Nifanye biashara gani ambayo naweza kuingiza laki moja kila siku

Manzile

JF-Expert Member
Apr 23, 2020
344
1,000
Milioni 20 jenga vyumba 20 vya kupangisha,
Chumba simple cha kupangisha mpaka kukamilika ujenzi ni 1mil × 20 = 20mil.

Ni chumba simple,
Ukihitaji vyumba classic vitapungua idadi.

Fundi ninaye.
milion 20 vyumba 20? hauko serious mkuu.

nimejenga msingi tu ni zaidi ya 27m, mpaka sasa nimetumia 120m+ nyumba ndio nimepiga plasta,
hapa uangalizi ulikuwa wa hali ya juu, kama kuna wizi ni asilimia ndogo sana.

Huo ujenzi wa 20m kwa vyumba 20 ukoje?
 

aise

JF-Expert Member
May 16, 2018
2,892
2,000
milion 20 vyumba 20? hauko serious mkuu.

nimejenga msingi tu ni zaidi ya 27m, mpaka sasa nimetumia 120m+ nyumba ndio nimepiga plasta,
hapa uangalizi ulikuwa wa hali ya juu, kama kuna wizi ni asilimia ndogo sana.

Huo ujenzi wa 20m kwa vyumba 20 ukoje?
Wewe umejenga nyumba,
Mimi nimeshauri ajenge vyumba,
Huoni utofauti hapo?
Isitoshe komenti yangu imejitosheleza kuwa ni vyumba simple tu, havijapigwa plasta, havina aluminium windows etc.

Sasa inaonekana wewe umejenga nyumba, ambapo kuna korido, vyoo vya ndani, sebule, jiko, dining, vyumba vyenyewe, etc.
Kwahiyo usikatae, chumba cha kawaida mpaka kikamilike wastani 1m.
Kinakuwa chumba ambacho unaweza kukipangisha.

Kama huamini lete kazi.
 

Bushmamy

JF-Expert Member
Aug 18, 2019
7,324
2,000
Wewe umejenga nyumba,
Mimi nimeshauri ajenge vyumba,
Huoni utofauti hapo?
Isitoshe komenti yangu imejitosheleza kuwa ni vyumba simple tu, havijapigwa plasta, havina aluminium windows etc.

Sasa inaonekana wewe umejenga nyumba, ambapo kuna korido, vyoo vya ndani, sebule, jiko, dining, vyumba vyenyewe, etc.
Kwahiyo usikatae, chumba cha kawaida mpaka kikamilike wastani 1m.
Kinakuwa chumba ambacho unaweza kukipangisha.

Kama huamini lete kazi.
Wewe nawe ulikuwa unajidai darasa la saba? Thubutuu yako
 

aise

JF-Expert Member
May 16, 2018
2,892
2,000
Wewe nawe ulikuwa unajidai darasa la saba? Thubutuu yako
Mimi nilisoma mpaka darasa la saba.
Bahati mbaya sana hata mtihani wa kumaliza darasa la saba sikufanya.
Ila kama huamini, mimi sina uwezo wa kukulazimisha.

Mtaani nimejifunza mambo mengi sana, nadhani hata kuwazidi baadhi ya wasomi.
Tangia nilipochaa shule, nilienda kuishi maisha ya mtaani mbali na nyumbani, nikiwa kama chokoraa.
Niliona mengi, nilijifunza vitu vingi, mpaka leo niko mtaani naendelea kujifunza.
Kitu nilicho jaribu kuelezea hapo juu nimekishuhudia, maana nimejiingiza kwenye inshu zinazohusu ujenzi.
Mimi naamini kuna watu wengi sana wenye uwezo sana kuzidi mimi na hawajasoma hata kufikia la saba.
 

Ngajilo255

Member
Jul 8, 2020
56
125
Chukua milioni 10 fungua fixed akaunti NMB.
Milioni 10 iliyobakia nenda Silverland Tanzania/Silverland Dar nunua vifaranga aina y SASSO 1000 kila mmoja ni 1400, wafuge ndani ya miezi minne watakuwa wamekuwa wakubwa kweli kweli utauza kwa 15,000 au 20,000 kwa mmoja.
NB: SASSO ni kuku chotara wanaovumilia magonjwa na hali ngumu zote.

Gharama ya kuwahudumia SASSO 1000 pamoja na banda, madawa n.k havitazidi hata milioni 5.
Pia jifunze formula ya kutengeneza chakula cha kuku wewe mwenyewe ili kupunguza gharama.
Akishaanza huo ufugaji anitafute nimtengenezee machine ya kuchanganya vyakula vya kuku.

#Ngajilo255
 

Ngajilo255

Member
Jul 8, 2020
56
125
Amina. Kuwa makini na hao wanaokuita PM. Waambie kama wana ushauri wautoe hapa tuupime.

Wengi ni matapeli, wengine wanatumia hadi dawa ukikutana nao tu utawapa hela zote bila kujijua akili zinarudi hela zimeshaenda. Yamewakuta wengi.
Duuuuuuuh kazi ipo kwa kweli.

Ila sio wote wenye lengo kama hilo.

Fursa zingine unakuta ni maelezo mengi ukianza kuongea na kuielezea inaweza chukua hata dk 60+ .

Sasa maelezo ya dk60+ yanaweza geuzwa kwenye mawndishi itakuaje???

Bila shaka kitakua ni kitabu kizima. So, la msingi tunasema ifika wito kataa maneno.

Nenda PM huku ukiwa na Mungu wak akusaidie usilizwe.

#Ngajilo255
 

Kipangaspecial

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
14,770
2,000
Laki ni net income manake profit (faida) au? Biashara ya laki moja faida kwa siku manake 3 million tshs faida kwa mwezi zipo nyingi tu lakini ujue inaweza kukuchukua hata miaka mitatu tokea biashara ianze hadi upate hio faida ya 100k kwa siku. TANZANIA YA LEO NGUMU SANA KUANZISHA BIASHARA LEO HALAFU BAADA YA MWEZI MMOJA ETI UONE FAIDA YA 100K KWA SIKU. Lakini ukipata Location nzuri sana kama city center, ukawa na product nzuri sana watu wanayoihitaji, na ambapo una supply chain nzuri ambapo product unaipata kwa bei ndogo ya wholesale, na ukasimamia MWENYEWE kuondoa wizi, INAWEZEKANA SANA.
Hivi si wapo machangudoa wanaoingiza zaidi laki moja kwa siku, kwanni jamaa hasijiingize kwenye hiyo business
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom