NANDERA
JF-Expert Member
- Mar 18, 2014
- 2,024
- 2,488
Kuna harakati zinaendelea katika baadhi ya serikali za mitaa hapa dar labda na mikoani za kuhakiki nyumba za kuishi ili wamiliki walipe kodi stahiki. Hapa namaanisha nyumba uliyoijenga mwenyewe kwa fedha zako za mkopo, au za wizi au za kudunduliza au za ziada au ya urithi, au ya kununuliwa na "msamaria mwema" unaishi wewe na si umepangisha. Nimesikia watu wakilalamika huko changanyikeni kuwa wamekadiriwa kodi kubwa sana na kuna siku 30 za kuhakiki.
Najua kodi hii si ngeni duniani ila hapa kwetu ni ngeni. Tumezoea kulipa kodi za ardhi na za majengo ya biashara. Kwa hiyo hata viwanja vyenye hati tulimojenga nyumba zetu huwa tunalipia kodi ya ardhi. wataalamu wa kodi au wanasheria mnisaidie kuelewa dhana ya kodi kuhusiana na jambo hili.
Vigezo vya ukadiriaji ni vipi? Naomba kujua ili nijenge nyumba nitakayotozwa kodi kidogo.