Nietzsche: Namchukia Mama yangu. Sitaki hata kusikia sauti ya dada yangu

elishaezekiel

JF-Expert Member
Oct 16, 2016
563
1,461
Ni maneno ya Friedrich Nietzsche, Mwana falsafa wa Kijerumani ambaye alizaliwa Mwaka 1844 na kufariki mwaka 1900.

Aliawahi kuwa mkuu wa Chuo kikuu cha Basel ujerumani kabla hata hajahitimu masomo yake ya Phd, jina lake lilipendekezwa na Mwalimu wake.

Kauli nyingine za Nietzsche ( tamka Niiche) ni:
1. Mungu amekufa na Sisi ndio tuliomuua ( God is dead and we have Kiled Him)
2. Nawachukia watu, Nimewachoka watu puuu!! (I Hate my fellow man, we are tired of man )
3. I hate the New Testament of the Bible!!( Nalichukia agano jipya.
4 Katika agano jipya lote mtu anaestahili kuheshimiwa ni Pontiko Pilato, Gavana wa Kirumi!!

Nietzsche ameandika vitabu vingi ikiwemo The Antichrist; Human, all too human ; Beyond good and evil nk

Hakuoa na aliamini watoto ni mzigo na Mapenzi ni kamba zinazomnyima Mtu uhuru wake.

Nietzsche aliwahi kusema Watu wote wanaotaka uhuru wa Nafsi hawapashwi kuoa maana ni kujitwika majukumu yasiyo ya lazima. Wanafalsafa wengine ambao hawakuahi kuoa ni Plato, Aristotle, Zeno wa citium aliyeanzisha ustoa ama Stoicism,Galileo, Isaac Newton, Buddha pamoja na Pythagoras.

Buddha alimwacha mke wake na watoto ili kuisaka Enlightenment (Nirvana) Buddha alisema baada ya kuwa mtoto wake kuzaliwa “ Huu ni mnyororo, mnyororo wa kunifunga umezaliwa nyumbani kwangu “

Alisomea elimu ya dini pamoja na philologia kabla ya kuhamia na kujikita katika historia ya falsafa. Nietzsche, Aliuponda sana ukiristo akiamini unatoa Watu dhaifu wa kulia lia tu. Alisema analipenda agano la Kale kwa sababu Lina wanaume wa Ukweli Siyo agano jipya liliojaa watu ombaomba na wasio na akili. Huyo ndo Nietzsche bana
 
Mwishoni mwa maisha yake, alikuwa schizophrenic au chizi aka kichaa.

Aliugua kaswende akapata complications ama tertiary stage miaka mingi baadae. Aliipatia jeshini kipindi ameenda kujitolea kama mhudumu wa afya kwa askari wa kijerumani. Kwa hivyo haikuwa schizophrenia as it is but neurosyphilis iliyompelekea kuugua akili yake. Maneno yake ya mwisho yalionesha alikuwa mtu ambaye akili yake ni nzima isiyo na kichaa!!

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Yeye mwenyewe ni mfano mzuri wa watoto ambao ni mizigo.

Sasa mtu ambaye anaona watoto ni mizigo, haoni umuhimu wa ndoa, inamaana hafikirii hata yeye angepatikana vipi kama wazazi wake wangekuwa na mtazamo kama huo.
 
Kaswende aliipataje? Kwa Ngono bilashaka? Kama niko sahihi niendelee nanilichokiwaza.
 
Huenda alijuwa hilo ndio mana akaja na wazo Hilo.

Kimsingi ukitafakari nadharia yake utajuwa ni ukweli mtupu, lakini kwa watu dhaifu.

Watu walio majasiri huwa wanapambana kwelikweli, ndio sie tunaotunza Familia zetu kwa mapambano.
 
Umesema kweli.

Wanaume tunatakiwa tupambane, na kukubali kuwa jukumu la kutunza familia ni letu, kama tusipo zitunza sisi unadhani ni nini atafanya hivyo.
 
  • Thanks
Reactions: dtj
Yeye mwenyewe ni mfano mzuri wa watoto ambao ni mizigo.

Sasa mtu ambaye anaona watoto ni mizigo, haoni umuhimu wa ndoa, inamaana hafikirii hata yeye angepatikana vipi kama wazazi wake wangekuwa na mtazamo kama huo.

Swala la yeye kuzaliwa lipo nje ya uwezo wake. Hata kama asingezaliwa ni sawa tu haina tofauti. Kuhusu watoto wake yeye mwenyewe hilo lipo ndani ya uwezo wake ndio maana akaona Kuzaa hakuna maana.

Kama huwezi kufanya jambo lisilo na manufaa kwako, inakufaidia nini wewe ambaye utakufa kuzaa na kuhangaikia watoto ambao hata wao watakuja kufa baadae!!

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Yote tisa, ila huyo aliesemuita mtoto 'mnyororo' ni kitobo. Huyo mtoto alijizaa au mkewe alijinanii mwenyewe?

Sent using Jamii Forums mobile app

Buddha alikuja kufahamu maana ya maisha akiwa kaoa ndo maana akasema hivyo. Iweje ujihangaishe na mambo ambayo kimsingi baadae yanakosa maana ukitatazama kwa mapana yake ( in broad Perspective)!

Kama unajua kwa undani kabisa kuwa utakufa siku moja na kila Mtu atakufa siku moja na watoto wako watakufa siku moja kwa nini uhangaike na kupambana? Buddha wazazi wake hawakujua undani wa haya maisha ndo maana wakamzaa!!

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Huenda alijuwa hilo ndio mana akaja na wazo Hilo.

Kimsingi ukitafakari nadharia yake utajuwa ni ukweli mtupu, lakini kwa watu dhaifu.

Watu walio majasiri huwa wanapambana kwelikweli, ndio sie tunaotunza Familia zetu kwa mapambano.

Mkuu kupambana sana in broad Perspective kunakufaidia nini??

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
  • Thanks
Reactions: dtj
Swala la yeye kuzaliwa lipo nje ya uwezo wake. Hata kama asingezaliwa ni sawa tu haina tofauti. Kuhusu watoto wake yeye mwenyewe hilo lipo ndani ya uwezo wake ndio maana akaona Kuzaa hakuna maana.

Kama huwezi kufanya jambo lisilo na manufaa kwako, inakufaidia nini wewe ambaye utakufa kuzaa na kuhangaikia watoto ambao hata wao watakuja kufa baadae!!

Sent from my iPhone using JamiiForums
Kumbe! mtazamo wake finyu ulianzia kwenye kutokuona umuhimu wa yeye kuzaliwa.

Basi kwa mtazamo kama huu, haishangazi kwa yeye kuwa na nadharia za ajabu ajabu kama hizo.

Kwa sababu mtazamo wake ameujenga katika msingi mbovu.
 
Kaswende aliipataje? Kwa Ngono bilashaka? Kama niko sahihi niendelee nanilichokiwaza.

Mkuu kumbuka penicillin ilikuwa haijagunduliwa kipindi hiko na mtu kuvuka ujana haijakupata ilikuwa bahati sana. Kumbuka pia mazingira na namna ya kupigana vita kipindi kile.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
  • Thanks
Reactions: dtj
Mkuu kumbuka penicillin ilikuwa haijagunduliwa kipindi hiko na mtu kuvuka ujana haijakupata ilikuwa bahati sana. Kumbuka pia mazingira na namna ya kupigana vita kipindi kile.

Sent from my iPhone using JamiiForums
Mkuu!

Unajibu kwa uweledi Sana! Nimekuelewa Asante pia.
 
Back
Top Bottom