Nifanyaje mke wangu apunguze wivu? Ananikondesha sana


Veyron

Veyron

JF-Expert Member
Joined
Feb 6, 2012
Messages
509
Likes
289
Points
80
Age
27
Veyron

Veyron

JF-Expert Member
Joined Feb 6, 2012
509 289 80
Nampenda sana mke wangu ila cha ajabu haniamini kabisa mi nampenda. Ninamwambia kila siku vile nampenda hanielewi. Amekuwa akinifuatilia hadi ofisini. Na akifika hataki hata kuongea na secretary. Ni moja kwa moja anakimbilia niliko na kushika simu yangu.

Boss ameshaniambia sio vizuri eneo la kazi kufanya hivyo ila huwa ye haelewi. Nami nilishamwambia hilo hataki kuelewa. Sasa kumfukuza siwezi na kumwacha siwezi ila natafuta njia ya kuweka mambo sawa awe mpole.

Kwani tatizo nini mtu kuwa na mtu wa pembeni alafu akawa hamjali na anakujali wewe tu. Cha msingi wewe ndo mke halali na si mwingine na wewe ndio amekutambulisha hajatambulisha mwingine. Yani tatizo linakuja wapi enyi wanawake mnaokuwa na wivu wa namna hii usio na maana.?

Wanawake badilikeni na muende na wakati kuna mabadiliko mengi yanayowatokea ambayo lazima muelewe kuwa yatamtesa umpendae .

Nyakati za mwanamke anapokuwa mjamzito ni nyakati ngumu sana kwa mwanaume. Kwasababu itamlazimu akae kipindi kirefu bila kufanya tendo pendwa na mke wake (najua mnajua)

Sasa kuna wanaume wanaoweza wengine hatuwezi kiukweli ni swala la kuelewa na wakati mwingine kunishauri nifanye kwa uangalifu magonjwa ni mengi. Sio kuanza kukurupuka kugombana na majirani unaowakuta na mimi, unanifanya naonekana sio mwaminifu kwa mke wangu.

Ni swala la nyakati ulionayo ndio linasababisha yote haya ukisharudi kwenye hali yako ya kawaida maisha yanaendelea kama kawaida na mambo yatakuwa sawa. Inamaana nivumilie muda wote huo asee miezi kama tisa hivi ni mambo ya kizamani kiukweli nimeshindwa.

Unakuta kuna nyakati zinafika unasikia hamu mpaka mwili unatetemeka asee. Tena kama vijana tuliowahi kuoa tunateseka sana katika wakati huu. Aseee mi naomba mke wangu anisamehe na anikubali tu bado upendo uko kwake.

Nawashauri tu wanawake wapendeni waume zenu na mkubaliane na hali halisi wakati mwingine majaribu yanazidi kipimo.

Kwa wanaume nipeni ushauri tu niweze kuwa na mama watoto muda wote asinione namsaliti ajue bado mi ni wake tu na asijali kuhusu mambo mengine.
 
adden

adden

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2015
Messages
4,640
Likes
6,069
Points
280
adden

adden

JF-Expert Member
Joined Dec 27, 2015
4,640 6,069 280
Hiyo dawa ya kumtuliza ukiiipata utanipatia na mi
 
D

Dorrlyn

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2017
Messages
543
Likes
599
Points
180
D

Dorrlyn

JF-Expert Member
Joined Jan 10, 2017
543 599 180
Mleta mada una umri gani? Ulifundwa kweli wewe? Mke akiwa na mimba kama hana shida yoyote mnafanya mapenzi mpk anaingia labour.
Halafu mwambie mkeo abadilike na si wanawake wote maana wengine tuko na moyo mmoja hatutaki stress za kufuatilia watu tuliokutana nao tukiwa na meno 32. Halafu pia na wewe nakushauri ukubaliane na hali halisi maana hata sisi wanawake tuko na majaribu mengi tu kama hujui usifikiri ni nyie tu mnamajaribu.
 
bandamo

bandamo

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2017
Messages
1,961
Likes
1,339
Points
280
bandamo

bandamo

JF-Expert Member
Joined Aug 5, 2017
1,961 1,339 280
Umezidisha upole tangu mwanzo wa mahusiano yenu kuzuia ufanye kazi ya ziada 1 marufuku mke kukufuata kazini ile ni dhamana tu umepewa haina uhusiano na mke 2 muda wa kuingia ndani usijulikane (random time) 3 uchague kazi au mapenzi kubeba vyote umeshindwa. huyo atabadilika ukitepeta anakupanda kichwani utapoteza kazi
 

Forum statistics

Threads 1,236,125
Members 474,999
Posts 29,247,530