Nimeona tangazo la NGO ya Tanzania social support foundation, kuwa wanatoa ufadhili na mikopo kwa wanachuo wa vyuo vya elimu ya juu.Ili maombi yako yaweze kuhalalishwa inabidi muombaji aambatanishe kiasi cha fedha taslim SHS.50000/=.
Je hii NGO wafadhili wao ni kina nani? tovuti yao haionyshi nani ni wafadhili wa NGO hiyo!
Nimejiuliza kuwa NGO hii haiwezi kutumia fursa ya tatizo la ukosefu wa mikopo na kuja na mbinu ya kutoa scholarships za elimu ya juu kwa lengo la kujinufaisha? Fikiria mfano wakiomba wanafunzi 3000 nchi nzima X shs.50,000=150,000,000. Wakiweza kutoa 50,000,000 wakafadhili baadhi tu ya walioomba itahalalisha malengo ya taasisi wakati ikibaki na 100,000,000/=.
Naomba nisieleweke kama nina mtazamo hasi kuhusu malengo ya TSSF, ila ni swali fikirishi ili isije kuwa ni mbinu ya kujipatia kipato kwa kutumia fursa ya mbinyo kwa watanzania wanaohaha hasa kipindi hiki ambapo mikopo ya elimu ya juu imekuwa ni shida. ni mawazo yangu tu jamani silengi kumkwaza yeyote.