kisha unaenda TRA, kisha wizara ya viwanda na biashara, kisha BOT.
Hivi wana jamvi samahanini ninaweza kuanzsha microfinance kwa mtaji wa kiasi gani kwa kuanziya then baadaye ndo ujikuze wenyewe mtaji wangu koz karibia namaliza chuo so nataka nijiajiri mwenyewe plz naomba msaada kwa hilo kwa wote wenye experience na hyo kitu[/QU
Kwa hyo bandugu hakuna mtu ajuae?
Mkuu,..kwa ufahamu wangu..
Microfinance haiwi Governed na BOT kwa sababu haichukui customer deposits..inakopesha tu..
Taratibu za kuanzisha:
-Register kampuni kwa njia ya kawaida kabisa (peleka Memarts BRELA, pata TIN number toka TRA..etc)..lawyer mzuri anakufanyia hivi vyote kwa cost isiyozidi 1m
-Pata leseni kutoka wizara ya viwanda na biashara (Sio BOT!!!)
Anza biashara!!..as far as I know, hakuna minimum capital inayotakiwa, wala deposit huko BoT kwa sababu risk ni ya pesa zako mwenyewe na sio za kuchukua kwa wananchi...hapo baadaye unaweza kuzishawishi benki zikakukopesha pia...kama biashara nyingine...