Nifahamisheni madaraka ya Waziri na viongozi wengine kumuweka mtu mikononi mwa polisi

Zygot

JF-Expert Member
Apr 14, 2016
2,240
2,866
Nijuavyo, Rais, wakuu wa mikoa na Wilaya wanayo madaraka kisheria kumuweka mtu mahabusu. Lakini, inakuwaje waziri anatoa amri kwa polisi kumkamata raia yeyote, popote?

Nauliza baada ya kusikiliza waziri Mwakyembe akitoa amri ya kukamatwa kwa 'Dudu baya' kwa sababu ya kutaja maovu ya Ruge (RIP). Nilidhani Polisi wenyewe ndo wana uwezo wa kuchukuwa hatua kama hizo kulingana na taaluma yao ya usalama, lakini hapa ni waziri tu! Kwa akili yake.

Naomba kuelimishwa maana hii siyo mara ya kwanza. Kokote ktk ziara za mawaziri, wanatoa amri za aina hii.
 
Jamani nisaidieni maana baadaye hata Mbunge atatamka mwananchi kuwekwa ndani.
 
Back
Top Bottom